Sasatel is a let down company. Nilinunua modem yao Oktoba mwaka 2011, kwa minajili ya kutumia maskani jijini Dar. Nilipoijaribu katikati ya jiji spidi ya mtandao wao ilikuwa nzuri sana, ila nilipopeleka nyumbani kwangu nje ma ya mji (ni kama km 20) kukawa hakuna network yao. Shida hiyo ipo hadi leo, mpaka ninaandika ujumbe huu nimehifadhi modem maskani bila kujua cha kuifanyia, kwa sababu lengo langu ilikuwa ni kujinafasi na mtandao maskani. Mbaya zaidi modem yao haitumii line ya simu, kwamba ningechakachua nitumie line nyingine.