Kama umejisikia hivi sasa ndiyo unaweza kuishi na mwanamke!! Huwa nawashauri vijana usioe mpaka upate wito, kuishi na mtoto wa mtu kazi sana kama huna wito!!
Kupata mke usikurupuke!
1. Shirikisha marafiki werevu wake kwa waume wenye ufahamu na mahusiano
2. Shirikisha wazee (wajomba, shangazi, bibi na babu na hata baba na mama) wakupe dondoo mbili tatu kuna kitu watakuambia kitakuongoza sana!
3. Mfahamu mwanamke utakayemchagua kuanzia historia ya kwao! Mfano; Ni familia yenye maradhi ya kurithi? Ni familia yenye asili ya ukorofi? Huyo mpenzi wako kalelewa na single maza, ilikuwaje? Familia walevi? Wanaoleka na kuoa au ndiyo wale ukiingia kwao unakuta dada zake sita waliolewa na kuachwa na kaka zake wameoa na kuacha na watoto wapo kwa babu yao!!
Ndoa nyingi hazidumu sababu huwa tuna bypass baadhi ya mambo muhimu kwa kujitia usasa! Mwisho wa siku unaoa binti ambaye kwao ni wakorofi balaa! Halafu unashangaa eti mkeo mkorofi!!
Au unaoa familia ina historia ya kuugua kichaa bro!! Tutakukuta kitaa unakimbizana na mkeo halafu unajiuliza imekuwaje tena na alikuwa mzima?? Nakutakia kila la kheri