GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamebariki kifungo cha mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina cha kutohudhuria vikao 15 vya Bunge mfululizo kwa kosa la kumtuhumu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kuwa alilidanganya Bunge kuhusu sakata la kuagiza sukari nje.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mwenyekiti wa Kamati Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge, Ally Makoa kuwasililisha taarifa ya kamati hiyo na wabunge kutoa maoni kuhusu tuhuma za Mpina kudharau mamlaka ya Spika na Bunge, jijini Dodoma leo Jumatatu Juni 24, 2024.
Kamati ilipendekeza mbunge huyo kusimamishwa vikao 10 vya Bunge, lakinimaazimio na maoni ya wabunge wamependekeza kusimamishwa vikao 15. Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson amebariki adhabu hiyo.
Pia, Dk Tulia amesema adhabu ya mbunge huyo imeanza kuhesabiwa kuanzia leo Juni 24, 2024 na kusema hatarudi katika kikao cha pili cha Bunge cha Novemba, 2024.
Chanzo: mwananchi_official
Kama kuna Watu ambao siwaamini na sitowaamini Duniani kutokana na kuwa Wanafiki na Wasaliti ni Watanzania.