CAPO DELGADO
JF-Expert Member
- Aug 31, 2020
- 8,542
- 18,340
Club ya Pyramid FC ya Misri imetangaza kumsajli Mshambuliaji wa Kimataifa wa Congo DR Fiston Kalala Mayele (29) kutokea Yanga SC ya Tanzania.
Mayele anaondoka Yanga baada ya kucheza misimu miwili Tanzania kwa maanikio makubwa msimu wa kwanza 2021/2022 alimaliza nafasi ya pili kwa ufungaji magoli 16.
Msimu wa 2022/2023 akiibuka MVP wa Ligi Kuu Tanzania bara sambamba na tuzo ya Mfungaji bora wa Ligi sawa na Said Ntibazonkiza wa Simba wote wakifunga magoli 17.
Mayele anaondoka Yanga baada ya kuisaidia kutwaa taji la Ligi Kuu mara 2, FA Cup 2 Ngao ya Jami mara mbili na kuisaidia Yanga kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza katika historia yao msimu 2022/2023 na ndio Mfungaji bora wa Michuano hiyo akimaliza a magoli 7