Sasa ni dhahiri Rais wetu Magufuli amekwama

Sasa ni dhahiri Rais wetu Magufuli amekwama

wakupe tu ukuu wa mkoa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mimi ni msomaji mzuri sana wa makala za Pascal mayalla, kunatoafauti kubwa ya uandishi wake from the day ameitwa bungeni. Hata Mimi kidogo nilipata mashaka kwa kuona ameanza kuandika makala Kama za gazeti la uhuru.lakini ni kinyume chake bado ni mwandishi anayetumia akili na kalamu yake kwa umakini sana hasa kwenye kipindi hichi ambacho media imewekwa mfukoni. Ukitaka kuamini hilo soma between lines alichokoandika kuhusu ushindi wa ccm serikali za mitaa.ukisoma juujuu utahisi amesifia lakini kiuhalisia amekejeli sana kwenye ile makala.pascal ikitokea magufuli akampa udc let say Kama watu wanavyomtabiria, itakuwa ni kwa factor nyingine tu Ila kwenye kujipendekeza hayupo....soma vizuri anachoandika utaelewa ninachokiongea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningekuunga mkono kama katika hao kumi wamo watoto wako, baba, mama, mke, shangaz, mjomba, kaka na dada yako. lakini kwa sababu wanaokuhusu hawapo unawaona wenzako waliokfiwa na wapendwa wao na ndugu zao hawajapoteza kitu. You are likely to be witch or Satan.
Nikweli Mkuu , uwezo wa watu kufikiria na kutafakari mambo umekua duni sana au watu wanaamua kuongea ili kujifurahisha.

Tujiulize wale wenzetu waliolazimisha jana kutoka hospitali, hapo tutafakari siku zamu yetu ikifika.

Hakuna ukweli wowote kuhuse taarifa za wagonjwa ( Zero data credibility). Wangapi wamepimwa? na kwanini kila siku tusipewe taarifa za wangapi wamepimwa na wangapi wako positive. Kama unauwezo wa kupima kwanini tuseme watu wameshililiwa kwa uchunguzi.

Sikiliza taarifa ya waziri, ni bora kuomba Mungu na kuwaombea wenzetu waliokuwenye wakati mgumu huu. Itakapowakuta hawa wanaoshangilia kila kitu nadhani walau tutakua na maneno ya tafakuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningeshangaa kama ungeandika "naunga mkono hoja"!Ingekuwa ni mada ya kumpamba kwa shangwe na nderemo ungewahi kuandika neno hilo!
Hujui kusoma, zaidi ya kutamka silabi. Nenda kasome katikati ya mistari
 
Nilitegemea ungeenda kwenye hicho kitengo cha mawasiliano alichoenda yule mama yetu aliyekuwa wizara ya siha
Yaani leo tungesikia 1,000 recovered, new cases declined by 50%; hiyo ni ndani ya masaa 48
 
Juzi kasema watu waliopona wanafika 100 alafu Leo kuna wengine 30 wamepona nahisi mpaka kufika jumatatu watakuwa wamepona wagonjwa wote wa corona...
Sisi wanalumumba tunaamini Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo itakuwa haina new cases ifikapo wiki ijao
 
FB_IMG_1587726605657.jpg
 
As long as wagonjwa wanaendelea kupona Mimi binafsi sioni haja ya kumshutumu hpa.

Idadi ya maambukizi na vifo bado iko chini sana ukilinganisha na nchi nyingine. Pia hao wabeberu wa WHO ni ujinga tu ndo umewajaa kwa kusema kuwa Tanzania hatuchukui hatua serious kwenye huu ugonjwa wakati wao nchi zao kila siku idadi ya wagonjwa na vifo inaongezeka,sasa kwa macho ya kawaida kati ya sisi na wao nani hayuko serious na haya mapambano ya covid-19?

Tumuunge mkono Rais wetu kwenye hili jambo na namna tunavyoenda nalo ili mda wa kushinda hii vitu basi wote nchi nzima tuwe ni washindi.
 
Katika hotuba aliyoitoa Rais wetu hivi karibuni kule Chato, kuna mambo kadhaa ambayo yanatuonesha kwamba hali ya nchi kwa sasa ni tete:

1) Kwamba Rais yuko Chato kwa muda mrefu sasa
kwa kawaida Rais wetu Magufuli huenda Chato kwa mapumziko. hivi sasa ni muda umepita tunaona Rais yupo Chato. Corona ilipoanza kuchanganya, Rais wetu aliondoka Dar na kubanisha pale Dodoma, makao makuu. tulishuhudia Rais wetu akifanya MEDITATION kwenye majabali. naona baadaye akaona hiatoshi, akaamua kwenda mbali zaidi na hii Corona. na sasa tumeshuhudia akitoa Major Speech yake kutoka Chato. pia ni vema kukumbuka kwamba Rais wetu huwa ni mwoga sana wa majanga. amekuwa na kawaida ya kujitenga mbali na majanga, na kumwachia PM wake. hali kwa sasa ndio hiyo hiyo. Kamanda mkuu kaingia mitini. Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.

2) Hotuba inayochanganya
Katika hotuba aliyotoa, badala ya kutoa mwanga katika mapambano na Corona, imeleta giza. badala ya kutia matumaini, imeleta hofu zaidi. siyo ajabu sekeseke la Amana lilifuatia mara moja. Hotuba yake inaonesha anatumia zaidi uelewa wake na hisia zake, badala ya kutoa msimamo kutokana na sayansi ya kisasa kabisa, utafiti mpana, mjadala makini na wasaidizi wake, ushauri mpana na makini, na tafakari iliyo pevu. Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.

3) Anaongea na wakuu wa vyombo vya usalama
Rais Magufuli siku zote anapenda sana majeshi. akikwama popote pale anaita majeshi, na ni zaidi ya Rais yeyote aliyemtangulia. akikwama ujenzi, Jeshi. akikwama madaraja, Jeshi. na hata katika lile JANGA ALILOCHUMA MWENYEWE, JANGA LA KOROSHO, aliita jeshi. Katika kipindi hiki alichochanganyikiwa kabisa, aliona badala ya kuita maprofesa wa tiba na wataalamu wa magonjwa, wizara ya afya na wizara zingine, au hata Task force aliyounda mwenyewe kupambana na Corona, aliita wakuu wa vyombo vya usalama, majeshi. Na kama alivyoita wanajeshi ili ikiwezekana wabangue korosho kwa buti, kasema wazi kabisa kwamba anataka kutumia jeshi kupambana na korona. na kweli, IGP akatafakari atafanya nini hapa kwa kutumia upolisi wake, akaamua kufanya kile ambacho wengi walishasema siku nyingi. kuzuia raia wa kutoka nje. sasa tunasubiri CDF Mabeyo yeye atafanya nini , atoe amri wanajeshi waitandike buti Corona? Au yule wa Magereza aitie gerezani Corona? Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.

4) Visingizio vya ajabu
Labda katika hali inayoonesha kukwama zaidi, Rais ametoa visingizio. Badala ya kufuata njia sahihi za kukabiliana na Corona, aliamua kuziba masikio na kupokea sifa kutoka kwa wale waliomuona kwamba ni shujaa pale mwanzo. sasa vifo vinaongezeka kwa kasi, analaumu dawa za kupulizia, analaumu kwamba pengine amehujumiwa kwa kuletewa Barakoa zenye virusi vya Corona! Huyu ni mtu asiyetaka kubeba lawama begani na kujisahihisha. kukubali na kukiri alikosea, na kusonga mbele. Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.
Hopeless comment. Haya tumekusikia Dada!!
 
Ningekuunga mkono kama katika hao kumi wamo watoto wako, baba, mama, mke, shangaz, mjomba, kaka na dada yako. lakini kwa sababu wanaokuhusu hawapo unawaona wenzako waliokfiwa na wapendwa wao na ndugu zao hawajapoteza kitu. You are likely to be witch or Satan.
Hebu rudi usome tena then uje umwombe samahani. Mkuu kweli umeshindwa kumwelewa P??? Mbona katumia lugha rahisi sana!!
 
Natambua kazi aliyonayo Magufuli ni kubwa. Lakini kujitokeza kwake kuitwa shujaa kwa sababu anafanya tofauti na wengine, kuna risk zake. Ila shujaa anayejichanganya! Na anajificha?
 
Natambua kazi aliyonayo Magufuli ni kubwa. Lakini kujitokeza kwake kuitwa shujaa kwa sababu anafanya tofauti na wengine, kuna risk zake. Ila shujaa anayejichanganya! Na anajificha?
Hili nililiuliza hapa

Imeshika kasi: Tuendelee Ushujaa wa "Ka-Corona, tusitishane, tuchape kazi" tukiteketea; au tubadili msimamo na tusitisishe Mikusanyiko tuokoke? - JamiiForums

Ungetaka rais Magufuli awe ni shujaa wa aina gani kati ya Shujaa mpambanaji shupavu, ambaye mwisho wa siku atakufa kishujaa na kutamkwa ni shujaa wa taifa lakini kafa!.

Au shujaa Mpiganaji makini ambaye anapigana kwa makini ili asife hata kama hatashinda vita.

Kipi bora, abaki Dar a risk kuambukizwa Corona au ajichimbie Chato abaki salama hata kama atabezwa kuwa kajificha?
P
 
Back
Top Bottom