Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na ‘watu wasiojulikana’

Wako sahihi mzee wangu, hosp zetu hawakutibu bila pf3. Hata ukimleta mgonjwa ukasema naenda kuleta pf3 ukirudi utamkuta mgonjwa wako yupo vile vile wakiona huruma sana labla wampe paracetamol

Inasikitisha sana, kwanini hospitali isiwe na dawati la Polisi au mawasiliano na Polisi huku mtu aliyejeruhiwa akiendelea na matibabu?

Shida ni nini Idara,ya Polisi na Hospital kuwa na ushirikiano ili kuokoa maisha ya aliyejeruhiwa, kwa Polisi kufika haraka hospitali wakiwa na PF3, pingu, silaha na vyombo vya kurekodi picha, sauti ili kuwa na ushahidi badala ya kupoteza muda majeruhi kupitishwa kituo cha Polisi ambapo askari hawana ujuzi wa kuokoa maisha ya raia aliye majeruhi.
 
We jamaa ulikuwaga na akili. Siku hizi umekua kubwa la machawa
Kwa kweli sikutegemea kauli kama hiyo kutoka kwa Dr Matola PhD tuliyetoka naye mbali hata kama naye amekuja kufuzu katika Chuo Cha Machawa
Hawa ndio walimpiga Mdude mpaka sura ikapinda kama mkate wa kumimina.
Duh, nimeinua mkono kwa baadhi ya Watanganyika kwani kwa kweli taifa letu halikuwa hivi! CCM imetufikisha kuzimu...@Accumen Mo:, yaani aibu naona mimi.
 
Huyu ni Mkosoaji wa baadhi ya Sera za Wizara na SERIKALI ! Amekuwa Mwiba kwenye Wizara ya Afya na Mpaka akatumiwa onyo Mara kadhaa !

Amekuwa akimkosoa Ummya mwalimu kwa sera zake za kuondoa Toto Afya
NHIF na Bima kushindwa kusimamiwa!
Pia amekuwa akiunga mkono wote wanaoonesha udhaifu wa vituo vya afya na hospital


Britanicca
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…