Katika hotuba aliyoitoa Rais wetu hivi karibuni kule Chato, kuna mambo kadhaa ambayo yanatuonesha kwamba hali ya nchi kwa sasa ni tete:
1) Kwamba Rais yuko Chato kwa muda mrefu sasa
kwa kawaida Rais wetu Magufuli huenda Chato kwa mapumziko. hivi sasa ni muda umepita tunaona Rais yupo Chato. Corona ilipoanza kuchanganya, Rais wetu aliondoka Dar na kubanisha pale Dodoma, makao makuu. tulishuhudia Rais wetu akifanya MEDITATION kwenye majabali. naona baadaye akaona hiatoshi, akaamua kwenda mbali zaidi na hii Corona. na sasa tumeshuhudia akitoa Major Speech yake kutoka Chato. pia ni vema kukumbuka kwamba Rais wetu huwa ni mwoga sana wa majanga. amekuwa na kawaida ya kujitenga mbali na majanga, na kumwachia PM wake. hali kwa sasa ndio hiyo hiyo. Kamanda mkuu kaingia mitini. Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.
2) Hotuba inayochanganya
Katika hotuba aliyotoa, badala ya kutoa mwanga katika mapambano na Corona, imeleta giza. badala ya kutia matumaini, imeleta hofu zaidi. siyo ajabu sekeseke la Amana lilifuatia mara moja. Hotuba yake inaonesha anatumia zaidi uelewa wake na hisia zake, badala ya kutoa msimamo kutokana na sayansi ya kisasa kabisa, utafiti mpana, mjadala makini na wasaidizi wake, ushauri mpana na makini, na tafakari iliyo pevu. Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.
3) Anaongea na wakuu wa vyombo vya usalama
Rais Magufuli siku zote anapenda sana majeshi. akikwama popote pale anaita majeshi, na ni zaidi ya Rais yeyote aliyemtangulia. akikwama ujenzi, Jeshi. akikwama madaraja, Jeshi. na hata katika lile JANGA ALILOCHUMA MWENYEWE, JANGA LA KOROSHO, aliita jeshi. Katika kipindi hiki alichochanganyikiwa kabisa, aliona badala ya kuita maprofesa wa tiba na wataalamu wa magonjwa, wizara ya afya na wizara zingine, au hata Task force aliyounda mwenyewe kupambana na Corona, aliita wakuu wa vyombo vya usalama, majeshi. Na kama alivyoita wanajeshi ili ikiwezekana wabangue korosho kwa buti, kasema wazi kabisa kwamba anataka kutumia jeshi kupambana na korona. na kweli, IGP akatafakari atafanya nini hapa kwa kutumia upolisi wake, akaamua kufanya kile ambacho wengi walishasema siku nyingi. kuzuia raia wa kutoka nje. sasa tunasubiri CDF Mabeyo yeye atafanya nini , atoe amri wanajeshi waitandike buti Corona? Au yule wa Magereza aitie gerezani Corona? Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.
4) Visingizio vya ajabu
Labda katika hali inayoonesha kukwama zaidi, Rais ametoa visingizio. Badala ya kufuata njia sahihi za kukabiliana na Corona, aliamua kuziba masikio na kupokea sifa kutoka kwa wale waliomuona kwamba ni shujaa pale mwanzo. sasa vifo vinaongezeka kwa kasi, analaumu dawa za kupulizia, analaumu kwamba pengine amehujumiwa kwa kuletewa Barakoa zenye virusi vya Corona! Huyu ni mtu asiyetaka kubeba lawama begani na kujisahihisha. kukubali na kukiri alikosea, na kusonga mbele. Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.