Sasa huyu Bashe kamsaidia mkulima au kamuangamiza? Huu mchele wa Ruzuku unaweza kuuzwa 1,500/- kwa kilo

Sasa huyu Bashe kamsaidia mkulima au kamuangamiza? Huu mchele wa Ruzuku unaweza kuuzwa 1,500/- kwa kilo

Wewe ndio huelewi

Bashe kashindwa kutengeneza Win Win situation kwa mkulima na Mlaji
Nilitaka nikupe mfano wa hiyo win win but kwa sababu sielewi ngoja twende mpaka mwisho huo mchele tunaoagiza ukifika.

Utaelewa kwa vitendo siyo maneno!.
 
Ninavyowajua Watanzania wanapenda vitu vya bei rahisi Bila kuzingatia ubora

Hiyo michele iliyofichwa na Wakulima soon inaenda kuwadodea

Bashe ajipime kama anatosha!
Asante sana Bashe. We're should think about fee market. Were function is demand and supply of goods is considered. Ficheni mchele soko haliwasubiri. Ukitaka kusaidia watu wako hakikisha soko limejaa. Bei inajipanga yenyewe.
 
Idea ya kuwa ukipandisha bei unamsaidia mkulimaa asilimia 90 ni uongooo maana kiukweli wakulima huuza mazao yao msimu wa mavuno wakati bei ni chinii sanaaa... wenye hela zao wananunua wanatunzaa mkulima aliuza wastani wa kilo sh 1200 baada ya miezi ya mavuno kupita matajiri walionunua mzigo wanaanza kupush kilo 3800 hapo mkulima nae anarudi kununua kwa bei ya 3800... hii ni sawana kagomba tu ile ya korosho tofauti wale wanunua mali ikiwa shambani bado. mbolea bado zipo juuu...zana za kilimo kama matractor bado juuu mkulima najikongoja kulima kwa gharama kubwa ila faida wanakuja kupata MATAJIRI wanaonunua mzigo na kuweka stock period.
😀 😀 😀 😀
 
Ninavyowajua Watanzania wanapenda vitu vya bei rahisi Bila kuzingatia ubora

Hiyo michele iliyofichwa na Wakulima soon inaenda kuwadodea

Bashe ajipime kama anatosha!
Mbona hamueleweki Sasa. Alisema wakulima wauze nje mkalalamika eti bei huku ndani ni juu sana Sasa zinashuka mnalalamika tena, duh
 
Mkuu, mbona Umekigeuka Chama Sasa Hivi, Unapingana Na Ilani Iliyosema Kilogram Iwe Tshs 10000/=
Huyu bwam huwa Bado hajielewi na sijamuelewa Yuko upande gani Ni Mara nyingi huwa anasema Bei ipae kufikanjuu Mara wkt mwingine anamlaumu waziri

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ninavyowajua Watanzania wanapenda vitu vya bei rahisi Bila kuzingatia ubora

Hiyo michele iliyofichwa na Wakulima soon inaenda kuwadodea

Bashe ajipime kama anatosha!
Wakulima hawakuficha mchele wowote ndiyo maana sokoto haupatikani
 
Ninavyowajua Watanzania wanapenda vitu vya bei rahisi Bila kuzingatia ubora

Hiyo michele iliyofichwa na Wakulima soon inaenda kuwadodea

Bashe ajipime kama anatosha!
Kwani, si watauza popote duniani wanapopenda wenyewe kama walivyoshauriwa na mtaalam wao Bashe. Shida iko wapi?

Bashe ni debe tupu. Anapiga kelele nyingi sana, lakini kazi anayoifanya ni majanga matupu!
 
Wakilima Sana na soko likawa kidogo mtamsaindiaje mkulima?
Tulikokuwa tunaelekea mchele Kg ilikuwa ufike 5K kwa sababu matumizi home huwa nanunua kila baada ya wiki mbili ila ndani ya hii miezi miwili nilikuwa kila nikienda imeongezeka Tsh 300/700.

Ila vizuri zaidi wangewawezesha wakulima walime kwa wingi kila mkoa hali ingetulia.
 
Wabongo tuna tabu sana. Maana hata hatujui tunataka nini hasa...

Mchele ukipanda bei tunalalamika, na ukishuka bei tunalalamika...
Sio wote ila zoba ni yule anayelalama bila maana kama huyo uliyemkusudia.
 
Tatizo siyo mtoa mada bali akili yake imeshindwa kuchambua hadha ya kufichwa chakula, ugumu wa kupata mlo na wepesi wa kupata mlo.

Huyo huyo anaanzisha uzi 'mchele shs 3800kg bashe hafai' leo anaanzisha uzi 'Bashe anaangamiza mkulima' yaani ni hajui au anajifanya kusimama kati asionekane mpinzani.

Anang'ata na kupuliza!.
Aiseee halafu ndio shushushu anaetegemewa huyo ...
 
kwanini Mchele wa nje uwe bei rahisi kuliko wa ndani wakati kuna transportation kubwa, kodi za kutoka kwao na za kuingiza ndani ya Nchi? nahisi huenda mchele utakaokuja utakuwa ni ule wa ubora wa chini kabisa …TBS wanapaswa kusaidia Taifa kwa hili kuepusha ma Saratani ya siku za mbele

Mchele wa Vietnam inawezekanaje uwe bei rahisi kuliko wa kule Mbingu au Mang'ula Morogoro?
 
Tana 90000 sio mchezo kwa shilingi miambili kwa kilo mbona hela ndefu sana kama billion zakuzidi kuna watu wanaenda kupiga hela ndefu sana hapa
 
Kwa miezi hii hakuna mkulima anayefaidika na mfumuko wa bei ya mchele au nafaka zozote ambazo kwa kweli bei yake haikamatiki wanaofaidi ni wafanyabishara wakubwa waliohifadhi baada ya kununua kwa bei Chee kwa wakulima wakati wa mavuno .Uamuzi wa serikali wa kuagiza mchele nje si wa kupongezwa tu bali wa kuungwa mkono.Bei ya mchele na mahindi imekuwa kubwa kote hata mikoa ile the big five mahindi mchele bei zake ni majanga.Ila muhimu uje mapema kabla ili kufidia deficit hii na ulichelewa utaathiri bei ya ule wa wakulima halisi
 
Back
Top Bottom