Sasa naelewa kwa nini Democrats wanang'ang'ania kusiwepo na uhitaji wa kitambuliicho chochote kile wakati wa kupiga kura USA

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
4,460
Reaction score
13,715
Wanauiita ni mfumo wa kibaguzi

Wanataka mtu yoyote aishiye marekani aweze kupiga kura.

Kwa upande mwingine watu wanaamini hii ni mbinu wanatumia ili wahamiaji waliongia marekani bila vibali vya makazi wapewe fursa ya kupiga kura.

Kutokana na sera zao za open borders za term hii wamevunja rekodi kwa wahamiaji holela kuingia marekani kwa record numbers.

Sasa ndio hao ambao democrats wanaotaka wawapigie kura kwa malipo ya fadhira za kuwaacha waingie nchini marekani kirahisi.

Hadi sasa kuna majimbo yaliyoruhusu kupiga kura bila ID mengine lazima uwe na ID.
 
Uchaguzi wa marekani unachanganya sana maana wengine wasema sio wingi wa wapiga kura ila ni zile kura za majimbo tena Sasa ni wahamiaji haram
 
Ccm nayo nayo iige mtindo huo kwenda kupiga kura bila kitambulisho itapata kura nyingi sana maana kuna watu hawana vitambulisho vya mpiga kura
 
Uchaguzi wa marekani unachanganya sana maana wengine wasema sio wingi wa wapiga kura ila ni zile kura za majimbo tena Sasa ni wahamiaji haram
Uchaguzi wa Malekani ni wamaigizo, maana wingi wa watu hauamui uchaguzi wa Rais.
Mgombea akishinda jimbo fulani kwa kura za umma (popular votes), mfano California kwa Kamala Harris, anakuwa pia amejihakikishia kuvuna kura 54 za jimbo hilo (electoral votes).

Kila jimbo lina pointi ama kura zake kulingana na idadi ya maseneta na wawakilishi katika jimbo husika. Jumla ziko kura 538. Mgombea lazima apate zaidi ya nusu ya kura hizi (538/2) + 1 = 270.

Hii inasaidia sana kuwafanya wagombea watafute ushawishi kwenye majimbo yote, na siyo tu kushinda majimbo kadhaa ambayo huenda yana watu wengi zaidi kuliko mengine.

Tanzania, kwa mfano, mgombea akishinda Mbeya, Iringa, Dar labda na kanda ya ziwa na kaskazani, ana uhakika wa kuibuka kidedea. Sivyo kwa Marekani.
 
Electoral college (vote) wa Jimbo husika ndiye anayechagua rais . Na inaweza kutokea raia kwenye majimbo hayo wamemchagua rais flani Kwa kura nyingi lakini electoral wa Jimbo hilo akachagua mpinzani, hivo hupelekea kula za wengi(wananch) kutokua na maana.
 
Back
Top Bottom