Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Kipute cha robo fainali kati ya Simba na Orlando kimekwisha na Orlando amesonga mbele kwa kutupa faraja wana Yanga kuzima kelele, tambo na kejerli za Simba.
Tuongee ukweli tu ni kwamba mashabiki wa Simba hamna cha kuidai timu yenu kwa kutolewa robo fainali ni hatua nzuri timu imefika, nawapongeza sana kwa dhati kabisa, huwa tunaombea tu Simba ifungwe kwa sababu ya kelele na tambo tu za mashabiki wao.
Turudi kwa Yanga sasa, itakuwa ni fedhea kubwa kwa Yanga kuwa mabingwa wa nchi na kutolewa round ya kwanza tu hapo ndipo ulipo msingi wa hoja yangu.
Kama vile tunavyowakejeri Simba waje kupata tuition Yanga ya upigaji penati na sisi yanga tunapaswa kupata tuition tena nzito ya jinsi ya kuutumia uwanja wa nyumbani, siri yote ya mafanikio ya Simba iko hapo.
Haya mashindano ya Africa yalivyo kiuhalisia ni kwamba kila mtu ashinde mechi zake na hapa ndipo tuition ya Simba inapohitajika yale mazingaombwe yao pale kwa Mkapa Yanga hatuwezi kuyatumia?
Na kwakuwa mpira wa Africa umeonesha wazi kila mtu anashinda kwake basi tuwe na forward za ukweli kina Mayele watatu ili mechi za nyumbani unamaliza shughuri nyumbani kwa goli tano away unakwenda kuwachosha tu wapinzani wako.
Hongereni sana Simba kwa kuweza kuutumia vyema uwanja wa Mkapa kwa mbinu zozote zile, ziwe chafu au halali haijarishi cha msingi ni ushindi.