GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
- Thread starter
-
- #101
weka ushaidi sio maneno na huache kujiona bora kuliko wengine
Itasaidia nini? ? Husda tuu imekujaaAhsante mkuu hivi Malinzi anasubiria nini kujiuzulu ?? Jamaa kafanya udukuzi wa hali ya juu. Malinzi must resign as TFF boss.
mm sijapinga huo ushaidi wako bali kwenye comment zako kuna member umewazarau na jf sio sehemu ya tetesi kama fb weka ushaidi wa ubigwa wa azam kila mtu auone si porojo
duuh ina maana ule ubingwa wa azam una mambo yake, basi tumeuzwa zaidi ya tujuavyo
Huu Uzi sio wa Azam fc,huu ni maalum kwa ajili ya Malinzi kupanga matokeo,mbona mgumu kuelewa? Au ndio kusema kwa kuwa wewe wa rufiji basi unataka kila mtu awe kama wewe? Usituchanganyie habari tafadhalimm sijapinga huo ushaidi wako bali kwenye comment zako kuna member umewazarau na jf sio sehemu ya tetesi kama fb weka ushaidi wa ubigwa wa azam kila mtu auone si porojo
Na kwa TAARIFA yako tu mpangaji mzima wa ule ubingwa wao alikuwa ni Saad Kawemba CEO wa sasa wa Azam FC ambaye siku nitakuja na HABARI yake kamili ili mjue nini kinaendelea katika soka la bongo. Mkuu kazi hizi za UDUKUZI hatukuzianza leo wala jana na tumeshatishiwa hadi maisha lakini TUNAKOMAA kwani wengine hata maisha yetu tayari tumeshayaweka rehani na nitafurahi sana nikifa wakati nikifanya kazi yangu hii kwa maslahi ya nchi na Watanzania wenzangu ili huko mbeleni vizazi vije kunikumbuka.
huo ukanda unatoka wapi sasa nduguHuu Uzi sio wa Azam fc,huu ni maalum kwa ajili ya Malinzi kupanga matokeo,mbona mgumu kuelewa? Au ndio kusema kwa kuwa wewe wa rufiji basi unataka kila mtu awe kama wewe? Usituchanganyie habari tafadhali
kweli ww jamaa abunuasi tukukumbuke ww kwani ww ndo uliyoigundua hii kashifa kama lengo ndo hilo umepotea kijana itakukumbuka familia yako tu weka humu ushaidi sio porojoNa kwa TAARIFA yako tu mpangaji mzima wa ule ubingwa wao alikuwa ni Saad Kawemba CEO wa sasa wa Azam FC ambaye siku nitakuja na HABARI yake kamili ili mjue nini kinaendelea katika soka la bongo. Mkuu kazi hizi za UDUKUZI hatukuzianza leo wala jana na tumeshatishiwa hadi maisha lakini TUNAKOMAA kwani wengine hata maisha yetu tayari tumeshayaweka rehani na nitafurahi sana nikifa wakati nikifanya kazi yangu hii kwa maslahi ya nchi na Watanzania wenzangu ili huko mbeleni vizazi vije kunikumbuka.
Nilikuwa nasubiri kwa hamu sana mtu aje na hoja kama yako halafu nishushe nondo ili nikufundishe jinsi ya kufikiri na kujenga hoja iliyo timilifu mbele ya " majiniasi " tuliobobea humu. Umesema kuwa Malinzi hausiki na ukanidhihaki huku ukiwataka Moderators wautoe huu uzi sasa naweka hapa mazingira makuu manne ( 4 ) kisha nataka nipime uelewa wako katika kufanya critical thinking analysis na judgmental logical reasoning na ukinijibu ndipo nitajua uwezo wako wa kufikiri:
Mwisho naomba nikuulize Je:
- Katika hiyo clip kuna mtu amesikika wazi wazi akisema ametumwa na Rais Malinzi kwenda Geita kwa kazi maalum. Na kumbuka hicho kikao kilikaliwa siku 8 kabla ya mechi ya Geita Gold FC na FC Kanembwa. Je Malinzi ni nani TFF? Je huyo mjumbe wa TFF ameongopa wakati hicho kikao kilikaliwa na kuna mtu alihisi kuwa huko mbeleni wangerukana hivyo akajiongeza na kuwarekodi pasipo wao kushtuka.
- Kamati ya Mashindano ya TFF aliyokuwa akiiongoza Bwana Chacha aliyejiuzuru juzi ipo chini ya nani? Bwana Chacha anaweza kufanya mambo bila ridhaa au baraka za Kiongozi wake Rais wa TFF Bwana Jamal Malinzi?
- Kamati ya NIDHAMU ya TFF inawajibika kwa nani ukiondoa Katibu Mkuu wa TFF na Rais wa TFF? Kamati hiyo ya NIDHAMU ya TFF inaweza kukaa na kuamua yao bila MSUKUMO au BARAKA za Kiongozi wa juu wa TFF ambaye ni Rais Malinzi? Kwanini katika vile vikao vyao vyote wale wajumbe wawili walipoingia mule ndani kuhojiwa na wakatoa sauti ya MAAGIZO aliyokuwa akiyatoa Malinzi Mwenyekiti Tarimba akashurutishwa ahairishe kikao ili wajipange upya?
- Jana tu mtu wa karibu kabisa na Rais Malinzi Bwana Matandika amefukuzwa kazi ghafla wakati ni huyu huyu mtu ndiye anasikika karibu katika hizo clips zote akitoa MAELEKEZO. Je huyu jamaa Matandiko alikuwa anapata hayo MAAGIZO kutoka wapi kama siyo kwa Bosi wake Rais Malinzi?
Mwisho nikusihi tu siku nyingine kama ukiona huna UWEZO wa KUFIKIRI au kujenga HOJA mbele yangu tafadhali naomba usiwe unanisumbua kwani ubongo wangu una allergy na IDIOTS wa mfano wako. Na namalizia kwa KUSITITIZA tena bila UWOGA kuwa RAIS WA TFF NDUGU JAMAL MALINZI AMEHUSIKA MOJA KWA MOJA NA UPANGAJI HUU WA MATOKEO NA HASA HASA AKITAKA KUIBEBA TIMU YA GEITA GOLD FC ILI KURUDISHA FADHILA KWAO KWAKUWA TFF ILIPOISHIWA PESA NA PALE TRA WALIPOZUIA AKAUNTI YAO NA KUCHUKUA PESA WALIISHIWA NA IKABIDI JAMAL MALINZI RAIS WA TFF AENDE KWA RAFIKI YAKE MKUBWA ALIYEPO MGODINI HUKO AOMBE MSAADA WA HELA NA AKAPEWA LAKINI KAWA SHARTI KUU LA KUWASAIDIA WAPANDE LIGI KUU.
- Unajua kwanini Bwana Chacha AMEJIUZURU ghafla?
- Unajua CHANGA LA MACHO tulilopigwa kwa huyu Bwana Matandika KUFUKUZWA kazi ghafla jana?
- Unajua kwanini hizi SIRI zote sasa zinawekwa wazi?
- Unajua WAANDISHI wa habari za Michezo hasa wa MAGAZETI wamepewa TAKRIMA gani jana ili leo WASIRIPOTI hii kitu?
Una mengi sana ya kujifunza kutoka kwangu. Pata kwanza UFAFANUZI huu na ukiwa na swali jingine zaidi niulize kwani huwa napenda mno KUMBADILI KIFIKRA MPUUZI!
duuh ina maana ule ubingwa wa azam una mambo yake, basi tumeuzwa zaidi ya tujuavyo
safi aweke hoja kama malinzi kausika awajibike lakini sio porojoMkuu hizi zote ni tuhuma, tuwahukumu kwanza Chacha na Matandika ambao sauti zao zimesikika na ndo maana mmoja kajipima kaona aondoke mwenyewe na mwingne naona unasema kafukuzwa kazi tayari. Hii ni kwasababu hawa ushaidi wa sauti upo wazi kabisa ndo maana hatua zimechukuliwa haraka sana.
Kwenye clip hatuwezi kumuamin huyu aliyesema kwamba katumwa na Malinzi kwasababu anaweza kulitumia jina la Malinzi ili dau lake liwe kubwa sana.
Kwenye hili la kupokea hela ya kuendeshea ofisi kwa sharti la kuipandisha tim inabidi utupe ushahidi ili na sisi tukuunge mkono kwenye hili make ni kama unatulisha maneno bila ushahidi.
NOTE:
Jenga hoja ya Malinzi kujiuzuru kwa makosa ya watendaji wa chini yake ila sio aliyoyafanya yeye kwenye hili la upangaji matokeo make hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaomhusisha yeye mwenyewe
wambura huyu huyu ambae ezi zake na ndoranga kunachimbika leo malaika kule kwenye bodi ya stand united kilitokea nn kama sio upigaji bado sijaona kiongozi msafi tenga mwenye kaondoka kaacha deni tra chanzo cha kukamatwa mabasi lakini watu wanajua haya madeni ya malinzi bado sijamwona msafi wakuiongoza tffMalinzi mwenyewe kasema popote kwenye hela utamkuta . Huyu jamaa bora mngempa Wambura Richard Lawyer by Professional the guy is very smart. ILA huyu jamaa kwa kweli Ni kichomi Na kirusi kikubwa. MALINZI MUST GO.
Mkuu hizi zote ni tuhuma, tuwahukumu kwanza Chacha na Matandika ambao sauti zao zimesikika na ndo maana mmoja kajipima kaona aondoke mwenyewe na mwingne naona unasema kafukuzwa kazi tayari. Hii ni kwasababu hawa ushaidi wa sauti upo wazi kabisa ndo maana hatua zimechukuliwa haraka sana.
Kwenye clip hatuwezi kumuamin huyu aliyesema kwamba katumwa na Malinzi kwasababu anaweza kulitumia jina la Malinzi ili dau lake liwe kubwa sana.
Kwenye hili la kupokea hela ya kuendeshea ofisi kwa sharti la kuipandisha tim inabidi utupe ushahidi ili na sisi tukuunge mkono kwenye hili make ni kama unatulisha maneno bila ushahidi.
NOTE:
Jenga hoja ya Malinzi kujiuzuru kwa makosa ya watendaji wa chini yake ila sio aliyoyafanya yeye kwenye hili la upangaji matokeo make hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaomhusisha yeye mwenyewe