Dragunov Sniper
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 2,795
- 9
Nachelea kusema kwamba swali/andiko langu la kwanza umelisoma kwa kukulupuka, hukunielwa.
Nilichotaka kutoka kwako ni kifupi tu: WEWE BINAFSI, ULOSHIRIKI VIPI KUMPATA MWAKILISHI WAKO KATIKA BMK...
Mimi sikuhitaji elimu ninayoijua niipate tena kutoka kwako.
NI VIZURI KURUDIA MARA KADHAA ANDIKO LA MTU KABLA HUJAMJIBU...
Tafakari...
Wajumbe wa BMK walipatikana kwa njia halali kwani liliundwa na watu kutoka matabaka yote wakiwemo wajumbe waliochaguliwa na wananchi, wa viti maalum, pamoja wajumbe walioteuliwa na Rais.
Zaidi ya hayo BMK lilikuwa na makundi matatu ambayo ni Wabunge wa kuteuliwa, wabunge wanaotokana na majimbo ya uchaguzi pamoja na wabunge wa kutoka katika asasi mbalimbali za kiraia kama vile wakulimaa, wavuvi, waaandishi wa habari, wafugaji ambapo hawa wooote, wanafikisha idadi ya Wabunge 640 ambao wananchi ndiyo waliwaamini wawe wawakilishi wao. Kazi yao hawa ilikuwa kutunga Katiba iliyoongozwa na Rasimu ya Tume ya Katiba.
Kuhusu swali lako la "WEWE BINAFSI, ULOSHIRIKI VIPI KUMPATA MWAKILISHI WAKO KATIKA BMK" Kama umri wako ulikuwa zaidi ya miaka 18 mwaka 2010 na ulipiga kura, kwa njia hiyo ulishiriki kumchagua mbunge wa jimbo lako analokuwakilisha, hivyo ulishiriki kumpata mjumbe huyo, na namna nyingine ni wajumbe 201 walivyopatikana. Hawa walitoka miongoni mwa makundi mbalimbali, kama ulikuwa mshiriki mzuri katika kundi lako ulihusika kuwapata wajumbe hao maana wamepatikana kutoka miongoni mwetu.
Dhana ya kusema kuwa mambo fulani yametolewa kwenye Rasimu ya Warioba, Kazi ya Bunge Maalumu haikuwa na kazi ya kupitisha Rasimu, Kazi yake ilikuwa kuchambua na kuandaa Katiba Inayopendekezwa. Warioba hakutunga katiba, yeye aliandika mapendekezo tu, chombo chenye mamlaka kisheria ya kutunga katiba kilikuwa ni Bunge Maalum la Katiba tuu na si vinginevyo, BMK kupitia Sheria ya tangazo la serikali NA. GN. 254 lilipewa mamlaka ya bunge kuendelea na shughuli zake. Pia kifungu cha 25 cha Sheria ya katiba, BMK lilikuwa sahihi kufanya marekebisho yoyote pale palipohitjika ndiyo maana asilimia 75 ya masuala yote yaliyokuwepo kwenye Rasimu ya Katiba yamebaki na asilimia 25 yamefanyiwa maboresho ili yakidhi matakwa ya wananchi.
Msingi wa mambo yote hayo ya Katiba Inayopendekezwa nchini ni Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011.