Sasa rasmi bei ya unga ni kubwa kuliko sufuria

Sasa rasmi bei ya unga ni kubwa kuliko sufuria

KILA kitu bei juu colgate herbal big toka 3500 hadi 6000,dawa ya minyoo zentel toka 4000 hadi 8000.
Nyama kilo 8500,pesa haina thamani na haipatani. Bora ya Magu haikupatikana lakini ilikuwa na thamani. Yule jamaa pale wizaarani anachojua ni kuongeza sifuri tu
Ni hopeless, zero hakuna anachojua Hana ubunifu, hii inaonyesha elimu yetu ni ya kukariri kazi kujisifia ana first class
 
Dah!...wenye dhamana watupunguzie huu ukali aise.
 
Leo nimenunua sufuria moja dogo kwa shilingi 2000 na bei ya unga mtaani kwangu kwa kilo ni sh 2200.
Kwa lugha nyepesi ni rahisi kula masufuria na mboga kuliko kula ugali na mboga.
Yapi maoni yenu wakuu.
Mama anaupiga mwingi
 
Hebu kwanza tuone hako kasufuria ka buku mbili
 
theory, theory, theory, theory.

hizi mambo zinataka magwiji waliobobea na wenye maarifa ya kutosha sio hawa vijana waliotoka shule na kuanza kujifunzia kazi kwenye maisha ya watu.

Tumewekeza sana kwenye siasa, ni ngumu mtu kuamini kazi fulani mmemshinda bali atatumia nguvu kubwa kuonyesha anakwenda vizuri kulinda umaarufu wake kwenye siasa huku akiangamiza maisha ya watu.

Kuna watu nyadhifa fulani zimewashinda ukubwa, yadhifa hizi tunazichulilia kirahisirahisi na kuzifanya kisiasa lakini zonahitaji magwiji waliofanya kazi huku na kule ndani na nje ya nchi kwenye mataasisi na makampuni makubwa ikiwemo kuwepo kwenye ngazi kubwa za maamuzi.

Hawa watoto tunaotaka kuwaamini, ni wapi tumefanya juhudi kuwakuza vyema kwenye utendaji? au tunawapa mavyeo makubwa kulinda maslahi yetu? na kuendeleza tawala za undugu bila kujali maslahi ya taifa.

Tuwe serious na maslahi ya Taifa na watu wake.
 
Mi juzi nilienda kutuma hela m-pesa tozo ikawa kubwa kuliko nauli ya kwenda napotaka kutuma ikabidi nipande bus kuipeleka hela morogoro na kurudi
hahahaaaa
 
Sasa kama si hivyo Pesa za sherehe za Bunge zitatoka wapi? Wajikoni watakula vya jikoni Haina namna tuendelee kuwatumikia hawa Green-Yellow heads ili waish vyema.
 
Back
Top Bottom