Sasa hivi kwenye soka kazi ya supporting striker/ Play maker / namba 10 imekufa

Sasa hivi kwenye soka kazi ya supporting striker/ Play maker / namba 10 imekufa

Nikiwa mdogo nilikuwa natamani kucheza namba 9 kama Ronaldo de Lima wa Brazil au namba 7 ya David Bekham 😀
 
Tatizo hii nafasi lazima uwe na Creativity, vision, ball control, passing ability, good 1v1, some pace. Hivi vitu kuwa navyo vyote si mchezo, watu kama Lionel Messi ndo wanavyo vyote hivi vitu ndio maana unaona kama nafasi imepwaya lakini wapo sema hawana vyote hivi, mfano mwingine wa karibu kabisa na unao fit vizuri Kwa sifa za hii position ni yule dogo wa Bayern Jamal musiala, wapo wengine pia... Binafsi Sasa hivi tunahitaji sana namba Tisa natural hakuna wale top quality, Mimi nashangaa siku hizi ukiambiwa huyu ndo standing striker wetu utashangaa, kulikuwa na kina Marc Van basten, likisimama hapa ukilipa pasi hata kama mpira upo kwenye position gani lazima atie nyavuni, anafunga Kwa vichwa, miguu Hadi na makalio.
 
Back
Top Bottom