Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 40,476
- 26,173
Ndugu zangu Watanzania,
Poleni sana kwa kukesha mkiwa macho. Hongereni kwa kuendelea kuwa na imani na CCM, asanteni kwa kuendelea kutambua ya kuwa CCM ndiyo chama kilichobeba matumaini yenu, mstakabali wa maisha yenu, kesho ya watoto wenu, maisha ya wajukuu zenu, na uhai wa Taifa letu. Kwa hakika, CCM imeonyesha ni zaidi ya chama, ni zaidi ya imani. Imeonyesha ukubwa wake kwa Taifa letu.
Nawashukuru kwa kuendelea kutambua ya kuwa CCM ndiyo chama pekee chenye kutoa uongozi imara na wenye matumaini hapa nchini. Najua, na chama kinajua na kutambua, ya kuwa Taifa limekesha likiwa macho usiku kucha, huku macho na masikio yakielekezwa Dodoma kusikiliza na kuwajua wagombea waliopitishwa na CCM.
Chama kinajua kilitakiwa kutangaza majina hayo siku ya jana, lakini haikuweza kufanikiwa kutimiza jambo hilo. Hii ni kutokana na uzito na unyeti wa jambo hilo, na shughuli nzito inayoendelea mkoani Dodoma. Wagombea ni wengi sana, waliochukua na kurejesha fomu ni wengi sana, kila mmoja akiwa anataka kupata uteuzi wa chama ili kwenda kuwatumikia Watanzania.
Jambo ambalo limekipa chama na vikao vyake kazi kubwa na nzito ya kufanya uchujaji kwa umakini mkubwa sana, katika kuhakikisha kinawaletea Watanzania watu sahihi na wenye uwezo, dhamira, uzalendo, ushawishi, na kukubalika kwa watu. Lakini kubwa ni kuwa chama kinataka kuona haki ikitendeka, na watu sahihi wakipatikana kwa haki kabisa bila mawaa ili kuondoa malalamiko.
Hivyo basi, baada ya kushindikana kwa siku ya jana kukata kiu ya Watanzania, ni kuwa leo hii majira ya saa nne asubuhi chama, kupitia msemaji wake Mkuu Mwamba Mwenyewe — msomi kwelikweli na nguli wa mahesabu na uhasibu CPA Amos Makalla — atakuwa live mbele ya macho ya dunia, mbele ya waandishi wa habari, kuwatangazieni majina ya wagombea wote ambao wamepitishwa.
Kwa hiyo endeleeni kuwa wavumilivu, wenye subira, utulivu, kusubiri muda huo ambao nchi nzima inakwenda kusimama. CCM ndiyo chama chenye kutoa mwelekeo na mstakabali wa Taifa letu. Naweni na pateni kifungua kinywa, mtulie mbele ya TV zenu au kwa majirani wenye TV.
Kazi iendelee. Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa
Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.