Wako sahihi mzee wangu, hosp zetu hawakutibu bila pf3. Hata ukimleta mgonjwa ukasema naenda kuleta pf3 ukirudi utamkuta mgonjwa wako yupo vile vile wakiona huruma sana labla wampe paracetamol
Inasikitisha sana, kwanini hospitali isiwe na dawati la Polisi au mawasiliano na Polisi huku mtu aliyejeruhiwa akiendelea na matibabu?
Shida ni nini Idara,ya Polisi na Hospital kuwa na ushirikiano ili kuokoa maisha ya aliyejeruhiwa, kwa Polisi kufika haraka hospitali wakiwa na PF3, pingu, silaha na vyombo vya kurekodi picha, sauti ili kuwa na ushahidi badala ya kupoteza muda majeruhi kupitishwa kituo cha Polisi ambapo askari hawana ujuzi wa kuokoa maisha ya raia aliye majeruhi.