Taarifa ya awali ya Ndg, Edgar Edson Mwakabela, @Sativa255
Baada ya @Sativa255 akiwa Dar es Salaam kutekwa, kuteswa na kutupwa pori la Katavi, waliomuokota walimfikisha Hospitali ya Halmashauri ya Mpimbwe (Tupindo),
Hospitali ya Halmashauri ya Mpimbwe (Tupindo), ipo katika kata ya Mbede, Wilaya ya Mlele, mkoa wa Katavi. SATIVA amefikishwa hapo akiwa na maumivu makali.
Baada ya kufikishwa Hospitali ya Halmashauri ya Mpimbwe (Tupindo), huduma zilikuwa hafifu kutokana na kukosa mtu ambaye anamfahamu. Hakuwa na ndugu Mlele.
Kwa msaada wa haraka wa madaktari eneo hilo na tukampata Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya Mlele ambaye alimjuza Mkurugenzi Halmshauri ya Mpimbwe
Mganga Mkuu wa Halmashauri Mpimbwe alimjuza Mkurugenzi kuna mtu ameokotwa katika moja ya mapori la Katavi na anahitaji msaada wa kitabibu kwa haraka.
SATIVA akaendelea kupatiwa matibabu hospitali ya halmshauri ya Wilaya ya Mpimbwe (Tupindo). Wakati huo tukiomba apatiwe rufaa kwenda DAR au MBEYA
Mganga Mkuu wa Halmashauri Mpimbwe akasema kwa utaratibu, hawana mamlaka ya kutoa rufaa kwenda nje ya mkoa. Wenye mamlaka ni hospitali ya Rufaa Mkoa.
Wakati hayo yakiendelea, tukawatafuta mawakala wa kukata tiketi, wakatueleza kwamba, ndege ya Air Tanzania imeondoka leo Katavi, route nyingine ni hadi Jumamosi.
Hivyo basi, SATIVA anaendelea na matibabu hospitali ya Mpimbwe, ukifanyika utaratibu apelekwe Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi kuendelea na matibabu ya juu.
Tumezungumza na Mganga Mkuu, apelekwe Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi (huko kuna watu watampokea), na kuanzia hapo rufaa kwenda nje ya Katavi itawezekana.
Kulikuwa na concerns tofauti kutoka kwa ndugu, jamaa na rafiki zake Edgar, hususani mama yake mzazi, zote zikiwa kwa manufaa ya SATIVA. #JusticeForSativa
Martin Maranja Masese, MMM.