Sasa ni rasmi ili Taifa Stars ifuzu AFCON Kesho ' Babu Mtaalam ' kutoka Pemba kasema Kikosi Kipangwe hiki kwa dakika zote 90 Kisibadilike

Sasa ni rasmi ili Taifa Stars ifuzu AFCON Kesho ' Babu Mtaalam ' kutoka Pemba kasema Kikosi Kipangwe hiki kwa dakika zote 90 Kisibadilike

Ni hivi tunampiga mtu goli 3

Na goli moja ni la penati
 
1. Aishi Manula
2. Ramadhan Kessy
3. Abdi Banda
4. Erasto Nyoni
5. Kelvin Yondan
6. Jonas Mkude
7. Simon Msuva
8. Mudhathir Yahaya
9. Shaban Chilunda
10. John Boko
11. Shiza Kichuya


Ni huyu huyu ' Babu Mtaalam ' wangu kutoka Pemba ndiyo alikuwa akinihakikishia mechi zote za Simba SC dhidi ya Yanga SC na matokeo yake huwa kama vile ambavyo huniambia na hajawahi Kukosea hata siku moja.

Narudia tena Kikosi kisibadilike hadi Filimbi ya mwisho kwani kimekaa vizuri kwa Nyota ya Kesho na mambo mengine yote ya ' Kitaalam / Kiushirikina ' ambao ndiyo ' Utamaduni ' wetu nchi nyingi za Kiafrika.

Kikicheza hiki hadi mwisho kuna Magoli ama 3 kwa 1 au 2 kwa 0 Taifa Stars yetu itashinda Kesho na hatimaye kujiweka katika mazingira mazuri ya Kufuzu AFCON mwakani baada ya ukame wa miaka 38 ya Kutoshiriki.

Kazi kwenu TFF na wale mliopo na Timu huko Lesotho msiseme GENTAMYCINE sikuwaambieni.

Nawasilisha.
Match inaanza saa ngap?
 
Nimeweka Kikosi cha ' Kimkakati ' cha Ushindi na chenye Nyota ya Ushindi kwa mechi ya Kesho kama ambavyo nimeelekezwa na huyo ' Babu Mtaalam ' hivyo hao wengine unaonitajia Wewe hapa subiri mechi zingine utawapanga ila kwa mechi muhimu ya Kesho dhidi ya Lesotho Timu ikipangwa hivyo tutashinda na Kufuzu kwa mara ya pili huko AFCON baada ya Kukosa Kushiriki kwa miaka takribani 38.

Uyo mzee wa pemba ni kocha wa timu gani?
 
Weka list pembeni bandika Zanzibar Heroes hapo in a rush.
 
Back
Top Bottom