Jasusi,
Haya tazama basi kwa utumwa wetu wa mawazo huyo mkulima hadi kaja mzungu ndipo tunaona matunda ya fikra zozote zile.. Hapa Mwanakijiji, wewe na wanabodi wote kila siku mnazungumzia mambo chungu nzima hakuna mtu anayepata somo isipokuwa kama angezungmza mzungu ungeona mabadiliko..
Sababu kubwa ni kwamba yule mzungu anakuwa na muda wa kufatilia, vijisenti vyake alivyoviweka benki na idea anayokuja nayo anaiweka ktk majaribio na matunda ndio kaa hayo lakini bwana shamba wa Kitanzania kwanza yeye mwenyewe maisha yake anababatiza, saa moja kazini, saa inayofuata anatakiwa kufikiria familia yake watakula nini..Mtaji unapokuwa hautoki na nchi ambayo raia wake ni maskini na hawana credit yoyote ktk financial institution ni vigumu sana kuujenga mfumo wa Ubepari ktk jamii hiyo.
Ni lazima tuanzie mahala kama tunaukubali Ubepari lakini kama tutaendelea na kufikiria kwamba Ubepari ni Free market economy kama somo hatutafika mahala popote, tutabakia wafungwa ktk umaskini na kila siku tutaendelea kulaumiana..Huwezi kupanga safari ya abiria kwa baiskeli kwa uwezo na mwendo wa gari..
Maneno yako kweli kabisa lakini anhcosema mimi makosa sio ya serikali tu isipokuwa ni sote pamoja..Wanavyofikiria wao haina tofauti na Watanzania wengi..Mfano mzuri ni huu hapa swala limekuwa saudia badala ya Kumwezesha Mtanzania.Mkandara,
Kwa bahati mbaya sikuwepo enzi mnazungumzia suala la Kaburu na ardhi Afrika. Nakumbuka Mwinyi alipokwenda Afrika kusini kuaga mwaka 1985 aliwakaribisha Makaburu waje Tanzania. Tatizo la viongozi wetu ni kufikiria kuwa sisi hatuwezi. Wageni tu ndio wanaoweza. Nimesoma ripoti moja ya mkulima huko Mbeya ambaye sasa hivi anatengeneza shillingi millioni 100 kwa mwaka kwa kulima mchele, vitunguu, nyanya., nk na anasema kuna wakulima kama 200 katika kundi lake wenye kipato hicho. Na hawa waliwezeshwa kwa kupewa simple education na mhisani mmoja. Kwa hiyo uwezo wa kuwakwamua wakulima wetu upo. Sasa tungetumia mfano huo katika majimbo mengine hali ya maisha yetu ingebadilika sana na vijana hawatakuwa na sababu tena ya kukimbilia mijini kwa sababu kuna hela ya kutosha huko mashambani.
Tuwe waangalifu na ardhi yetu isije ikawa yale yale yaliyotokea katika ardhi ya madini.
Huo ndio mtizamo wangu.