Sasa hivi kumkopa au kumkopesha mtu ni kutaka kuvunja urafiki

Sasa hivi kumkopa au kumkopesha mtu ni kutaka kuvunja urafiki

Kuna mchiz wangu tumejuana since form 1
Alilia shida, nikamtoa 100k

Sasa navyopigishwa chenga[emoji119]. Uzuri wake najua tu atanilipa

Nimepanga akinilipa tu, namchana live. Ushikaji uendelee ila nisisikie habari za kuazimana pesa
Mwanangu ucmalumu mchizi na endelea kumpiga jeki! Mkuu hali ni mbaya saaaan amin kwamba
 
Wajameni, hali ni ngumu.
Nina ndugu, jamaa na marafiki amabo kila kukicha ni kutaka kunikopa.
Tatizo ni moja tu, ukimkopesha mtu sasa hivi stress inahamia kwako.

Kumfuatilia mtu uliyemkopesah ni shughuli pevu.
Mara simu haipatikani, amekublock!

Sasa tufanyeje wajameni , tuingie ugomvi wa kutomkopesha mtu, tuanze uadui, au umkopeshe mtu na asilipe tuanze uadui?
Na hapo si kwamba mimi sina shida, ila ni kiongozi wa ukoo fulani wenye ng'ombe wengi!!!
Fact sana ndugu maisha yanalazimisha ivyo
 


Sasa huu ni moja ya mikasa ya kumdai mtu.
Unamwona lakini anajificha.
 
Kweli kabisa unachosema mimi nadai karibia laki 4 kwa watu wa karibu mpaka nimeamua kusamehe ila nimejifunza

Mmoja namdai elfu 30 na anafanya kazi

Mmoja ni mjomba wangu namdai laki 1.5 anafanya kazi

Mwingine namdai 1.6 huyu ni rafiki yangu

Mwingine namdai elfu 60 ni jirani yangu

Nimeacha kukopesha sasa hivi mtu akipiga simu nasema nyumbani kuna mgonjwa au kumetokea msiba imeisha hyo nimejifunza sirudii tena ujinga.
 
Back
Top Bottom