Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Israel bila Marekani, si kitu huko Mashariki ya Kati.
Taiwan bila Marekani, si kitu mbele ya China.
Korea Kusini bila Marekani, si kitu mbele ya Kim Jong Un.
Na Ukraine bila msaada wa Marekani, si kitu mbele ya Urusi ya Putin.
Jana Rais Trump kachomoa misaada ya kijeshi ya Marekani kwenda Ukraine, leo Volodymyr Zelenskyy kasema sasa yuko tayari kusitisha mapigano na kufikia muafaka wa kumaliza vita na Urusi na kwamba anasikitika kwa kilichotokea Ijumaa ya wiki iliyopita pale ikulu ya Marekani.
Ukweli wa mambo ni kwamba Marekani ndiyo kiongozi wa dunia. Marekani ndo inayoiendesha dunia.
Muungano wa Ulaya, ulio na jumla ya nchi 27, umeshindwa kuipiga tafu Ukraine bila msaada wa Marekani.
Viongozi wa Ulaya sasa hivi wana matumbo joto wakihofia tetesi kuwa huenda Marekani ikajitoa kwenye jumuiya ya NATO.
Ulaya imeonyesha udhaifu wa kiwango cha hali ya juu sana kwa kuwa tegemezi ya Marekani.
Bila jeshi la Marekani, nchi zote za EU hazifui dafu mbele ya Urusi [kijeshi].
Msioipenda Marekani, poleni sana maana hii hali na hadhi vitaendelea kuwepo kwa muda mrefu sana.