Hahahaaa! Hautaliona hilo. Nyerere alisema kuwa hawezi kutoa nchi kwa mbwa - 1995. Bila Nyerere kujua, nchi tayari imeingia kwenye mikono ya mbwa.
Ni mbwa pekee wanaoweza kuteka wagombea pinzani ili wao wapite bila kupingwa. Ni mbwa pekee wanaoweza sema ruhusa TLP na UDP kusapoti CCM lakini haramu CHADEMA kusapoti ACT kwenye uchaguzi.
Ni mbwa pekee wanaoweza kufoji utaratibu wa kuteua wabunge wa viti maalum wakihusisha Bunge, mahakama na serikali halafu ikawa kama vile hakuna baya lililotendeka.
Ni mbwa pekee wanaoweza kuwawekea vikwazo wagombea wa vyama ambavyo vipo kikatiba ili wasifanye uchaguzi ambao upo kikatiba kwa kuwanyima usafiri ama kuzua usafiri wao wenyewe ili wasifanye kampeni.
Ni mbwa pekee wanaoweza kuchapisha makaratasi ya kura, weka tiki kwa CCM wakiwa majumbani na mahotelini, halafu kuyaingiza kwenye vituo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi. Halafu jioni wakaacha kuhesabu kura kwenye hayo makaratasi. Badala yake wakasoma matokeo yaliyotoka kwa Mahera!
Ni mbwa pekee wanaweza kuvunja katiba yetu watakavyo na kusiwe na consequences.