Mkuu nimependa sana hoja zako. Kwanza naomba kuweka maslahi yangu binafsi kwenye hii miradi, mimi ni muwekezaji na mnufaikaji wa mradi wa machimbo ya mchanga unaoendelea huko Misugusugu Kibaha. Kwakweli huyu Mzee Abdul na Mke wake ni wastaarabu na waungwana mno. Nimefika Kibaha licha ya kutuma pesa hata kabla ya kuonana nao.
Alichosema ni kweli kulikua na uchelewaji kutokana na mvua lakini alitoa habari na maendeleo kila mara kutujulisha tatizo liko wapi. Kama lugha za
FaizaFoxy hazijakufurahisha kwa namna moja ama nyingine, naomba umuwie radhi kama binadam lakini usiwaelekezee tuhuma hawa wazee.
Mzee Abdul ni kweli kazi mnayofanya ni nzuri sana. Ningependa kuungana na
Shark pamoja na
Titicomb kujua hali ya biashara (soko la mchanga) likoje? Kuna miradi mikubwa ya ujenzi inaendelea kipindi hichi? Nauliza hivyo kwa sababu lengo sio mimi tu kama muwekezaji kufaidika, ni vizuri na nyie mnaoendesha na kusimamia miradi mfaidike. Kama shughuli za ujenzi zinadorora inamaana kutakua na shida kidogo.
Vinginevyo niwatakie kila la kheri na baraka kwenye shughuli zenu.
N.B vilevile mimi ni miongoni mwa wanachama wa Vitendo Saccoss inayoratibiwa na Mzee Abdul.