kirengased
JF-Expert Member
- Jan 10, 2016
- 6,818
- 7,493
Salaam,
Moja kati ya mambo muhimu kwa taifa letu tunayoweka uvivu kuyarekebisha ni hili la Elimu. Kiukweli hatutoweza kufikia maendeleo endelevu bila kuwekeza vyema kwenye elimu ya teknolojia. Tazama Asia, nchi nyingi zimeibuka kiuchumi kwa kuboresha elimu kwanza.
Mimi namiliki kajishule na nasikitishwa sana na mfumo wetu wa elimu jinsi tunavyowapotezea muda watoto wengi kwa kuwafundisha mambo mengi ambayo hayawahusu, hawayapendi na hawatoyatumia katika maisha yao ya kazi.
Sasa ninaishauri serikali sikivu ya Mama Suluhu isuluhishe mgogoro wa elimu, kiundwe kikosi-kazi siyo kuhusu siasa bali cha kuichambua elimu yetu na kuifanya iendane na dunia ya leo ya sayansi na teknolojia!
Watoto wanateseka na njaa na lishe mbaya inayodumaza akili na miili yao huku wakisoma mambo rundo. Kiufupi tunaandaa vijana dhoofu kimwili na kiakili pia kiroho kwakuwa elimu ya dini tumeipuuzia mashuleni, nadhani hili ni jambo muhimu linalohitaji marekebisho ya haraka.
Binafsi kwa kifupi ninapendekeza kila wilaya hapa nchini iteuwe shule moja tuu kubwa na kuibadili kuifanya "Shule ya Sekondari ya Ufundi". Vijana wenye vipaji toka shule za msingi wanapoanza kidato cha kwanza wasome masomo matatu tuu yaani hesabu, fizikia na kemia kisha wazame kwenye kuunda na kukarabati vitu, iwe simu, kompyuta, pikipiki, ujenzi wanyumba, magari nk.
Hizi samani za kisasa tusiagize China kilal eo. Hizi shule zitakuwa tajiri maana zitatengenezea watu vitu kwa teknolojia ya juu na bei rahisi na zakuaminika. Shule zitajiendesha zenyewe kiuchumi na kusambaza teknolojia mpya mpaka vijijini.
Ni aibu leo nchi hii mafundi wengi ni wakubabaisha babaisha kwa kujifunzia vichochoroni, tunapaswa kubadilika! Tanzania tulitakiwa tuunde 'solar pannel' zetu kwa gharama yoyote ikiwamo kuiba teknolojia na kila nyumba yenye umeme ilazimishwe kununua 'solar panel' kupitia TANESCO. Ni aibu nchi hii usiku kuingia gizani wakati mchana tumeteseka najua kali Hii ni aibu kuu.
Rwanda wanateknolojia nzuri ya toyo za umeme sisi tunakwama wapi? Prof. Mkenda Waziri wa elimu anikodishie kitengo cha elimu ufundi ndani ya wizara ya elimu nina hakika ndani ya miaka mitano nchi hii haitokaa ilalamike kuingia gizani.
Hii ni kuzoea mambo yasiyofaa kwa kushindwa kufikiri vyema. Tujadili elimu kwani ndiyo chimbuko la maendeleo ya vizazi na vizazi.
Nawasilisha!