Update...
Excavator project tayari tuna 34m Target ni 40m. Bado tunahitaji 6m tuanze kazi.
Fursa inaaga hiyo.
Wadau,
Kwanza kabisa ninamshukuru sana Mwenyeezi Mungu kwa yote.
Pili nina furaha kubwa sana kuwafahamisha kuwa mradi wetu wa excavator umeanza ku take kukamilisha kuchangishana mtaji. Tumeweza kufikia lengo letu la kuzipata Shillingi million 40 kabla ya deadline iliyokuwa tarehe 30 Septemba 2017.
Jana saa tano na dakika hamsini na moja za usiku tuliweza kufanikisha kufikia lengo letu kupitia mwana VTS, ndugu yetu, Dada yetu, binti yetu Bi Happyness.
Hakika Happyness ameliishi jina lake kwa kuleta furaha kwa wengi tuliokuwa tunaufatilia mradi huu kwa karibu. Asante sana kwa hilo.
Natoa Shukrani zangu za dhati kwa wana VTS wote waliofanikisha jambo hili. Asanteni sana.
Kila kazi haikosi changamoto zake na katika kukamilisha zoezi letu hili tukakumbwa na changamoto iliotufanya tuongeze bajeti ya Shillingi million tano kwenye mradi. Tikaiita hio contingency. Contingency hio haituzuwii kuanza kazi zetu lakini ni vyema tukaipata.
Kwa hio wale wote watakaovutiwa na aina hii mpya ya mageuzi ya kupata mtaji wa uwekezaji kihalali katika uwekezaji halali bado kuna fursa.
Contingency yetu baina ya jana usiku na leo alfajiri imeshuka toka 5m mpaka kufikia 4.55m.
Mnakaribishwa wote kujiunga nasi kwenye Vitendo SACCOS katika kuleta mageuzi ya kiuchumi binafsi Tanzania.
Baadae tutajaribu kuwaletea jinsi zoezi lilivyokwenda jana kabla ya kufanikisha.
Asanteni sana kwa kutufatilia.
VITENDO SACCOS tunawakaribisha.
Abdul Ghafur
Mwenyekiti
Vitendo SACCOS.
0625249605.