Ohh sawa. Licha ya changamoto zilizojitokeza na zinazojitokeza hasa baada ya Uhuru ufisadi, rushwa, Vita, na tamaa ya madaraka nk Bado kwa miaka hii tumeendelea kuwa Bora zaidi ya jana.
Maendeleo Ni makubwa Sana. Miaka miwili iliyopita nilikua nikipiga stories na mzee wangu juu ya tulipotoka hakika inatisha. Tulipotoka nyuma kidogo ya 1985 hata sabuni, viwalo, chakula na sukari lilikua tatizo kuu.
Naambiwa hata mafuta ya mboga wananchi waliandika na kusgiza bidhaa hii huku wakisubiri kwa mawiki kuipata. Huo Ni mfano tu. Lakini hata hivyo pengine Ni mikakati TU iliyotuangusha viwanda vilianzishwa, majengo yakatandikwa lakini mchwa walitafuna mazao ya haya yote.
Hata leo jitihada za kuelekea unafuu zinadumazwa na ubadhirifu . Juzi nimeona kibanda kidogo Cha futi nne kwa tatu Cha mlinzi kimejengwa kwa tsh milioni 11. Nani anajali? Si fedha za kuletewa TU bwanaa.
Nb.
Bado tuko kwenye njia nzuri ya kuelekea maziwa na asali.
Barabara
Shule
Afya
Kilimo
Si vya kubeza