Sasa ni rasmi ili Taifa Stars ifuzu AFCON Kesho ' Babu Mtaalam ' kutoka Pemba kasema Kikosi Kipangwe hiki kwa dakika zote 90 Kisibadilike

Sasa ni rasmi ili Taifa Stars ifuzu AFCON Kesho ' Babu Mtaalam ' kutoka Pemba kasema Kikosi Kipangwe hiki kwa dakika zote 90 Kisibadilike

Ngoja tusubiri muda ufike saa kumi na Moja sio mbali

Mungu ibariki Taifa stars
 
1. Aishi Manula
2. Ramadhan Kessy
3. Abdi Banda
4. Erasto Nyoni
5. Kelvin Yondan
6. Jonas Mkude
7. Simon Msuva
8. Mudhathir Yahaya
9. Shaban Chilunda
10. John Boko
11. Shiza Kichuya


Ni huyu huyu ' Babu Mtaalam ' wangu kutoka Pemba ndiyo alikuwa akinihakikishia mechi zote za Simba SC dhidi ya Yanga SC na matokeo yake huwa kama vile ambavyo huniambia na hajawahi Kukosea hata siku moja.

Narudia tena Kikosi kisibadilike hadi Filimbi ya mwisho kwani kimekaa vizuri kwa Nyota ya Kesho na mambo mengine yote ya ' Kitaalam / Kiushirikina ' ambao ndiyo ' Utamaduni ' wetu nchi nyingi za Kiafrika.

Kikicheza hiki hadi mwisho kuna Magoli ama 3 kwa 1 au 2 kwa 0 Taifa Stars yetu itashinda Kesho na hatimaye kujiweka katika mazingira mazuri ya Kufuzu AFCON mwakani baada ya ukame wa miaka 38 ya Kutoshiriki.

Kazi kwenu TFF na wale mliopo na Timu huko Lesotho msiseme GENTAMYCINE sikuwaambieni.

Nawasilisha.
Kwanini Ujenzi Rukwa ilishuka daraja ?
 
Nimeweka Kikosi cha ' Kimkakati ' cha Ushindi na chenye Nyota ya Ushindi kwa mechi ya Kesho kama ambavyo nimeelekezwa na huyo ' Babu Mtaalam ' hivyo hao wengine unaonitajia Wewe hapa subiri mechi zingine utawapanga ila kwa mechi muhimu ya Kesho dhidi ya Lesotho Timu ikipangwa hivyo tutashinda na Kufuzu kwa mara ya pili huko AFCON baada ya Kukosa Kushiriki kwa miaka takribani 38.
baba muombe huyo mtaalamu amuondoe kessi maana
 
Nmeona kikosi kocha kapanga mabeki kuanzia namba 2 mpka namba 9.
 
kikos kinachoanza leo TANZANIA vs LESOTHO saa 11 kamili.
98f00e2e6b59ea54997243b3ad7229a5.jpg


Sent from my TECNO H5 using JamiiForums mobile app
 
Huyo babu mtaalam wako toka Pemba atukome!! Asiibe utukufu wa Mungu maana watanzania tumemwomba Mungu ili timu yetu ishinde.. Sasa ikishinda usije kusema ni utaalamu wa huyo babu mchawi koko!!!, bali ni majibu ya Mungu aliye hai kwa maombi yetu watanzania!!!!
 
Back
Top Bottom