kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,677
Ujenzi huo utaanza miezi minne ya mwanzoni mwa mwaka huu wa 2021. Usafiri wote wa umma utakuwa chini. Mwanamfalme Salman ametangaza lengo lake la kuanzisha mradi wa ujenzi wa mji usiokuwa na barabara na usioruhusu magari na kutoa maelezo ya taarifa hiyo siku ya Jumapili.
Kwa mujibu wa mwana mfalme Mohammed bin Salman, alisema ifikapo 2050, watu bilioni moja watakuwa hawana makazi kutokana na hewa chafu ya kaboni. Ndio maana Saudi Arabia imepanga kujenga mji mpya ambao hautakuwa na magari.
Takwimu zinaonesha kuwa ni watu milioni moja tu ndio wataishi katika mji huo. Asilimia tisini ya idadi ya watu duniani inapata changamoto ya hewa chafu. "Kwanini dunia iruhusu watu milioni 7 kufariki kila mwaka kwasababu ya matokeo ya hewa chafu?"
"Watu wengine milioni 7 wafariki kutokana na ajali za barabarani."
Mji huu utajengwa ukiwa unazingatia hali rafiki kwa mazingira. Mji huo utakuwa na shule ,hospitali, bustani, na usafiri wa mwendo kasi wa chini. Ujenzi wa mji huo mpya kwa Saudi Arabia ni sehemu ya kuacha utegemezi wa rasilimali moja ya mafuta pekee.
BBC SWAHILI