Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na ‘watu wasiojulikana’

Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na ‘watu wasiojulikana’

Unadhani ni rahisi, mwakyembe walimng'oa meno kwa plaiz hapa, alipofikishwa afrika kusini kupata tiba, akasema akirudi atasema yote atawataja woote, kiko wapi alirudi na akapoa, sijui yuko wapi siku hizi
Mwakyembe waziri mstaafu au?
 
Vikitokea vitendo vya kishenzi kama hivi lazima tumkumbuke mwasisi wa huu ushenzi, ndiyo legasi aliyoacha
Kukaa kimya wakati wewe ni msaidizi mkuu wa Rais ni kuunga mkono mipango, matendo na maamuzi yake.

Ndege wafananao huruka pamoja kwa hiyo tusishangae kuona mambo mengi tu yakijirudia...kazi iendelee!
 
Unao ushahidi na hayo uliyoandika?

Sitetei uovu kwenye jamii, lakini, tunao ushahidi kuwa watekaji ni wa chama fulani?

Watu wengine wanachukua wake za watu, halafu, yanawakuta ya kuwakuta, tunakimbilia kusema wametekwa kwa sababu za kuikosoa Serikali. Huu ni mfano tu, sina ushahidi kama jamaa alifanya hivyo.
Wewe hujui kitu tulia mkuu
 
Kuna sehemu aligusa walimpa warning ila akaipost Ile dm aliopewa warning kama akiikejeli nahisi ndo ilimletea shida ila watu walishutumu awamu ya sita kwa mambo haya kunyakuana mbona Bado yapo
 
Taarifa ya awali ya Ndg, Edgar Edson Mwakabela, @Sativa255


Baada ya @Sativa255 akiwa Dar es Salaam kutekwa, kuteswa na kutupwa pori la Katavi, waliomuokota walimfikisha Hospitali ya Halmashauri ya Mpimbwe (Tupindo),


Hospitali ya Halmashauri ya Mpimbwe (Tupindo), ipo katika kata ya Mbede, Wilaya ya Mlele, mkoa wa Katavi. SATIVA amefikishwa hapo akiwa na maumivu makali.


Baada ya kufikishwa Hospitali ya Halmashauri ya Mpimbwe (Tupindo), huduma zilikuwa hafifu kutokana na kukosa mtu ambaye anamfahamu. Hakuwa na ndugu Mlele.


Kwa msaada wa haraka wa madaktari eneo hilo na tukampata Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya Mlele ambaye alimjuza Mkurugenzi Halmshauri ya Mpimbwe


Mganga Mkuu wa Halmashauri Mpimbwe alimjuza Mkurugenzi kuna mtu ameokotwa katika moja ya mapori la Katavi na anahitaji msaada wa kitabibu kwa haraka.


SATIVA akaendelea kupatiwa matibabu hospitali ya halmshauri ya Wilaya ya Mpimbwe (Tupindo). Wakati huo tukiomba apatiwe rufaa kwenda DAR au MBEYA


Mganga Mkuu wa Halmashauri Mpimbwe akasema kwa utaratibu, hawana mamlaka ya kutoa rufaa kwenda nje ya mkoa. Wenye mamlaka ni hospitali ya Rufaa Mkoa.


Wakati hayo yakiendelea, tukawatafuta mawakala wa kukata tiketi, wakatueleza kwamba, ndege ya Air Tanzania imeondoka leo Katavi, route nyingine ni hadi Jumamosi.


Hivyo basi, SATIVA anaendelea na matibabu hospitali ya Mpimbwe, ukifanyika utaratibu apelekwe Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi kuendelea na matibabu ya juu.


Tumezungumza na Mganga Mkuu, apelekwe Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi (huko kuna watu watampokea), na kuanzia hapo rufaa kwenda nje ya Katavi itawezekana.


Kulikuwa na concerns tofauti kutoka kwa ndugu, jamaa na rafiki zake Edgar, hususani mama yake mzazi, zote zikiwa kwa manufaa ya SATIVA. #JusticeForSativa


Martin Maranja Masese, MMM.
 
Back
Top Bottom