Sasa ni rasmi Rais wa TFF, Jamal Malinzi amehusika na upangaji matokeo

Sasa ni rasmi Rais wa TFF, Jamal Malinzi amehusika na upangaji matokeo

weka ushaidi sio maneno na huache kujiona bora kuliko wengine

Kama mpaka sasa huna clip yenye mazingira yote ya USHAHIDI huo unaoutaka kwanini unadhani nisijione bora kuliko wewe? Siyo kosa langu kukufanya uwe na huo UPEO wako mdogo mkuu ila najiona bora kwa kuwa najua ninachokisema, nakisimamia na nakijengea hoja zenye mashiko. Huwa nasikia raha sana kujibu post za wenye uvivu wa kufikiri wa aina yako hii.
 
mm sijapinga huo ushaidi wako bali kwenye comment zako kuna member umewazarau na jf sio sehemu ya tetesi kama fb weka ushaidi wa ubigwa wa azam kila mtu auone si porojo
 
Ahsante mkuu hivi Malinzi anasubiria nini kujiuzulu ?? Jamaa kafanya udukuzi wa hali ya juu. Malinzi must resign as TFF boss.
Itasaidia nini? ? Husda tuu imekujaa
 
mm sijapinga huo ushaidi wako bali kwenye comment zako kuna member umewazarau na jf sio sehemu ya tetesi kama fb weka ushaidi wa ubigwa wa azam kila mtu auone si porojo

Nakusihi pitia upya threads zangu zote za masuala NYETI kama haya humu JF kisha niambie ni ipi ambayo haikuwa ya kweli na haijaleta impact. Hata wewe nimeshakudharau na usinipotezee muda tafadhali. Fungulia E fm sasa hivi usikilize WANAMUME wenye AKILI, MAARIFA na UPEO wanavyochambua hili SUALA. Na ndiyo maana NAWADHARAU kwakuwa mna UPEO hafifu!
 
duuh ina maana ule ubingwa wa azam una mambo yake, basi tumeuzwa zaidi ya tujuavyo

Na kwa TAARIFA yako tu mpangaji mzima wa ule ubingwa wao alikuwa ni Saad Kawemba CEO wa sasa wa Azam FC ambaye siku nitakuja na HABARI yake kamili ili mjue nini kinaendelea katika soka la bongo. Mkuu kazi hizi za UDUKUZI hatukuzianza leo wala jana na tumeshatishiwa hadi maisha lakini TUNAKOMAA kwani wengine hata maisha yetu tayari tumeshayaweka rehani na nitafurahi sana nikifa wakati nikifanya kazi yangu hii kwa maslahi ya nchi na Watanzania wenzangu ili huko mbeleni vizazi vije kunikumbuka.
 
mm sijapinga huo ushaidi wako bali kwenye comment zako kuna member umewazarau na jf sio sehemu ya tetesi kama fb weka ushaidi wa ubigwa wa azam kila mtu auone si porojo
Huu Uzi sio wa Azam fc,huu ni maalum kwa ajili ya Malinzi kupanga matokeo,mbona mgumu kuelewa? Au ndio kusema kwa kuwa wewe wa rufiji basi unataka kila mtu awe kama wewe? Usituchanganyie habari tafadhali
 
Na kwa TAARIFA yako tu mpangaji mzima wa ule ubingwa wao alikuwa ni Saad Kawemba CEO wa sasa wa Azam FC ambaye siku nitakuja na HABARI yake kamili ili mjue nini kinaendelea katika soka la bongo. Mkuu kazi hizi za UDUKUZI hatukuzianza leo wala jana na tumeshatishiwa hadi maisha lakini TUNAKOMAA kwani wengine hata maisha yetu tayari tumeshayaweka rehani na nitafurahi sana nikifa wakati nikifanya kazi yangu hii kwa maslahi ya nchi na Watanzania wenzangu ili huko mbeleni vizazi vije kunikumbuka.

aisee umenifungua sana macho, nashauri katiba ya tff itamke wazi mtu atapata uongozi wa tff baadaa ya kufanyiwa vetting ya kutosha kuondoa madoa doa kama hayo, endelea kutujuza mkuu
 
Huu Uzi sio wa Azam fc,huu ni maalum kwa ajili ya Malinzi kupanga matokeo,mbona mgumu kuelewa? Au ndio kusema kwa kuwa wewe wa rufiji basi unataka kila mtu awe kama wewe? Usituchanganyie habari tafadhali
huo ukanda unatoka wapi sasa ndugu
 
Na kwa TAARIFA yako tu mpangaji mzima wa ule ubingwa wao alikuwa ni Saad Kawemba CEO wa sasa wa Azam FC ambaye siku nitakuja na HABARI yake kamili ili mjue nini kinaendelea katika soka la bongo. Mkuu kazi hizi za UDUKUZI hatukuzianza leo wala jana na tumeshatishiwa hadi maisha lakini TUNAKOMAA kwani wengine hata maisha yetu tayari tumeshayaweka rehani na nitafurahi sana nikifa wakati nikifanya kazi yangu hii kwa maslahi ya nchi na Watanzania wenzangu ili huko mbeleni vizazi vije kunikumbuka.
kweli ww jamaa abunuasi tukukumbuke ww kwani ww ndo uliyoigundua hii kashifa kama lengo ndo hilo umepotea kijana itakukumbuka familia yako tu weka humu ushaidi sio porojo
 
Nilikuwa nasubiri kwa hamu sana mtu aje na hoja kama yako halafu nishushe nondo ili nikufundishe jinsi ya kufikiri na kujenga hoja iliyo timilifu mbele ya " majiniasi " tuliobobea humu. Umesema kuwa Malinzi hausiki na ukanidhihaki huku ukiwataka Moderators wautoe huu uzi sasa naweka hapa mazingira makuu manne ( 4 ) kisha nataka nipime uelewa wako katika kufanya critical thinking analysis na judgmental logical reasoning na ukinijibu ndipo nitajua uwezo wako wa kufikiri:

  1. Katika hiyo clip kuna mtu amesikika wazi wazi akisema ametumwa na Rais Malinzi kwenda Geita kwa kazi maalum. Na kumbuka hicho kikao kilikaliwa siku 8 kabla ya mechi ya Geita Gold FC na FC Kanembwa. Je Malinzi ni nani TFF? Je huyo mjumbe wa TFF ameongopa wakati hicho kikao kilikaliwa na kuna mtu alihisi kuwa huko mbeleni wangerukana hivyo akajiongeza na kuwarekodi pasipo wao kushtuka.
  2. Kamati ya Mashindano ya TFF aliyokuwa akiiongoza Bwana Chacha aliyejiuzuru juzi ipo chini ya nani? Bwana Chacha anaweza kufanya mambo bila ridhaa au baraka za Kiongozi wake Rais wa TFF Bwana Jamal Malinzi?
  3. Kamati ya NIDHAMU ya TFF inawajibika kwa nani ukiondoa Katibu Mkuu wa TFF na Rais wa TFF? Kamati hiyo ya NIDHAMU ya TFF inaweza kukaa na kuamua yao bila MSUKUMO au BARAKA za Kiongozi wa juu wa TFF ambaye ni Rais Malinzi? Kwanini katika vile vikao vyao vyote wale wajumbe wawili walipoingia mule ndani kuhojiwa na wakatoa sauti ya MAAGIZO aliyokuwa akiyatoa Malinzi Mwenyekiti Tarimba akashurutishwa ahairishe kikao ili wajipange upya?
  4. Jana tu mtu wa karibu kabisa na Rais Malinzi Bwana Matandika amefukuzwa kazi ghafla wakati ni huyu huyu mtu ndiye anasikika karibu katika hizo clips zote akitoa MAELEKEZO. Je huyu jamaa Matandiko alikuwa anapata hayo MAAGIZO kutoka wapi kama siyo kwa Bosi wake Rais Malinzi?
Mwisho naomba nikuulize Je:

  1. Unajua kwanini Bwana Chacha AMEJIUZURU ghafla?
  2. Unajua CHANGA LA MACHO tulilopigwa kwa huyu Bwana Matandika KUFUKUZWA kazi ghafla jana?
  3. Unajua kwanini hizi SIRI zote sasa zinawekwa wazi?
  4. Unajua WAANDISHI wa habari za Michezo hasa wa MAGAZETI wamepewa TAKRIMA gani jana ili leo WASIRIPOTI hii kitu?
Mwisho nikusihi tu siku nyingine kama ukiona huna UWEZO wa KUFIKIRI au kujenga HOJA mbele yangu tafadhali naomba usiwe unanisumbua kwani ubongo wangu una allergy na IDIOTS wa mfano wako. Na namalizia kwa KUSITITIZA tena bila UWOGA kuwa RAIS WA TFF NDUGU JAMAL MALINZI AMEHUSIKA MOJA KWA MOJA NA UPANGAJI HUU WA MATOKEO NA HASA HASA AKITAKA KUIBEBA TIMU YA GEITA GOLD FC ILI KURUDISHA FADHILA KWAO KWAKUWA TFF ILIPOISHIWA PESA NA PALE TRA WALIPOZUIA AKAUNTI YAO NA KUCHUKUA PESA WALIISHIWA NA IKABIDI JAMAL MALINZI RAIS WA TFF AENDE KWA RAFIKI YAKE MKUBWA ALIYEPO MGODINI HUKO AOMBE MSAADA WA HELA NA AKAPEWA LAKINI KAWA SHARTI KUU LA KUWASAIDIA WAPANDE LIGI KUU.

Una mengi sana ya kujifunza kutoka kwangu. Pata kwanza UFAFANUZI huu na ukiwa na swali jingine zaidi niulize kwani huwa napenda mno KUMBADILI KIFIKRA MPUUZI!

Mkuu hizi zote ni tuhuma, tuwahukumu kwanza Chacha na Matandika ambao sauti zao zimesikika na ndo maana mmoja kajipima kaona aondoke mwenyewe na mwingne naona unasema kafukuzwa kazi tayari. Hii ni kwasababu hawa ushaidi wa sauti upo wazi kabisa ndo maana hatua zimechukuliwa haraka sana.

Kwenye clip hatuwezi kumuamin huyu aliyesema kwamba katumwa na Malinzi kwasababu anaweza kulitumia jina la Malinzi ili dau lake liwe kubwa sana.

Kwenye hili la kupokea hela ya kuendeshea ofisi kwa sharti la kuipandisha tim inabidi utupe ushahidi ili na sisi tukuunge mkono kwenye hili make ni kama unatulisha maneno bila ushahidi.

NOTE:
Jenga hoja ya Malinzi kujiuzuru kwa makosa ya watendaji wa chini yake ila sio aliyoyafanya yeye kwenye hili la upangaji matokeo make hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaomhusisha yeye mwenyewe
 
Malinzi mwenyewe kasema popote kwenye hela utamkuta . Huyu jamaa bora mngempa Wambura Richard Lawyer by Professional the guy is very smart. ILA huyu jamaa kwa kweli Ni kichomi Na kirusi kikubwa. MALINZI MUST GO.
duuh ina maana ule ubingwa wa azam una mambo yake, basi tumeuzwa zaidi ya tujuavyo
 
Ule ubingwa wa azam kwa aliyeshuhudia mechi Yao ya mwisho pale sokoine na mbeya city Huwezi mbishia mtoa Mada.
 
Kama uko mkoani unaweza kusikiliza efm kupitia tuneln radio. unaidownload kutoka play store.
 
Mkuu hizi zote ni tuhuma, tuwahukumu kwanza Chacha na Matandika ambao sauti zao zimesikika na ndo maana mmoja kajipima kaona aondoke mwenyewe na mwingne naona unasema kafukuzwa kazi tayari. Hii ni kwasababu hawa ushaidi wa sauti upo wazi kabisa ndo maana hatua zimechukuliwa haraka sana.

Kwenye clip hatuwezi kumuamin huyu aliyesema kwamba katumwa na Malinzi kwasababu anaweza kulitumia jina la Malinzi ili dau lake liwe kubwa sana.

Kwenye hili la kupokea hela ya kuendeshea ofisi kwa sharti la kuipandisha tim inabidi utupe ushahidi ili na sisi tukuunge mkono kwenye hili make ni kama unatulisha maneno bila ushahidi.

NOTE:
Jenga hoja ya Malinzi kujiuzuru kwa makosa ya watendaji wa chini yake ila sio aliyoyafanya yeye kwenye hili la upangaji matokeo make hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaomhusisha yeye mwenyewe
safi aweke hoja kama malinzi kausika awajibike lakini sio porojo
 
Malinzi mwenyewe kasema popote kwenye hela utamkuta . Huyu jamaa bora mngempa Wambura Richard Lawyer by Professional the guy is very smart. ILA huyu jamaa kwa kweli Ni kichomi Na kirusi kikubwa. MALINZI MUST GO.
wambura huyu huyu ambae ezi zake na ndoranga kunachimbika leo malaika kule kwenye bodi ya stand united kilitokea nn kama sio upigaji bado sijaona kiongozi msafi tenga mwenye kaondoka kaacha deni tra chanzo cha kukamatwa mabasi lakini watu wanajua haya madeni ya malinzi bado sijamwona msafi wakuiongoza tff
 
Mkuu hizi zote ni tuhuma, tuwahukumu kwanza Chacha na Matandika ambao sauti zao zimesikika na ndo maana mmoja kajipima kaona aondoke mwenyewe na mwingne naona unasema kafukuzwa kazi tayari. Hii ni kwasababu hawa ushaidi wa sauti upo wazi kabisa ndo maana hatua zimechukuliwa haraka sana.

Kwenye clip hatuwezi kumuamin huyu aliyesema kwamba katumwa na Malinzi kwasababu anaweza kulitumia jina la Malinzi ili dau lake liwe kubwa sana.

Kwenye hili la kupokea hela ya kuendeshea ofisi kwa sharti la kuipandisha tim inabidi utupe ushahidi ili na sisi tukuunge mkono kwenye hili make ni kama unatulisha maneno bila ushahidi.

NOTE:
Jenga hoja ya Malinzi kujiuzuru kwa makosa ya watendaji wa chini yake ila sio aliyoyafanya yeye kwenye hili la upangaji matokeo make hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaomhusisha yeye mwenyewe

Bandiko refu lakini ni full of TITO and GIGO. Umenitaka nijenge hoja kuwa Rais wa TFF Jamal Malinzi anahusikaje hivyo naanza sasa kukujibu na ili kuonyesha kuwa kazi naijua na naiweza najua kuwa kuna vijana tena waandishi wa habari 7 na Wafanyakazi 3 loyal kwa Bosi wenu Malinzi mmepewa kazi MAALUM ya kuja kunijibu huku na kunipinga ili kukwepesha lengo na tayari kwa msaada wa Mtaalam wangu wa IT na wa Mtu mliyenae hapo hapo TFF nimeshakujua wewe ni nani ila nakustahi tu nisije kukuharibia image yako kwa Wapenda soka lakini ukiendelea kujifanya kichwa ngumu namwaga identity yako hapa hapa ili wakujue.

Umesema Jamal Malinzi Rais wa TFF hahusiki sasa naomba uniambie hawa Watu wafuatao wanawajibika kwa nani na iweje wote wawepo katika zile clips na inserts zote tulizozisikia jana na leo E fm na Clouds fm :

  1. Bwana Chacha ( MKURUGENZI WA MASHINDANO WA TFF ).
  2. Bwana Matandika ( MSAIDIZI WA KARIBU SANA WA RAIS WA TFF JAMAL MALINZI KATIKA UTENDAJI ).
  3. Bwana Kulunge ( MWENYEKITI WA TFF MKOA WA GEITA ).
Kama leo unasema KUWA NAMSINGIZIA RAIS MALINZI WA TFF Basi naomba na wewe pia unijibu hao watu watatu hapo juu WANAWAJIBIKA KILA SIKU KWA NANI? Kuna mwenzako mmoja alikuja na swali kama wewe na nikamwelewesha huku nikimtaka akapate msaada wa Kisheria ili ajiridhishe na nikajua kuwa hata wewe utakuwa uliipitia kumbe hukufanya hivyo. Mwisho niendelee tena KUWASIHI WATANZANIA ACHENI KUISHI KAMA MBAYU WAYU KWAMBA ILI IAMINIKE RAIS WA TFF JAMAL MALINZI KAHUSIKA BASI NI LAZIMA YEYE KAMA YEYE ASIKIKE SAUTI YAKE AU AONEKANE AKIFANYA KITENDO CHA UFISADI BALI TAMBUENI KUWA KISHERIA MTU HUHUKUMIWA HATA TU KWA MAZINGIRA YANAYOJITOSHELEZA KAMA YA HAPO JUU NILIYOYAELEZA NA YALIYOPO KATIKA CLIPS ZOTE.

Hivi :

  • Rais Mstaafu Mzee wetu Mwinyi alipojiuzuru miaka ya 80 akiwa Waziri baada ya UFISADI / UBADHIRIFU kutokea katika ile Wizara yeye ALIHUSIKA moja kwa moja kama mlarushwa?
  • Waziri Mkuu aliyejiuzuru Edward Lowassa alipoamua kujiuzuru kwa Kashfa ya RICHMOND bungeni je yeye kama yeye ndiye MHUSIKA?
  • Aliyekuwa Rais wa FIFA Sepp Blater katika zile tuhuma zake kama 13 ukiondoa 2 tu ambazo zinamgusa yeye kama yeye je zile zingine 11 zilizobaki na ambazo ndizo ZILIMMALIZA alihusika nazo moja kwa moja?
NB: Hakuna heshima duniani kwa Kiongozi yoyote kama kuwa RESPONSIBLE na ACCOUNTABLE kwa jambo linalokutokea katika mazingira yako ya KIUONGOZI. Bado NASISITIZA Kuwa Rais wa TFF Ndugu Jamal Malinzi HANA MAHALA ATASEMA HAHUSIKI NA HILI SAKATA NA TUNAOJUA TUNASEMA AJIUZURU UPESI NA HARAKA KABLA WAZIRI Nape na TAKUKURU HAWAJAGUNDUA mengine zaidi.

Naomba post yangu hii IKUFIKIE WEWE NA WENZAKO WENGINE WOTE MNAOLITAZAMA HILI KWA UPEO WA NYASI ZA NYOKA NA JIFUNZENI KUTOKA NJE YA BOX. Sina CHUKI NA Jamal Malinzi kama yeye bali NINAPINGA UOZO WAKE NA ANAPOLIPELEKA SOKA LETU na katika hili SITONYAMAZA au KUBAKI NYUMA.

Aluta continua!
 
hivi huyu malinzi ndo yule waliokuwa viongozi wa FAT kipindi kile na WAMBURA au si yeye?maana ile FAT ilikua corrupted kinoma
 
Back
Top Bottom