Sasa nimeelewa ni kwanini mbunge wa Liwale alisema Bwawa la umeme Nyerere liko Liwale

Mlango wa bwawa upo kati ya Mkoa wa Pwani na Morogoro, Lakini mawanda ya bwawa Kwa asilimia kubwa yatakuwa kwenye Jimbo la Liwale.

Kwani serikali ikisema hivyo watapungukiwa nini?
Na mtu mwingine atasema mto Nile uko Tanzania, mwingine atasema mto Nile uko Uganda na mwingine atasema mto Nile uko Burundi na Wamisri wanajua mto ule ni wao.
 
Khe!!

Kwanza ni jambo la kisayansi tu.

Kwani maji ukiyazuia huwa kinatokea Nini??

Yale maji toka pale langoni yatarudi nyuma mpaka kilomita 100. Sasa Kwa Nini lisizidi ukubwa Wa ziwa Rukwa?
kwanini wanayafungulia?,kwanini wasiyaaache yazidi ziwa Rukwa?
hivi unaamini wanasiasa na mbwembwe zao,eti mkuu.utaachwa na basi ukose pakulala hapa tz mkuu.shtuka!
 
Na mtu mwingine atasema mto Nile uko Tanzania, mwingine atasema mto Nile uko Uganda na mwingine atasema mto Nile uko Burundi na Wamisri wanajua mto ule ni wao.
Angalia Tena ulichoandika.

Mto Nile umepita pia Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Sudan na Sudani ya Kusini, Tanzania, Uganda, na Ethiopia.
 
kwanini wanayafungulia?,kwanini wasiyaaache yazidi ziwa Rukwa?
hivi unaamini wanasiasa na mbwembwe zao,eti mkuu.utaachwa na basi ukose pakulala hapa tz mkuu.shtuka!
Kwani mradi wenyewe ushakamika basi... Watu wanakbizana na Uchaguzi Wa mwakani... Waseme waliahidi wametimiza.
 
Angalia Tena ulichoandika.

Mto Nile umepita pia Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Sudan na Sudani ya Kusini, Tanzania, Uganda, na Ethiopia.
Umepitaje Burundi na Rwanda? kisa kuna mito kule inamwaga maji yake ziwa Victoria? weka utafiti wa kisayansi hapa
 
kwanini wanayafungulia?,kwanini wasiyaaache yazidi ziwa Rukwa?
hivi unaamini wanasiasa na mbwembwe zao,eti mkuu.utaachwa na basi ukose pakulala hapa tz mkuu.shtuka!
Mtera hata sasa maji yamefunguliwa, Bwawa limejaa.
Nafikiri hivyo vijiji vihamishwe pawe na fursa ya kupata Bwawa la Rufuji, itasaisia kuongeza shughuli za kiuchumi.
 
Back
Top Bottom