Nimefuatilia mlolongo wa njia ilizopitia CHADEMA nikagundua iliwekewa mitego mingi Sana ili ife lakini haikufa.
Iliondokewa na viongozi wake nguli walioiinua kwa mikono, jasho na damu zao lakini haikufa, wachache ni Slaa, Zitto, Kitila, Mwigamba, Arfi na msululu wa viongozi wake nguli CHADEMA haijafa.
Kuna watu ndani ya CCM walipanga mipango ya wazi na ya kificho ili CHADEMA ife wakijiapiza hadharani na mafichoni kuwa wataiua, lakini ama wao wamepoteza nafasi zao za kazi ama wao ndio wamekufa na kuiacha CHADEMA hai.
Kuna watu walitabiri hata mwaka kuwa ifikapo mwaka Fulani CHADEMA itakua historia. Naona watu hao wengine walipoteza nafasi zao za ubunge, uwaziri ama kwenye chama ama Serikalini lakini CHEDEMA ipo inadunda.
Kitu kilichonivutia Sana ni kampeni za 2020. Mgombea wa CHADEMA aliweka historia ya kutokuwa na bango hata moja, kutokutangazwa kwa mikutano yake mingi, kutokuwa na hela za kutosha za kampeni, kutokuwa na wasanii wakubwa na wengi, lakini mikutano yake ilikuwa ina hamasa ya Hali ya juu sana.
CHADEMA haijafa, kama mnabisha ruhusuni harakati za kisiasa kama zamani.
Narudia kusema waliotaka kuiua CHADEMA wamepoteza fedha za umma bure hasa kwenye operesheni manunuzi ya viongozi wake. Baadhi ya waliotaka CHADEMA ife hapo zamani leo hii hawapo.