Sasa hivi sitalilia tena mapenzi na hii ndio sababu!

Sasa hivi sitalilia tena mapenzi na hii ndio sababu!

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
36,625
Reaction score
89,385
Nimekaa nikatafakari nimegundua mapenzi ni utapeli tu!, Haiwezekani ati mtu kwa kukubusu tu useme hayo ndio mapenzi!, yani mtu anatumia kiungo chake cha kusagia chakula (mdomo) kukuonyesha mapenzi!, How come..?

Ama mtu anakuonyesha mapenzi kwa kukupa kiungo chake cha uzazi yani uzazi ndio mapenzi!, hii ni LBL. mbona kama neno Mapenzi limekaa vizuri mno tofauti na vile tunavyopeana!.
Mbona wanyama hawafanyiani hivi ila wanaishi tu!, yani mdomo unafanya kazi yake ya kula na kuongea na uzazi ni kwaajili ya kuzaliana tu.
ndio maana sisi tunafikia mpaka kuuana kisa mapenzi!.. maana tunatapeliana tu!.
unanichumu kupitia mdomo ambao ni mashine yakusagia chakula ukiniuma je..?

Mtu anaenda mpaka kwa mganga akuroge ili umpende yeye tu na vitu vyako umpe yeye tu!, haya sio mapenzi ni ubinafsi na ni ukiritimba wa hali ya juu!.

Mi naona ni kama tunaleta ubunifu kwa kitu ambacho hatuna na ndio maana tunayoyaita mapenzi yanatuvuruga!.

Binafsi kuanzia leo sitaki tena kujihusisha na mapenzi, kizazi changu nitakitumia kuzalisha tu full stop!.

Hayo sio maneno yangu ni maneno ya rafiki yangu amenitumia ujumbe kwa njia ya WhatsApp!, najiuliza sijui nini kimempata mi nimemuambia tu ashikilie msimamo wake asilegelege!.
 
Tangu tuwe wapenzi,

Tumependana kiukweli pendo letu la moyoni,

Mioyo tusibadili wangu kipenzi dada tuepuke ushauri eeh,

Kwa mahasidi , kipenzi oooh sauda,

Kwa mahasidi kipenzi dada,

Tuepuke ushauri kwa mahasidi wapenzi ooh sauda, kwa mahasidi dada, oooooh sauda
 
Tangu tuwe wapenzi,

Tumependana kiukweli pendo letu la moyoni,

Mioyo tusibadili wangu kipenzi dada tuepuke ushauri eeh,

Kwa mahasidi , kipenzi oooh sauda,

Kwa mahasidi kipenzi dada,

Tuepuke ushauri kwa mahasidi wapenzi ooh sauda, kwa mahasidi dada, oooooh sauda
Kwa mujibu wa rafiki yangu yeye anaona hichi ulichoandika ni sawa na mchezo wa aviator!
 
Back
Top Bottom