Sasa nchi inapumua. Mama songa mbele, kazi iendelee

Sasa nchi inapumua. Mama songa mbele, kazi iendelee

Unaishi nchi gani ndugu toka 1500 hadi 2000 na usheee ndio stabilization hiyo ?
 
Yaani ukiambiwa kuna ugonjwa unaosumbua baadhi ya watanzania hasa wanaccm ni kutamini kua nchi iko katika seasoni mpya kabisa, tena ni ugonjwa mbaya huu zaidi kuliko hata UVIKO-19.
Tuna binadamu wana roho za kinyama zisizo na huruma eti wanajifanya wao ndio wanaumia kwa sasa. Kamwe hamtaweza kumkwamisha Mama na hilo haliwezekani kamwe.

Wananchi wanalia maisha magumu ni kwa sababu mifumo ya uzalishaji iliharibiwa na kikundi cha watu, ametokea mtu mwenye hofu ya Mungu hataki dhuluma na hata uonevu lakini bado kuna visokorokwinyo vinapiga kelele? Na Mama ana miaka 10 yake mbeleni, akimaliza ataweka mifumo mizuri ya kupata kiongozi mzuri wa kufanana naye, ninyi endeleeni kulialia tu.

Hakuna matukio ya watu kutekwa, hatusikii watu wakiokotwa ufukweni, hatusikii wafanyabishara wakiporwa mali zao, hatusikii watu wakipotea hovyo. Halafu bado kuna kikundi cha watu wanatukana watu kuwaita wahuni? Wenye hofu ya Mungu ndiyo wahuni? Wasiofanya biashara ya kununua watu ni wahuni?

Kwakua Rais anaelewa maadili ya kazi yake mnataka na yeye asimame aseme hali ya haifai hili alivyokuta? Mtanataka naye aropoke kua anajua siri za nchi hii?

Nchi ambayo tuliwafungia mipaka majirani hatuwezi kufanya nao biashara, tukavunja urafiki na marafiki wengi, hivi tungeendeleaje? Kama biashara tu zilikua zinasuasua,hii miradi ingekamilika kwa pesa za kutoka wapi? Tingeendelea kukusanya mapato toka kwa nani wakati uzalishaji ulianza kua shida?

Tuaiache nchi ipumue!
Mama kazi iendelee!
Wahuni kazini,
Unadhani kama hali ya maisha ingekua nzuri kuna mtu ana haja na viongozi?
Viongizi wanapaswa kukumbushwa kama hali ni mbaya maana wao hilo hawalijui.
 
Mpuuzi kabisa wewe ,jiwe alikuta bei ya sukari ni shilingi ngapi ?
Na samia kakuta mafuta ya kula na ya magari sh ngapi?
Tumia akili na sio makario.
Wewe unazungumzia sukali tu hebu sema mwenyewe vitu gani kwa sasa havishikiki kila siku vinapanda?
 
Kama kweli ana nia ya kuweka mazingira mazuri katika Nchi hembu muulize kuhusu Katiba mpya tumsikie atajibu nini.
Amekazana kupindua ya Magufuli ila yale yanayomfaidisha ameyakumbatia. Marufuku ya shughuli za vyama vya siasa na madai ya katiba mpya .
 
Alafu fikiria anakuja mpumbavu mmoja anaandika huu upuuzi wake! Umeme mgao,Maji mgao,Bei za bidhaa,Mafuta,Mbolea zimepanda maradufu alafu bila aibu mjinga mmoja anakuja na mashairi ya kusifia ujinga ujinga hapa! NONSENSE!
Takataka kabisa hao.
 
Amekazana kupindua ya Magufuli ila yale yanayomfaidisha ameyakumbatia. Marufuku ya shughuli za vyama vya siasa na madai ya katiba mpya .
Hawanaga hata nia njema hao watu, maslahi yao ndio mambo ya msingi kwao.
 
Hii ndiyo nchi inayopumua👇🤡🤡🤡
16402654753460.jpg
 
Naunga mkono hoja
P
Wewe Mayala ushakuwa kama taahira inamaana huwezi kuendesha maisha yako bila kujipendekeza kwa wanasiasa? Tuambie kipi kimepumua hapa nchini? Kama demokrasia bado mambo yale yale kasoro rangi,bei za bidhaa zimepanda,ufisadi na uzembe kazini umeanza kushamiri! Lete hapa data utuambie wewe mzee! Nyie ndo mnazeeka bila hata maendeleo yoyote kwa kuwa hamjitambui!
 
Back
Top Bottom