Sasa ni zamu ya Los Angeles. Ni Alhamisi 21 Aprili, uzinduzi wa pili wa Royal Tour

Sasa ni zamu ya Los Angeles. Ni Alhamisi 21 Aprili, uzinduzi wa pili wa Royal Tour

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
377
Reaction score
435
SASA NI ZAMU YA LOS ANGELES. NI KESHO ALHAMISI, UZINDUZI WA PILI WA ROYAL TOUR.

Na Bwanku M Bwanku.

Baada ya Juzi Jumatatu Aprili 18, 2022 Rais Samia Suluhu Hassan kuusimamisha Ulimwengu wakati akiongoza Uzinduzi wa Filamu Maalum ya Watanzania ya Royal Tour Mahususi kwa ajili ya Kutangaza Utalii na Uwekezaji wa Tanzania Kimataifa pale New York, Marekani, sasa kesho Alhamisi Aprili 21, 2022 ni zamu ya Los Angeles. Ni historia nyingine inakwenda kuwekwa Los Angeles katika safari ya kuisimamisha Tanzania kwenye Anga za Kimataifa.

Baada ya Rais Samia kuwaongoza Watanzania kuzindua Filamu hii kwa mara ya kwanza toka kuandaliwa kwake pale New York, sasa macho na masikio yanahamia Los Angeles kwenye Uzinduzi wa Pili wa Filamu hii ya Royal Tour inavyokwenda kupaisha zaidi Sekta ya Utalii na Uwekezaji ili Taifa letu lipate Maendeleo makubwa zaidi. Ni kesho Alhamisi pale Los Angeles, Marekani.

#TunaImaninaRaisSamia
#TanzaniaRoyalTour
#KaziInaendelea

Bwanku M Bwanku.

255785897913_status_dbac70b9a8704fae99944e01d9cedb70.jpg
 
Nadhani hii ngoma haijawa kama tulivyokuwa tunategemea.

Tujipange upya.

Lazima kama nchi tujitathimini.

Kick ya ZAI wa Zanzibar imezidi hii ya Royal tour.

Huko kwenye social networks wanapost TBC na Ikulu na watanzania wachache, sioni media kubwa za nje zikijadili hii kiki ya Royal tour.

Angekuwa anafanya hili jambo mtu kama Uhuru Kenyata lingebamba dunia. Sisi bado sana. Wasaidizi wa mama wamelala yo, na kumwacha yeye na Peter wake wakijipigia ngoma na kucheza wawili. Nadhani wasaidizi hawataki kuingia kwenye kashfa nzito baada ya hii movie kukwama.
 
[emoji28][emoji28][emoji28]baada ya kuisimamisha ulimwengu[emoji28][emoji28][emoji28]

Tucheke Tena......[emoji28][emoji28][emoji28]

Tucheke Tena na Tena[emoji28][emoji28][emoji28]

Sawa Mr big chawa tumekusoma tukiwa Huku buza ndani ndani ambako cyo duniani....
 
Kama sijakosea nimeona mawaziri kadhaa sura zao ziko USA na Hangaya.

1.Rais na wasaidizi wake,

2.Mawaziri na wasaidizi wao.

3.Huku bungeni wanajadili kishindo cha kura 2020.Na wanalipwa seating allowance.

4.Huku mwenge unafyonza tozo.Kama hali ngumu kwanini tusiuzime kwa kipindi hiki ambacho Rais ametutangazia kuwa lazima vitu vitapanda.Kuwasha na kuuzima si iko mikononi mwetu.

Sasa karibia wiki moja,Hizi gharama jumla yake sizingefidia huu ukali wa maisha.
 
Piga kazi mama tumecheleweshwa mnooo kama taifa. Zaidi ya miaka 6 tulikwama mnoooo
 
Huyu bibi naona hataki kuachwa nyuma na kina diamond sasa hizi show anazopiga za kimataifa huu mwendo kauanzisha hawezi kuumaliza tegemeeni kusikia yupo china muda si mrefu hakosagi ka sababu
 
ULIMWENGU ULISIMAMA JUZI??

NI KWELI UNAANDIKA HAYA UKIWA NA AKILI ZAKO KAMILI?

Nchi hii tuna mengi sana ya vivutio vya Utalii.

Hata akili za watanzania pia ni kivutio cha utalii.
 
Yaani ukumbi unachukua watu 400 alafu uaime kasimamisha ulimwengu? Ni aibu kubwa mtu mzima kuwa CHAWA.
 
ULIMWENGU ULISIMAMA JUZI??

NI KWELI UNAANDIKA HAYA UKIWA NA AKILI ZAKO KAMILI?

Nchi hii tuna mengi sana ya vivutio vya Utalii.

Hata akili za watanzania pia ni kivutio cha utalii.
sasahivi madoctor hawatoi kizazi wanatoa mishipa ya aibu tu, Sipati picha huyu jamaa anafananaje
 
Yaani ukumbi unachukua watu 400 alafu uaime kasimamisha ulimwengu? Ni aibu kubwa mtu mzima kuwa CHAWA.
Hao watu 400 ni sawa na madarasa mawili ya wanafunzi wa darasa la kwanza kwa jinsi wanavyo shonana anakuja kbaka anakwambia ni ulimwengu huo
 
ULIMWENGU ULISIMAMA JUZI??

NI KWELI UNAANDIKA HAYA UKIWA NA AKILI ZAKO KAMILI?

Nchi hii tuna mengi sana ya vivutio vya Utalii.

Hata akili za watanzania pia ni kivutio cha utalii.
Duh !
 
Huyu kikongwe mvaa ushungi anazidi kuchanja mbuga.

Hatulii akakaa kwenye mji wake anapapatika kwenye nchi za watu kama sungura-tope.

Ati Royal Tour? Ujinga mtupu!
 
Back
Top Bottom