Sasa ni rasmi, Fiston Kalala Mayele atambulishwa Pyramid FC ya Misri

Sasa ni rasmi, Fiston Kalala Mayele atambulishwa Pyramid FC ya Misri

Umeshamaliza kumfundisha Bocco kuwa golikipa? Ukishamaliza inabidi ukajifuze nafasi za wachezaji na majukumu yao makuu. Nani aliyekwambia Skudu kaja kuchukua nafasi ya Mayele?
Kwani mwokozi lazima awe striker?

Kuhusu Bocco, mtafute mtu anaitwa Jorge Campos. Vilevile kasome historia ya David De Gea
 
Inawezekana mkuu
Pale Al Ahly panga pangua , Alou Dieng na Percy Tau lazima waanze
Kule Wydad fanya ufanyavyo ila Zoa lazima aanze hata kama ana bandeji kichwani
USM Alger watapanga kikosi ila lazima Orebonye aanze
Kwa hiyo nkuu inawezekana Kwa mwamba kutoboa,muhimu akiendeleza discipline yake aliyokua nayo Yanga
Jamaa mtu Sana Yule, we wish him all the best
Daah huyo Alou Dieng ni hatari.
 
Daaaah 😳😳😳 Sa itakuwaje au skudu ndo mwokozi wetu aliyebaki? Tumpe thank you yake basi, tuache vinyongo
Amepewa thank you yenye maua mengi mno
Never seen before that kind of farewell
Screenshot_20230730-231635.png
 
View attachment 2703284

Club ya Pyramid FC ya Misri imetangaza kumsajli Mshambuliaji wa Kimataifa wa Congo DR Fiston Kalala Mayele (29) kutokea Yanga SC ya Tanzania.

Mayele anaondoka Yanga baada ya kucheza misimu miwili Tanzania kwa maanikio makubwa msimu wa kwanza 2021/2022 alimaliza nafasi ya pili kwa ufungaji magoli 16.

Msimu wa 2022/2023 akiibuka MVP wa Ligi Kuu Tanzania bara sambamba na tuzo ya Mfungaji bora wa Ligi sawa na Said Ntibazonkiza wa Simba wote wakifunga magoli 17.

Mayele anaondoka Yanga baada ya kuisaidia kutwaa taji la Ligi Kuu mara 2, FA Cup 2 Ngao ya Jami mara mbili na kuisaidia Yanga kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza katika historia yao msimu 2022/2023 na ndio Mfungaji bora wa Michuano hiyo akimaliza a magoli 7
Yanga SC wakiambulia Pesa nyingi ya Mgao basi itakuwa ni Shilingi Elfu Mbili ( Tsh 2,000/= ) tu za Kitanzania na watakaopata nyingi ni Klabu yake ya AS Vita, Maniema FC na Tajiri wa Congo DR anayemmiliki Mchezaji Mayele na Wachezaji wengine 23 walioko Ulaya na baadhi ya nchi za Bara la Afrika.
 
Maandiko yako yamejaa kejeli na jazba za wivu ndani yake
 
Yanga tumefanya biashara nzuri 3b ni pesa ndefu kumbuka Mayele tulimpata kama free agent
Tukamunoa sasa tumemuuza pesa ndefu hongereni viongozi wa yanga

Mwakani tunaamuza Musonda 5b na Job

Namtakia kila la heri Fiston
Nidhamu, bidii yake naamini atafanikiwa
Miezi mitatu kutoka sasa rudi hapa uyarudia maneno yako haya
 
Yanga SC wakiambulia Pesa nyingi ya Mgao basi itakuwa ni Shilingi Elfu Mbili ( Tsh 2,000/= ) tu za Kitanzania na watakaopata nyingi ni Klabu yake ya AS Vita, Maniema FC na Tajiri wa Congo DR anayemmiliki Mchezaji Mayele na Wachezaji wengine 23 walioko Ulaya na baadhi ya nchi za Bara la Afrika.
Wewe ndio mke wa huyo tajiri?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Baada ya kumkosa mchezaji wao waliyekuwa wanamtegemea hatimaye waamua kama mbwayi na iwe mbwayi wamfanyia Bonge la Utambulisho Mwamba Mayele. Hatimaye kimeeleweka ni Pyramid na Ufalme mpya wa Mayele pale Misri.
.
.
.
.
#solomatv_updates
96a2c6b075814c60be6be9da14b29fd9_363364832_18197983867271475_637726271393576236_n.jpg
925ce55ec0fb4675829aff7d5ac50785_362249988_18197983939271475_2638917497723122399_n.jpg
fc9b1b46bf5241f092c86bd48698f31e_363362902_18197983918271475_1151010637464748103_n.jpg
4d23d58369484b54a9e2aefdf13d5e11_364027991_18197983927271475_5671782732998015679_n.jpg
8a61cfb661c54bcda11909a9f4faaee2_364171409_18197983882271475_2868872837038642439_n.jpg
936bc88c21a04c14ada7eefb11cfefd8_363369620_18197983891271475_6380067403868678825_n.jpg
7bd7eb769aa64f7aa57187233cad7f43_364243907_18197983909271475_8421581151004402817_n.jpg
 
Back
Top Bottom