Sasa nchi inapumua. Mama songa mbele, kazi iendelee

Prof Koboko

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
350
Reaction score
2,550
Yaani ukiambiwa kuna ugonjwa unaosumbua baadhi ya watanzania hasa wanaccm ni kutamini kua nchi iko katika seasoni mpya kabisa, tena ni ugonjwa mbaya huu zaidi kuliko hata UVIKO-19.
Tuna binadamu wana roho za kinyama zisizo na huruma eti wanajifanya wao ndio wanaumia kwa sasa. Kamwe hamtaweza kumkwamisha Mama na hilo haliwezekani kamwe.

Wananchi wanalia maisha magumu ni kwa sababu mifumo ya uzalishaji iliharibiwa na kikundi cha watu, ametokea mtu mwenye hofu ya Mungu hataki dhuluma na hata uonevu lakini bado kuna visokorokwinyo vinapiga kelele? Na Mama ana miaka 10 yake mbeleni, akimaliza ataweka mifumo mizuri ya kupata kiongozi mzuri wa kufanana naye, ninyi endeleeni kulialia tu.

Hakuna matukio ya watu kutekwa, hatusikii watu wakiokotwa ufukweni, hatusikii wafanyabishara wakiporwa mali zao, hatusikii watu wakipotea hovyo. Halafu bado kuna kikundi cha watu wanatukana watu kuwaita wahuni? Wenye hofu ya Mungu ndiyo wahuni? Wasiofanya biashara ya kununua watu ni wahuni?

Kwakua Rais anaelewa maadili ya kazi yake mnataka na yeye asimame aseme hali ya haifai hili alivyokuta? Mtanataka naye aropoke kua anajua siri za nchi hii?

Nchi ambayo tuliwafungia mipaka majirani hatuwezi kufanya nao biashara, tukavunja urafiki na marafiki wengi, hivi tungeendeleaje? Kama biashara tu zilikua zinasuasua,hii miradi ingekamilika kwa pesa za kutoka wapi? Tingeendelea kukusanya mapato toka kwa nani wakati uzalishaji ulianza kua shida?

Tuaiache nchi ipumue!
Mama kazi iendelee!
 
... kuna uwezekano waunga mkono juhudi hawataunga mkono juhudi za SSH? Kwamba lile zoezi limeondoka na mwendazake?
 
Mama ambae anadai kuwa urais kwake ni janga hawezi kusonga mbele wala kazi haiwezi kuendelea.She is hopeless.
 
Labda kama inapumilia Mashine ?

Na haya hayataisha leo wala kesho bali mpaka pale tutakapoondokana na kutegemea mtu ndio atuvushe... (mbaya zaidi sampuli za watu wa sasa ni kuangalia matumbo yao)

In short tutasubiri sana.....
 
Hapa morogoro walimwaga changalawe juu ya lami na sasa hivi wamerukia mfereji wa maji ya mvua ili mradi tu fedha itumike wasije nyang'anywa na UMMY Mwalimu na kupangiwa kazi nyengine.Manispaa morogoro Wana nia ya kuhakikisha Mama muda wake wote asijenge hata km 20 za barabara ndani ya manispaa muda wake wote
Mwenzi June 2021 walikomaa na viraka viraka na ujenzi wa mitaro.
Mara wakarukia alama za barababarni.
Ni hakika wanahakikisha mama anamaliza muda wake kwa kutoonyesha mafanikio lililojema.
 
Gharama za ujenzi zinapanda halafu mnasema nchi inapanuliwa!

Inaonekana watanzania hatujui kwamba tuna Haki ya kutendewa mazuri na viongozi, badala yake tunageuka kuwasujudia kama miungu.

Huwa najiuliza sana!
 
Mungu ampe maisha marefu mama yetu na Rais wetu pia.Hakika mungu ni mwema saaaana ,miaka takribani sita ya mateso ya kila aina hatimae sasa tunaishi kama binadamu .Nakumbuka kuna Christmas nilikuwa naelekea moshi kwa ajili ya mapumziko ilikuwa ni kama vita kati ya wasafiri na trafic .Ulikuwa unaulizwa hadi unafanya kazi gani hadi unaenda nyumbani kwa mapumziko ?jamani tumetoka mbali aisee
Yaani ukiambiwa kuna ugonjwa unaosumbua baadhi ya watanzania hasa wanaccm ni kutamini kua nchi iko katika seasoni mpya kabisa, tena ni ugonjwa mbaya huu zaidi kuliko hata UVIKO-19.
Tuna binadamu wana roho za kinyama zisizo na huruma eti wanajifanya wao ndio wanaumia kwa sasa. Kamwe hamtaweza kumkwamisha Mama na hilo haliwezekani kamwe.

Wananchi wanalia maisha magumu ni kwa sababu mifumo ya uzalishaji iliharibiwa na kikundi cha watu, ametokea mtu mwenye hofu ya Mungu hataki dhuluma na hata uonevu lakini bado kuna visokorokwinyo vinapiga kelele? Na Mama ana miaka 10 yake mbeleni, akimaliza ataweka mifumo mizuri ya kupata kiongozi mzuri wa kufanana naye, ninyi endeleeni kulialia tu.

Hakuna matukio ya watu kutekwa, hatusikii watu wakiokotwa ufukweni, hatusikii wafanyabishara wakiporwa mali zao, hatusikii watu wakipotea hovyo. Halafu bado kuna kikundi cha watu wanatukana watu kuwaita wahuni? Wenye hofu ya Mungu ndiyo wahuni? Wasiofanya biashara ya kununua watu ni wahuni?

Kwakua Rais anaelewa maadili ya kazi yake mnataka na yeye asimame aseme hali ya haifai hili alivyokuta? Mtanataka naye aropoke kua anajua siri za nchi hii?

Nchi ambayo tuliwafungia mipaka majirani hatuwezi kufanya nao biashara, tukavunja urafiki na marafiki wengi, hivi tungeendeleaje? Kama biashara tu zilikua zinasuasua,hii miradi ingekamilika kwa pesa za kutoka wapi? Tingeendelea kukusanya mapato toka kwa nani wakati uzalishaji ulianza kua shida?

Tuaiache nchi ipumue!
Mama kazi iendel
 
Alafu fikiria anakuja mpumbavu mmoja anaandika huu upuuzi wake! Umeme mgao,Maji mgao,Bei za bidhaa,Mafuta,Mbolea zimepanda maradufu alafu bila aibu mjinga mmoja anakuja na mashairi ya kusifia ujinga ujinga hapa! NONSENSE!
Mpuuzi kabisa wewe ,jiwe alikuta bei ya sukari ni shilingi ngapi ?
 
Gharama za ujenzi zinapanda halafu mnasema nchi inapanuliwa!

Inaonekana watanzania hatujui kwamba tuna Haki ya kutendewa mazuri na viongozi, badala yake tunageuka kuwasujudia kama miungu.

Huwa najiuliza sana!

Gharama za ujenzi zinapanda halafu mnasema nchi inapanuliwa!

Inaonekana watanzania hatujui kwamba tuna Haki ya kutendewa mazuri na viongozi, badala yake tunageuka kuwasujudia kama miungu.

Huwa najiuliza sana!Ne
 
Back
Top Bottom