Sasa ni rasmi, Fiston Kalala Mayele atambulishwa Pyramid FC ya Misri

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2020
Posts
8,542
Reaction score
18,340
Your browser is not able to display this video.


Club ya Pyramid FC ya Misri imetangaza kumsajli Mshambuliaji wa Kimataifa wa Congo DR Fiston Kalala Mayele (29) kutokea Yanga SC ya Tanzania.

Mayele anaondoka Yanga baada ya kucheza misimu miwili Tanzania kwa maanikio makubwa msimu wa kwanza 2021/2022 alimaliza nafasi ya pili kwa ufungaji magoli 16.

Msimu wa 2022/2023 akiibuka MVP wa Ligi Kuu Tanzania bara sambamba na tuzo ya Mfungaji bora wa Ligi sawa na Said Ntibazonkiza wa Simba wote wakifunga magoli 17.

Mayele anaondoka Yanga baada ya kuisaidia kutwaa taji la Ligi Kuu mara 2, FA Cup 2 Ngao ya Jami mara mbili na kuisaidia Yanga kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza katika historia yao msimu 2022/2023 na ndio Mfungaji bora wa Michuano hiyo akimaliza a magoli 7
 
Club ya Pyramid FC ya Misri imetangaza kumsajili Mshambuliaji wa Kimataifa wa Congo DR Fiston Kalala Mayele (29) kutokea Yanga SC ya Tanzania.

Mayele anaondoka Yanga baada ya kucheza misimu miwili Tanzania kwa mafanikio makubwa msimu wa kwanza 2021/2022 alimaliza nafasi ya pili kwa ufungaji magoli 16.

Msimu wa 2022/2023 akiibuka MVP wa Ligi Kuu Tanzania bara sambamba na tuzo ya Mfungaji bora wa Ligi sawa na Saido Ntibazonkiza wa Simba wote wakifunga magoli 17.

Mayele anaondoka Yanga baada ya kuisaidia kutwaa taji la Ligi Kuu mara 2, FA Cup 2 Ngao ya Jamii mara mbili na kuisaidia Yanga kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza katika historia yao msimu 2022/2023 na ndio Mfungaji bora wa Michuano hiyo akimaliza na magoli 7.
 
KWAHERI Mayele Kila LAKHERI huko uendako.

MAMBO KUMI YA FISTON MAYELE.

1.Ulikuwa mshambuliaji Bora.
2. Ulikuwa mchezaji unayejituma mno.
3. Ulikuwa mchezaji unaejitoa sana.

4.Ulikuwa mchezaji MWENYE Nidhamu mno.
5. Ulikuwa mchezaji PENDWA sana.
6. Ulikuwa Unazungumza kiswahili kuliko mchezaji yoyote yule kutoka DRC.

7. STAYLE yako (ya Kongo)Ya ushambuliaji ilikuwa na msisimko WA Hali ya juu.

8. Ulishiriki vizuri Ibada za KANISA lako ST Peter.

9. Ulikuwa na Familia Bora sana

10. Hakika Mwamba Ulitetema.

HATA MASHABIKI WA SIMBA TUKIWA NYUMBANI TULIKUWA TUNAJARIBU KUTETEMA.
 
Ni ngumu sana kwa Wabantu kutoboa kwenye Ligi za hapo uarabuni. Sitoshangaa Mayele akishindwana nao!
Inawezekana mkuu
Pale Al Ahly panga pangua , Alou Dieng na Percy Tau lazima waanze
Kule Wydad fanya ufanyavyo ila Zoa lazima aanze hata kama ana bandeji kichwani
USM Alger watapanga kikosi ila lazima Orebonye aanze
Kwa hiyo nkuu inawezekana Kwa mwamba kutoboa,muhimu akiendeleza discipline yake aliyokua nayo Yanga
Jamaa mtu Sana Yule, we wish him all the best
 
Mpaka sasa Pyramid bado hawajaingiza hata senti tano kwenye akaunti ya Yanga kwa ajili ya malipo ya kumnunua Mayele.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yanga tumefanya biashara nzuri 3b ni pesa ndefu kumbuka Mayele tulimpata kama free agent
Tukamunoa sasa tumemuuza pesa ndefu hongereni viongozi wa yanga

Mwakani tunaamuza Musonda 5b na Job

Namtakia kila la heri Fiston
Nidhamu, bidii yake naamini atafanikiwa
 
Ameen
 


MANIEMA UNION.
 
Daaaah 😳😳😳 Sa itakuwaje au skudu ndo mwokozi wetu aliyebaki? Tumpe thank you yake basi, tuache vinyongo
Umeshamaliza kumfundisha Bocco kuwa golikipa? Ukishamaliza inabidi ukajifuze nafasi za wachezaji na majukumu yao makuu. Nani aliyekwambia Skudu kaja kuchukua nafasi ya Mayele?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…