Sasatel Iko Katika Hati Hati Ya Kufungwa...

Sasatel Iko Katika Hati Hati Ya Kufungwa...

hawana effect kubwa hata wakidisapper he he he.....but nilikuwa kila siku nasikia watajita watajitanua na hamna kilichotokea but mara ya mwisho kuangalia kwenye list ya TCRA nakumbuka kama vile wana licence ya national
 
Mkuu kwani kuna mtu kawazuia kujitanua?
Mkuu sio kwamba kuna mtu anawazuia ila kama kampuni haijatengeneza faida yoyote kwa investor itajitanua vipi which means kampuni kama kampuni inashindwa kujiendesha yenyewe, hapa Dar es Salaam penyewe network yao haipatikani sehemu zote
 
Kampuni ambayo mmoja ya main shareholders ni Mchungaji Lwakatare lazima ife! yule mama mshirikina tu
 
Jamaa walijitoa kwenye soko la simu za mkononi kwa kwenda na technolojia ya CDMA hakuna anayetaka kununua simu ambayo itafanya kazi kwenye network moja tu na option za simu ni chache sana kwa CDMA kuna thread humu tulibishana sana kampuni ilipoanzishwa. Nadhani profits nyingi zipo kwenye voice calls Bongo sio kwenye data.

Anyway itakuwa loss kubwa maana nasikia walikuwa wanalipa vizuri.
 
Mobile industry is niot that saturated .................ni kweli hii kampuni ilianzishwa ili ife............deal fulan hivi
 
Sasatel is a let down company. Nilinunua modem yao Oktoba mwaka 2011, kwa minajili ya kutumia maskani jijini Dar. Nilipoijaribu katikati ya jiji spidi ya mtandao wao ilikuwa nzuri sana, ila nilipopeleka nyumbani kwangu nje ma ya mji (ni kama km 20) kukawa hakuna network yao. Shida hiyo ipo hadi leo, mpaka ninaandika ujumbe huu nimehifadhi modem maskani bila kujua cha kuifanyia, kwa sababu lengo langu ilikuwa ni kujinafasi na mtandao maskani. Mbaya zaidi modem yao haitumii line ya simu, kwamba ningechakachua nitumie line nyingine.
 
Breaking News:Sasatel yafa Rasmi.
Noma sana kuna mshikaji flani namjua aliacha kazi kwa mbwembwe akaenda Sasatel nadhani na yeye atakuwa anapumulia mashine,vijana wengi wanapenda sana maendeleo ya harakaharaka yakija makampuni mapya anakimbilia tu bila kutafakari anaacha sehemu aliyekuwepo miaka miwili anaenda kwenye kampuni ambayo haijui ina background gani anatema Big G kwa karanga za kuonjeshwa,Kuna kampuni ilikuja miaka ya 2008 inaitwa Hits Tanzania kampuni ya simu ilikuwa na prefix 0741xxxxxx ilinyang'anya wafanyakazi wengi kutoka kampuni za simu watu walikimbilia kisa walikuwa wanaenda kulipwa $3000 wakaacha kazi za huku walipokuwa wanalipwa 1.3m baada ya miezi mi3 wakakumbana na mtikisiko wa uchumi kampuni ikafa wakaanza kuemea mashine ahmad wengine wakapata zari wakaenda Equatorial Guine ndio ikawa manusura otherwise ilikuwa aibu maana walikuwa wamekaa miezi mi3 bila mshaara ikabidi wengine wakaanza kuuza magari yao haya makampuni mapya yanayokuja ni majanga sio mazuri kukimbilia...RIP sasatel
 
Back
Top Bottom