Mgombea akishinda jimbo fulani kwa kura za umma (popular votes), mfano California kwa Kamala Harris, anakuwa pia amejihakikishia kuvuna kura 54 za jimbo hilo (electoral votes).
Kila jimbo lina pointi ama kura zake kulingana na idadi ya maseneta na wawakilishi katika jimbo husika. Jumla ziko kura 538. Mgombea lazima apate zaidi ya nusu ya kura hizi (538/2) + 1 = 270.
Hii inasaidia sana kuwafanya wagombea watafute ushawishi kwenye majimbo yote, na siyo tu kushinda majimbo kadhaa ambayo huenda yana watu wengi zaidi kuliko mengine.
Tanzania, kwa mfano, mgombea akishinda Mbeya, Iringa, Dar labda na kanda ya ziwa na kaskazani, ana uhakika wa kuibuka kidedea. Sivyo kwa Marekani.