Wazanzibari wamedai madaraka yao wee mpaka wamechoka, leo hii sisi wantanganyika tumekunwa kidogo ndo tunawaelewa wazanzibari maumivu waliyo yapitia miaka yote hyo.
Mkuu hivi mpaka leo hujaelewa? Wazanzibar walidai madaraka yao na walishapewa yote. Ambacho haijatamkwa rasmi ni Zanzibar kuwa nchi kamili, na suala lakuwa na jeshi lao la ulinzi wamekataliwa, lakini kila kitu wamepewa. Hata Raisi au kiongozi yeyote wa wa Muungano kutokuwa na sauti Zanzibar au kutotoa maagizo yeyote kwa Zanzibar walishakubaliwa.
Kwa mfano, mamlaka ya kusajiri meli ambayo walinyanganywa wakati wa Magufuli, wamerudishiwa tena, na wanazisajiri kama serikali ya Muungano
Uwepo wa Samia kama Raisi na Abdul umewapa fursa ya kupewa kila kitu walichodai huko nyuma,kimya kimya.
Na bonasa wanayoipata,pamoja na yote waliyopewa, ni kujazwa kwenye nafasi za huku bara wizarani na kwenye ukurugenzi katika mikoa nk
Kuna wakati Scotland walifanya referendum ya kutaka kujitenga na England after 300+ yrs ya muungano. Iko shida gani ya kufanya referendum ya huu muungano wetu. Wengi wakisema tunataka kuendelea hivi nani atakuwa na ubavu wa kupinga?