Sasa ni dhahiri, super power ni moja tu hapa duniani

Sasa ni dhahiri, super power ni moja tu hapa duniani

Israel bila Marekani, si kitu huko Mashariki ya Kati.

Taiwan bila Marekani, si kitu mbele ya China.

Korea Kusini bila Marekani, si kitu mbele Kim Jong Un.

Na Ukraine bila msaada wa Marekani, si kitu mbele ya Urusi ya Putin.

Jana Rais Trump kachomoa misaada ya kijeshi ya Marekani kwenda Ukraine, leo Volodymyr Zelenskyy kasema sasa yuko kusitisha mapigano na kufikia muafaka wa kumaliza vita na Urusi na kwamba anasikitika kwa kilichotokea Ijumaa ya wiki iliyopita pale ikulu ya Marekani.

Ukweli wa mambo ni kwamba Marekani ndiyo kiongozi wa dunia. Marekani ndo inayoiendesha dunia.

Muungano wa Ulaya, ulio na jumla ya nchi 27, umeshindwa kuipiga tafu Ukraine bila msaada wa Marekani.

Viongozi wa Ulaya sasa hivi wana matumbo joto wakihofia tetesi kuwa huenda Marekani ikajitoa kwenye jumuiya ya NATO.

Ulaya imeonyesha udhaifu wa kiwango cha hali ya juu sana kwa kuwa tegemezi ya Marekani.

Bila jeshi la Marekani, nchi zote za EU hazifui mbele ya Urusi [kijeshi].

Msioipenda Marekani, poleni sana maana hii hali na hadhi vitaendelea kuwepo kwa muda mrefu sana.
Nilijua bidhaa zinazosemwa viwanda vimeongezeka kuwatishia USA wamerusha setelaiti picha ya mama.
IMG_0748.jpeg
 
Mkuu unaambiwa viwanda vingi sasa hivi hakuna watu. Hao undocumented walikuwa wanategemewa sana kama labourers. Wanaogopa kwenda kazini. Kazi walizokuwa wanafanya Maga na black Americans hawazitaki. Matunda na mbonga zinadoda mashambani. Kwenye restaurants na huduma zingine hali mbaya. Sasa hivi stock exchange toka jana imeshuka vibaya.

Hata right wings media WSJ na Fox zimeshaanza kulalamika na kutahadharisha ambacho siyo kitu cha kawaida.

Hata traditional Republican kina mitch McConnell George bush dick Cheney wanasikitika sana.

Hali itakuja kuwa ngumu zaidi na tayari imeshaanza.

Trump ni kama mtoto utadhani mimi na nyau adriz humu jamvini.

Leadership needs critical thinking, vision, mental strength and maturity.

By the mimi nina green card ya marekani japo siishi huko inaniuma sana.

Nyau de adriz
Hapa nimekuelewa vizuri
 
😂😂😂 I try to imagine mwanajeshi wa kihindi akiwa battle field anakuwaje maana si uvivu ule, hivi hata wana historia ya kupigana vita yoyote wakashinda?
wana hao marines wao, marine commando forces(MARCOS)

moja kati ya vikosi maalum makini duniani

wana nuclear submarines 2
 
Kibongo Bongo Trump angeitwa dikteta kama ilivyokuwa kwa JPM 😂
 
Russia 🇷🇺 ni dude kubwa fikiria mataifa 27 ya EU & USA 🇺🇸 yamemchangia kidume Putin bado yupo.

Russia 🇷🇺 si Zimbabwe 🇿🇼
 
Mkuu hata mimi namkubali lakini kwa tarrifs, kufukuza undocumented na kuindolea misaada ya kijeshi Ukraine kakosea sana. Ifikapo mwezi wa saba na wa nane mwaka ndio utaona athari ya carelessness yake.

Nasubiri kwa hamu job report ya February, ijumaa hii kutoka labour department.

mshamba_hachekwi

Nyau de adriz
Ya kwamba waendelee kuteketeza pesa kwenye vita ambavyo wanajua hawawezi kushinda?
 
Waziri mkuu wa Canada dogo Justin Trudeau alisema Trump akiweka tozo na Sisi tunaweka, Leo naona jasho linamtika anawahaidi wananchi wake kuwa wajiandae na Hali ngumu ya maisha, ila anatafuta namna ya kumaliza vita hii ya miuchumi haraka iwezekanavyo!
Kashaweka, na kamwamvia Donald hata kama ni smart, ila uamuzi ilichukua ni dumb.
 
Israel bila Marekani, si kitu huko Mashariki ya Kati.

Taiwan bila Marekani, si kitu mbele ya China.

Korea Kusini bila Marekani, si kitu mbele ya Kim Jong Un.

Na Ukraine bila msaada wa Marekani, si kitu mbele ya Urusi ya Putin.

Jana Rais Trump kachomoa misaada ya kijeshi ya Marekani kwenda Ukraine, leo Volodymyr Zelenskyy kasema sasa yuko tayari kusitisha mapigano na kufikia muafaka wa kumaliza vita na Urusi na kwamba anasikitika kwa kilichotokea Ijumaa ya wiki iliyopita pale ikulu ya Marekani.

Ukweli wa mambo ni kwamba Marekani ndiyo kiongozi wa dunia. Marekani ndo inayoiendesha dunia.

Muungano wa Ulaya, ulio na jumla ya nchi 27, umeshindwa kuipiga tafu Ukraine bila msaada wa Marekani.

Viongozi wa Ulaya sasa hivi wana matumbo joto wakihofia tetesi kuwa huenda Marekani ikajitoa kwenye jumuiya ya NATO.

Ulaya imeonyesha udhaifu wa kiwango cha hali ya juu sana kwa kuwa tegemezi ya Marekani.

Bila jeshi la Marekani, nchi zote za EU hazifui dafu mbele ya Urusi [kijeshi].

Msioipenda Marekani, poleni sana maana hii hali na hadhi vitaendelea kuwepo kwa muda mrefu sana.
kuna mwehu mmoja alikuwa kiongoz wa USSR , alikuwa na akili kama za Trump , ila mwisho wa utawala wake , USSR iligeuka kuwa kama Msumbiji , kila member states alianza jitoa
 
Movie tu kama movie zingine.

Irremediabilis Romaticus

Ni vizuri Trump amechaguliwa, na anaweka wazi vitu ambavyo wazungu walikuwa wakivificha kwa mda, kwamba ni waongo sana na ajenda yao ni kutawala Dunia. Kwa kiasi kikubwa wameweza kutawala fikra na mawazo ya wengi, ila safari hii, upo uwezekano wakatawala mpaka ardhi zao.

Ukoloni mamboleo is real.
kwann utawaliwe ilihali una akili sw na mzungu , utagundua unapenda mseleleko , nyiny ndo mnairudisha ccmu madarakan kwa hongo ya tshirt na mziki wa singeli
 
Waziri mkuu wa Canada dogo Justin Trudeau alisema Trump akiweka tozo na Sisi tunaweka, Leo naona jasho linamtika anawahaidi wananchi wake kuwa wajiandae na Hali ngumu ya maisha, ila anatafuta namna ya kumaliza vita hii ya miuchumi haraka iwezekanavyo!
Analialia kwamba ni njama ya Trump ya kuua uchumi wao kisha alichukue kirahisi Canada kama jimbo la 51 la Marekani. Trump katweet akisema mmwambieni huyo Gavana wa Canada kuwa akiweka tariff na Mimi nitaongeza kiwango hicho hicho.
 
Mimi nishangae eti Norway anatoa misaada ila naye anapokea kutoka USAID!
Wametuhadaa sana watu wa Ulaya.

kwann utawaliwe ilihali una akili sw na mzungu , utagundua unapenda mseleleko , nyiny ndo mnairudisha ccmu madarakan kwa hongo ya tshirt na mziki wa singeli
Sihongeki.

Ety mseleleko, mie sie babako alietoa mseleleko wa fuvu lako😅😉

Hata hivyo usinibadilishie kibao hapa. Mie sio mleta mada.

Tambua hilo.

Mzungu hajawahi, na haitatokea aje kunitawala, sio kwa fikra, na wala kimawazo.

Umechangamsha genge lakini😂😂😂
 
Marekani ndio hulinda hadi Mekka ikiwemo lile jiwe wao huenda kuliabudu, ila wakishiba unaskia "death to America"
 
Back
Top Bottom