Sasa nina hakika CHADEMA haitakufa tena kwa matakwa ya binadamu

Sasa nina hakika CHADEMA haitakufa tena kwa matakwa ya binadamu

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,485
Nimefuatilia mlolongo wa njia ilizopitia CHADEMA nikagundua iliwekewa mitego mingi Sana ili ife lakini haikufa.

Iliondokewa na viongozi wake nguli walioiinua kwa mikono, jasho na damu zao lakini haikufa, wachache ni Slaa, Zitto, Kitila, Mwigamba, Arfi na msululu wa viongozi wake nguli CHADEMA haijafa.

Kuna watu ndani ya CCM walipanga mipango ya wazi na ya kificho ili CHADEMA ife wakijiapiza hadharani na mafichoni kuwa wataiua, lakini ama wao wamepoteza nafasi zao za kazi ama wao ndio wamekufa na kuiacha CHADEMA hai.

Kuna watu walitabiri hata mwaka kuwa ifikapo mwaka Fulani CHADEMA itakua historia. Naona watu hao wengine walipoteza nafasi zao za ubunge, uwaziri ama kwenye chama ama Serikalini lakini CHEDEMA ipo inadunda.

Kitu kilichonivutia Sana ni kampeni za 2020. Mgombea wa CHADEMA aliweka historia ya kutokuwa na bango hata moja, kutokutangazwa kwa mikutano yake mingi, kutokuwa na hela za kutosha za kampeni, kutokuwa na wasanii wakubwa na wengi, lakini mikutano yake ilikuwa ina hamasa ya Hali ya juu sana.

CHADEMA haijafa, kama mnabisha ruhusuni harakati za kisiasa kama zamani.

Narudia kusema waliotaka kuiua CHADEMA wamepoteza fedha za umma bure hasa kwenye operesheni manunuzi ya viongozi wake. Baadhi ya waliotaka CHADEMA ife hapo zamani leo hii hawapo.
 
Chadema wote wameamia ccm ya mama samia.

ccm mbele kwa mbele.
Na huo nao ndio udhaifu mwingine wa CCM, CCM Sasa hivi haina viongozi wa maana kabisa, inachukua kutoka CHADEMA, CHADEMA imekua chuo au mtambo wa kuzalisha viongozi, imekua Kama ilivyokua chuo Cha sayansi ya siasa kivukoni enzi za Nyerere.

CCM inabidi initafakari kabisa.

Imeishiwa watu mahili imebakiza watu aina ya kibajaji na msukuma n.k.

CHADEMA iko vizuri aisee.
 
Hilo halina ubishi Mkuu, zaidi sasa lina ushahidi.
Ile kauli ya CHADEMA huwa ina nguvu Sana ila watu shingo zao ngumu tu, kauli ya
"Tulianza na Mungu tutamaliza na Mungu"
Sasa aje mtu ajaribu kuiua CHADEMA uone Kama atabaki salama.
Nakuhakikishia kwamba kila atayejiapiza kuua Chadema atakufa yeye iwe kisiasa au kimwili .
 
Mgombea wa Chadema aliweka historia ya kutokua na bango hata moja,kutokutangazwa kwa mikutano yake mingi,kutokua na hela za kutosha za kampeni,kutokua na wasanii wakubwa na wengi...
Tahadhali sana mkuu.

CHADEMA inaweza kufa kuanzia sasa kama wasipokuwa waangalifu.

Hatari kubwa inaweza kuwepo kuanzia sasa na kuendelea.

Ni lazima wajipange vizuri sana kushindana bila ya misuguano. Hiyo huitwa "vita baridi."

Ufafanuzi wa hili nitaueleza siku nyingine.
 
Namkumbua Mzee Wasira sijui Yuko wapi,alitabiri Chadema kufa.
Mwacheni Mungu aitwe Mungu.
Sawa
Tahadhari sana mkuu.

CHADEMA inaweza kufa kuanzia sasa kama wasipokuwa waangalifu.

Hatari kubwa inaweza kuwepo kuanzia sasa na kuendelea.

Ni lazima wajipange vizuri sana kushindana bila ya misuguano. Hiyo huitwa "vita baridi."

Ufafanuzi wa hili nitaueleza siku nyingine.
Sawa Mkuu,nitashukuru Kama utanitag
 
Back
Top Bottom