GE2025 Sasa mkutano wa kutangaza wagombea kufanyika saa Nne asubuhi ya Julai 29, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
IMG-20250727-WA0028.jpg
 
Watanzania ama waliotia nia ndio wamekesha?
Shamba la bwana kheri, mbuzi wa bwana kheri! To each their own 🙄
 
Kitu ambacho huwa sijui Madai YA kusema kuwa CCM Ni kubwa ilhali kila uchaguzi unaweka mpira kambani

CCM pamoja Na umri mkubwa unaogopa CDM kama ukoma...inajua kuwa CDM ndio chama kikubwa nchini ambacho kimejengek mioyoni mwao raia wote

CCM Ina vibaraka tu wasio Na mema YA nchi..mafisadi wote wanajificha ndani YA ccm
 
Kaa kwa kutulia maana mambo ni mazito kwelikweli. Chama kinataka kikitoka hadharani kutoa ripoti basi kila mtu anabakie akibubujikwa na machozi ya furaha
Waandishi wa habari wamekesha ukumbini wakisubiri MAKALA aendelee na kikao hadi sasa bila bila. Kikao kimeahirishwa hadi saa 4 asbh ya leo.
Jana mliwageuza waandishi kuwa walinzi🤣🤣🤣🤣
 
Kitu ambacho huwa sijui Madai YA kusema kuwa CCM Ni kubwa ilhali kila uchaguzi unaweka mpira kambani

CCM pamoja Na umri mkubwa unaogopa CDM kama ukoma...inajua kuwa CDM ndio chama kikubwa nchini ambacho kimejengek mioyoni mwao raia wote

CCM Ina vibaraka tu wasio Na mema YA nchi..mafisadi wote wanajificha ndani YA ccm
Ukubwa wa ccm ni kama pua kubwa.. Haimaanishi itatoa kamasi nyingi
 
Kuwa mtulivu ndugu yangu. Kazi ni Nzito kwelikweli na siyo Nyepesi kama unavyofikiria. Embu Fikiria Mama yetu Mpendwa Amekesha siku mbili mfululizo Bila kupata hata muda wa kulala kwa sababu ya kuongoza vikao hivyo vizito na vyenye kutoa muelekeo na mstakabari wa Taifa letu.
Una uhakika huyo mamako alikesha na kwamba hakuwa amelala na mmewe?!.
Kumbuka dodoma kwasasa kuna baridi hasa jioni!
 
Mkunduh wewe...nani anaweza kukesha kwa ajili ya nyie mbwa...Yan mtu akeshe kwa ajili yenu ? Watu wametoka kwenye shuhul zao wamechoka wapumzike, eti wakeshe kwa upuuzi wenu..watakesha mazombie kama Hawa
downloadfile-5.jpg
 
Ndugu zangu Watanzania,

Poleni sana kwa kukesha mkiwa macho. Hongereni kwa kuendelea kuwa na imani na CCM, asanteni kwa kuendelea kutambua ya kuwa CCM ndiyo chama kilichobeba matumaini yenu, mstakabali wa maisha yenu, kesho ya watoto wenu, maisha ya wajukuu zenu, na uhai wa Taifa letu. Kwa hakika, CCM imeonyesha ni zaidi ya chama, ni zaidi ya imani. Imeonyesha ukubwa wake kwa Taifa letu.

Nawashukuru kwa kuendelea kutambua ya kuwa CCM ndiyo chama pekee chenye kutoa uongozi imara na wenye matumaini hapa nchini. Najua, na chama kinajua na kutambua, ya kuwa Taifa limekesha likiwa macho usiku kucha, huku macho na masikio yakielekezwa Dodoma kusikiliza na kuwajua wagombea waliopitishwa na CCM.

Chama kinajua kilitakiwa kutangaza majina hayo siku ya jana, lakini haikuweza kufanikiwa kutimiza jambo hilo. Hii ni kutokana na uzito na unyeti wa jambo hilo, na shughuli nzito inayoendelea mkoani Dodoma. Wagombea ni wengi sana, waliochukua na kurejesha fomu ni wengi sana, kila mmoja akiwa anataka kupata uteuzi wa chama ili kwenda kuwatumikia Watanzania.

Jambo ambalo limekipa chama na vikao vyake kazi kubwa na nzito ya kufanya uchujaji kwa umakini mkubwa sana, katika kuhakikisha kinawaletea Watanzania watu sahihi na wenye uwezo, dhamira, uzalendo, ushawishi, na kukubalika kwa watu. Lakini kubwa ni kuwa chama kinataka kuona haki ikitendeka, na watu sahihi wakipatikana kwa haki kabisa bila mawaa ili kuondoa malalamiko.

Hivyo basi, baada ya kushindikana kwa siku ya jana kukata kiu ya Watanzania, ni kuwa leo hii majira ya saa nne asubuhi chama, kupitia msemaji wake Mkuu Mwamba Mwenyewe — msomi kwelikweli na nguli wa mahesabu na uhasibu CPA Amos Makalla — atakuwa live mbele ya macho ya dunia, mbele ya waandishi wa habari, kuwatangazieni majina ya wagombea wote ambao wamepitishwa.

Kwa hiyo endeleeni kuwa wavumilivu, wenye subira, utulivu, kusubiri muda huo ambao nchi nzima inakwenda kusimama. CCM ndiyo chama chenye kutoa mwelekeo na mstakabali wa Taifa letu. Naweni na pateni kifungua kinywa, mtulie mbele ya TV zenu au kwa majirani wenye TV.

Kazi iendelee. Mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa

Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Aksante sana kwa taarifa kijana wa KINDALI, MNDALI wa Vwawa 😀😀😀🙏🙏
 
Kwani kulikuwa na nini...unakesha kuwasubiri wapiga meza Bungeni na wazee wa Ndiyooooooooo, itakuwa aibu sana.
 
Kumbe ni saa nne za Cuba?
 
Back
Top Bottom