Saudi investors eye Tanzanian farmland

Saudi investors eye Tanzanian farmland

Jasusi,
Mkandara,
Kwa bahati mbaya sikuwepo enzi mnazungumzia suala la Kaburu na ardhi Afrika. Nakumbuka Mwinyi alipokwenda Afrika kusini kuaga mwaka 1985 aliwakaribisha Makaburu waje Tanzania. Tatizo la viongozi wetu ni kufikiria kuwa sisi hatuwezi. Wageni tu ndio wanaoweza. Nimesoma ripoti moja ya mkulima huko Mbeya ambaye sasa hivi anatengeneza shillingi millioni 100 kwa mwaka kwa kulima mchele, vitunguu, nyanya., nk na anasema kuna wakulima kama 200 katika kundi lake wenye kipato hicho. Na hawa waliwezeshwa kwa kupewa simple education na mhisani mmoja. Kwa hiyo uwezo wa kuwakwamua wakulima wetu upo. Sasa tungetumia mfano huo katika majimbo mengine hali ya maisha yetu ingebadilika sana na vijana hawatakuwa na sababu tena ya kukimbilia mijini kwa sababu kuna hela ya kutosha huko mashambani.
Tuwe waangalifu na ardhi yetu isije ikawa yale yale yaliyotokea katika ardhi ya madini.
Huo ndio mtizamo wangu.
Maneno yako kweli kabisa lakini anhcosema mimi makosa sio ya serikali tu isipokuwa ni sote pamoja..Wanavyofikiria wao haina tofauti na Watanzania wengi..Mfano mzuri ni huu hapa swala limekuwa saudia badala ya Kumwezesha Mtanzania.
Haya tazama basi kwa utumwa wetu wa mawazo huyo mkulima hadi kaja mzungu ndipo tunaona matunda ya fikra zozote zile.. Hapa Mwanakijiji, wewe na wanabodi wote kila siku mnazungumzia mambo chungu nzima hakuna mtu anayepata somo isipokuwa kama angezungmza mzungu ungeona mabadiliko..
Sababu kubwa ni kwamba yule mzungu anakuwa na muda wa kufatilia, vijisenti vyake alivyoviweka benki na idea anayokuja nayo anaiweka ktk majaribio na matunda ndio kaa hayo lakini bwana shamba wa Kitanzania kwanza yeye mwenyewe maisha yake anababatiza, saa moja kazini, saa inayofuata anatakiwa kufikiria familia yake watakula nini..Mtaji unapokuwa hautoki na nchi ambayo raia wake ni maskini na hawana credit yoyote ktk financial institution ni vigumu sana kuujenga mfumo wa Ubepari ktk jamii hiyo.
Ni lazima tuanzie mahala kama tunaukubali Ubepari lakini kama tutaendelea na kufikiria kwamba Ubepari ni Free market economy kama somo hatutafika mahala popote, tutabakia wafungwa ktk umaskini na kila siku tutaendelea kulaumiana..Huwezi kupanga safari ya abiria kwa baiskeli kwa uwezo na mwendo wa gari..
 
Zakumi,
Mkuu nipo nawe kabisa ktk hili, majuzi tu nimeshangaa kusikia familia ya Myahudi mmoja tajiri sana hapa Canada (inasemekana wamejenga almost half ya mji wa Toronto -downtown) ndio wajenzi wakubwa wa mji wa Dubai..Sasa nambie Myahudi kuwa mjenzi (contactor) mkubwa wa Dubai.. kweli hii inaingia akilini mwa Mdanganyika!
 
Jamani tuangalieni Economic aspects za hili swala na sio kujaza laundry ya lawama.
Tanzania ya leo in heka na heka ambazo ni undeveloped, na there is no signs kuonyesha kwamba hizo heka zinaweza kulimwa leo wala kesho. Population growth ya Tanzania ni around 2% hapo, than means kwamba bado tuna ardhi ya kujitosheleza.

Ukweli ni kwamba ni investors wachache sana ambao wako willing kuweza kwenye kilimo ( sector ambayo ina tumikisha more than 70% ya watanzania). Sasa kama hawa Wasaudi wameamua kuwekeza i guess hii ni nice move IF and ONLY IF swala hili litafanywa katika UWAZI( TRANSPARENCY) na KUWASHIRIKISHA WAKAZI WA MAENEO AMBAYO YATATUMIKA.

kusema ya kwamba watuachie ardhi yetu tulime wenyewe mchele is just uongo. Tanzania haina enough tools ambazo zitatuwezesha kuendesha kilimo cha kisasa. Tunachotakiwa ni kujifunza kutokana na makosa, kama sector hii ya kilimo itakuwa na kuongeza changio kwenye ukuaji wa uchumi (GDP) then Tanzania inaweza kutransform kutoka kwenye agro based economy kwenda kwenye uchumi ulio changanyika. I guess this is a nice move kama tuuu tutaifainya kwa maendeleo ya Taifa.

I support JANUARY comment kwamba kama tutaendesha mpango ambao Watanzania nao watafaidika na wawekezaji nao watafaidika then i believe tutaweza kufikia lengo.

Other than that let us wait and see.

Tatizo sio mpango wa uwekezaji. Binafsi naungana nao lakini soko kuu liwe Tanzania and only surplus ndio iende huko so ili wapate mazao ya kutosha nchini kwao wanatakiwa kuongeza uzalishaji hapo kutakuwa na mutual benefit. Pili kulease for 99 years sio sahihi sana mkataba wowote huwa unakifungu cha renewal so we can go for shorter period say 30 years kwa kuwa miaka ya mwazo itahitaji heavy capital investment from there tukawana utaratibu wa kurenew every after 5 years hivi.
 
Mkandara,
Kwa bahati mbaya sikuwepo enzi mnazungumzia suala la Kaburu na ardhi Afrika. Nakumbuka Mwinyi alipokwenda Afrika kusini kuaga mwaka 1985 aliwakaribisha Makaburu waje Tanzania. Tatizo la viongozi wetu ni kufikiria kuwa sisi hatuwezi. Wageni tu ndio wanaoweza. Nimesoma ripoti moja ya mkulima huko Mbeya ambaye sasa hivi anatengeneza shillingi millioni 100 kwa mwaka kwa kulima mchele, vitunguu, nyanya., nk na anasema kuna wakulima kama 200 katika kundi lake wenye kipato hicho. Na hawa waliwezeshwa kwa kupewa simple education na mhisani mmoja. Kwa hiyo uwezo wa kuwakwamua wakulima wetu upo. Sasa tungetumia mfano huo katika majimbo mengine hali ya maisha yetu ingebadilika sana na vijana hawatakuwa na sababu tena ya kukimbilia mijini kwa sababu kuna hela ya kutosha huko mashambani.
Tuwe waangalifu na ardhi yetu isije ikawa yale yale yaliyotokea katika ardhi ya madini.
Huo ndio mtizamo wangu.

Jasusi:

Masahihisho 1985 Mwinyi alikuwa bado makamu wa rais.
Labda hiyo ilikuwa 1995. Lakini nakumbuka 1988 Mwinyi alifanya ziara ya kwanza Uingereza na aliomba apewe mameneja waliostaafu waje kufanya kazi Tanzania kwa sababu aliona mameneja wengi wana-boronga. alizua mgogoro mkubwa kuwa anataka kurudisha ukoloni na aamini wataalamu wa Tanzania. Ata mimi mwenyewe niliona anachemsha. Lakini baada ya kufanya kazi kwenye projects mbalimbali hapa US, nimeona kuwa kinachotukwamisha katika investments ni technocrats na capital. Na kama kuna nafasi ya watu wa nchi zingine kuleta capital na investments wapeni nafasi hizo.
 
Zakumi,
kinachotukwamisha katika investments ni technocrats na capital. Na kama kuna nafasi ya watu wa nchi zingine kuleta capital na investments wapeni nafasi hizo.
Mkuu hili ndilo tatizo kubwa tena nashukuru sana umelisema..Hili ni somo zito sana na itachukua muda mrefu sana sisi kuweza kukubali..
Wala sii kazi ngumu sana au elimu kubwa inatakiwa isipokuwa ni uzoefu na vianzo kuwepo..Tatizo letu tunafikiria kuwa kama umeweza kuendesha baiskeli itakuwaje vigumu kuendesha gari la matairi manne!..tena tulivyokuwa wapumbavu tunataka kuendesha gari la abiria...haiendi hivyo..
 
Jasusi,
Mkuu wewe ni Mtanzania una jumba hapo US, sijui umekodishiwa kwa miaka mingapi au umeuziwa kabisaaa!... hivi kweli bongo ingewezekana kwa mtazamo wa JF!
What the heck!

Swala la kumiliki nyumba halina tabu mbona mataifa libao yanamiliki nyumba na mahotel hapo bongo kama kwao tu. Issue ya ardhi ni tete tuijadili vizuri ndio source ya mapigano yasiyoisha Israel tusiifanyie masihara
 
Zakumi,
Mkuu nipo nawe kabisa ktk hili, majuzi tu nimeshangaa kusikia familia ya Myahudi mmoja tajiri sana hapa Canada (inasemekana wamejenga almost half ya mji wa Toronto -downtown) ndio wajenzi wakubwa wa mji wa Dubai..Sasa nambie Myahudi kuwa mjenzi (contactor) mkubwa wa Dubai.. kweli hii inaingia akilini mwa Mdanganyika!

Mkandara:

Mimi na wewe tutabishana masuala ya Ujamaa na ubepari kama sehemu ya kuelimisha na kufahamishana. Hili suala la hapa ni practical matter.

Ukweli wa mambo ni za mafuta zinatengenezHivyo wanavyofanya sasa ni kufanya diversification ya mapato yao hili wasitegemee mafuta tu.

Mtanzania anashabikia soccer anaona raha mwarabu akiweka a pesa nzuri na wao wanajua kuwa siku moja mafuta hayatakuwa na wateja. -investment yake kwenye club ya Liverpool, Arsenal au Manchester City.

Katika mambo ya investment ni lazima tuwe wakweli. Pesa haina dini au ukabila.
 
1. Assume wewe ni mwakilishi wa Saudi Arabia kwenye mazungumzo, ungekubaliana na point ya 1?

2. Wanachotaka hawa jamaa ni kulima mpunga na ngano. Hawajasema kwamba wana tatizo la mananasi na machungwa. Ni kweli tungependa wawekeze kwenye usindikaji wa chakula, but it's not in their interest to do so. How do you negotiate that?

3. Kitu kingine cha kufahamu ni kuwa hawa jamaa hawalazimishi and we are not a monopoly when it comes to land supply. So, tukiona hakuna maslahi, tunaweza kukataa. Other countries will grab the opportunity and play the cards appropriately.

1. I am assuming to be mwakilishi wa Tanzania, ninajua thamani ya ardhi yangu na kwamba matumizi yake, priority iwe kwa manufaa ya nchi yetu.

2. Super markets za Saudi, Dubai na nchi nyinginge Uarabuni wanauza processed products including machungwa na nanasi. Nimeona mpaka packaged dried pineapples toka Vietnam. Mchele mwingi wa Saudi unatoka South East Asia, kutokana na demography, geo-politics na socio-economic changes, SEA is no longer a reliable source of food supply to Saudi & rest of middle East. Of course Saudi have the right to invest wherever they want, the fact they are interested in our land speaks for itself, therefore we should equally benefit.

3. Serikali yetu inaweza kutumia fursa hii, ku-facilitate Saudi iwe soko kubwa la mazao toka Tanzania. We can sell them beef, onions, rice, fruits, sunflower oil etc. More important having processing and preservation facilities on the ground will give us the edge. Hili la kuuza nafaka Saudi watanzania tunaweza. Fifteen years ago, nani alihisi Tanzania tungeweza ku-export mauwa (roses) kwenda Europe. Hapo Arusha na Moshi kuna wazalendo wengi [waziri wa kwanza wa fedha, mbunge wa sasa wa Arusha, even ma-advocate] wakulima wana-green houses na wamefanya export business ya roses kwenda Europe kwa miaka kadhaa. They are organised and have their own (Tanzania Horticulture) association, taking advantage ya flower market ya Europe. Ni hivi karibuni tuu mambo yanakwenda vibaya kwa sababu ya current economic crisis. Ukiweza kuuza mauwa Europe, kwa nini ushindwe kuuza nafaka Saudi? Hili lawezekana na sio lazima ku-lease 500,000 hectors for 99 years kwa Dubai.

4. The bottom line, given incentives & government support (mfano wa Igumilo kule Mbarali) we have able Tanzanian's who can farm and export large quantities of rice & wheat to Saudi. The fully potential of BIG FIVE REGIONS (Mbeya, Ruvuma, Mtwara, Rukwa & Iringa) in terms of food security can be tested to the limit to supply food requirements of Saudi.
 
Jasusi:

Masahihisho 1985 Mwinyi alikuwa bado makamu wa rais.
Labda hiyo ilikuwa 1995. Lakini nakumbuka 1988 Mwinyi alifanya ziara ya kwanza Uingereza na aliomba apewe mameneja waliostaafu waje kufanya kazi Tanzania kwa sababu aliona mameneja wengi wana-boronga. alizua mgogoro mkubwa kuwa anataka kurudisha ukoloni na aamini wataalamu wa Tanzania. Ata mimi mwenyewe niliona anachemsha. Lakini baada ya kufanya kazi kwenye projects mbalimbali hapa US, nimeona kuwa kinachotukwamisha katika investments ni technocrats na capital. Na kama kuna nafasi ya watu wa nchi zingine kuleta capital na investments wapeni nafasi hizo.
Zakumi,
Thanks. Nilimaanisha 1995 alipokuwa anamaliza muhula wake.
 
..binafsi nadhani tuwe na juhudi za makusudi kabisa za kuhakikisha wakulima wetu wanaongeza uzalishaji per unit area.

..juhudi hizohizo zielekezwe kuwawezesha wafugaji na wavuvi kuongeza thamani ya mazao yao.

..binafsi sioni umakini na juhudi za serikali ktk kushughulikia masuala hayo mawili niliyoeleza.

..vilevile vipi kuhusu wawekezaji wa ndani? kwanini hawa hawasaidiwi kuweza kulikamata soko la ndani?

..Tanzania kumejaa waagizaji na wachuuzi tu. kina TATA,DAEWOO,..wa Tanzania ni kina nani? we need our own indigenous industrial captains.

RaiaMwema said:
MATOKEO YA MRADI WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI

MRIDI Kidumba ni miongoni mwa wakulima wadogo zaidi ya 200 kwenye mfumo wa umwagiliaji wa Igomelo, Wilaya ya Mbarali, Mbeya, kwa kazi yao wakulima hawa wanathibitisha uwezo wa mkulima mdogo nchini wa kuweza kulisha nchi na kutoa ziada ya kuuza nje iwapo atawezeshwa.

Katika umri wa miaka 42 sasa, Kidumba anaonyesha ni jinsi gani kilimo cha umwagiliaji kilivyoweza kumbadili kimaisha, kiasi kwamba unapozungumza naye unabaini ni jinsi gani fedha inavyoweza kumjengea mtu moyo wa kujiamini.

Kidumba alidhihirisha nguvu ya mkulima mdogo katika mapinduzi ya kilimo nchini hivi karibuni pale alipotembelewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akiwa katika ziara yake maalumu ya siku mbili mkoani Mbeya kukagua shughuli za kilimo.

Akijibu swali kuhusu mabadiliko aliyoyapata kutokana na kilimo hicho Kidumba alimwambia Waziri Mkuu Pinda:

"Kilimo kimenisaidia sana kuyabadili maisha yangu. Mwaka jana nilifikisha akiba ya shilingi milioni kumi. Zilikuwa kwenye SACCOS yetu. Nyumbani huwa tunakuwa na matatizo mbali mbali kama vile kuugua, huwa tunahangaika sana, kwa hiyo nilinunua taxi (gari dogo) ipo nyumbani kwa ajili ya kuhudumia familia.

"Sehemu nyingine ya ile pesa nikanunulia pembejeo kwa ajili ya kilimo cha msimu huu ambapo nimelima mpunga, mahindi, vitunguu na mazao mengine, kwenye akiba sasa zimebaki shilingi milioni moja.

"Nina nyumba ya tofali na nimepiga bati, lakini sasa naiona haifanani na mimi. Nimeanza kujenga nyumba nyingine bora zaidi itakayofanana na mimi."

Maelezo ya mkulima huyo yalimvutia Waziri Mkuu Pinda, hususan uamuzi wake wa kujenga nyumba nyingine inayofanana na hadhi ya mkulima huyo ya kifedha ya sasa, na ndipo alipomuuliza iwapo nyumba hiyo ataweza kulala kiongozi kama yeye?

Alijibu Kidumba kwa kujiamini: "Ni nyumba ambayo itakuwa ya hadhi ya kulala hata Waziri Mkuu."

Lakini fundisho kubwa lipatikanalo kutoka kwa wakulima hao ni jinsi kilimo cha umwagiliaji kilivyoongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo na kuwawezesha kulima mazao mbali mbali katika kipindi cha mwaka mzima.

Kidumba anasimulia akibainisha tofauti ya tija kati ya huko walikotoka na waliko sasa akisema: "Nilianza kulima kwenye skimu hiyo mwaka 1986, tulilima kienyeji, hatukuwa na utaalamu wowote, lakini baadaye skimu yetu iliboreshwa, tukapata utalaamu kupitia mabwana shamba, shamba darasa na mzungu mmoja aliyekuja hapa kijijini kwetu.

"Nimeongeza uzalishaji wa mpunga, sasa navuna gunia kati ya 25 hadi 30 za mpunga kwa ekari moja, huko nyuma nilivuna kati ya gunia saba hadi kumi. Mwaka jana nilivuna gunia 31 katika ekari yangu moja niliyolima, niliuza gunia 15 na kubakiza 16 kwa ajili ya chakula na mbegu.

"Hapa ni kulima mwaka mzima, tunaita hakuna kulala, mpunga nalima mara moja kwa mwaka, halafu kuna vitunguu nalima mara mbili kwa mwaka, mwaka jana nililima ekari mbili na kuvuna gunia 80 kila ekari, lakini nikienda vizuri navuna hadi gunia 100 kwa ekari.

"Kwa mfano Julai mwaka jana nilivuna gunia 100 kwa kila ekari, safari ya pili nilivuna gunia 107, na safari ya tatu nilivuna gunia 96, bei ya Januari huwa ni shilingi 50,000 kwa gunia la vitunguu, lakini baada ya Januari huongezeka hadi kufikia shilingi 70,000."

Ni wazi basi kipato cha mkulima huyu mdogo kutokana na vitunguu tu si chini ya shilingi milioni 12 kwa uzao mmoja iwapo ataviuza kwa shilingi 60,000 kila gunia na mavuno yakawa wastani wa gunia 100 kwa ekari moja na akalima hizo ekari zake mbili.

Ongezeko hilo la kipato halijionyeshi kwa mkulima huyu pekee, bali kwa wakulima wote zaidi ya 200 wanachama wa Ushirika wa Umwangiliaji Igomelo kama anavyoelezea Kidumba mwenyewe:

"Tupo zaidi ya wakulima 200 na tunafanana. Tukinunua pikipiki ni wote. Tunasomesha watoto hadi kwenye sekondari za kulipia, hatutegemei za Serikali pekee."

Hiki ni kipato kizuri kwa kiwango chochote kile kwa mwananchi wa kijijini tena kwa zao moja tu kati ya mengi anayolima, ni maelezo ya mkulima huyo mdogo kuhusu mafanikio yake yaliyomsukuma Waziri Mkuu Pinda kutoa tamko la kuwataka Hifadhi ya Kipawa Kipengere kufuta wazo lao la kulichukua eneo hilo akisema ni uwenda wazimu.

Alihoji Waziri Mkuu Pinda: "Hivi kweli mtu na akili zako unakuja hapa Igomelo na ukasema unachukua mashamba haya kuwa hifadhi, Serikali imewekeza, mlikuwa wapi huko nyuma?"

Pamoja na kuwa wakulima hawa wameboreshaji mfumo wao wa umwagiliaji na utalaamu waliopatiwa, yupo mtu muhimu sana kwao ambaye wanasema ndiye aliyewabadili kifikra ambaye wanamwita kwa jina la Daipesa, ambalo kwa hakika ni jina la mradi aliokuwa akiusimamia mzungu huyo.

Mwenyekiti wa Mfumo huo wa Kilimo cha Umwagiliaji Igomelo, Yohana Mbuna anasimulia: "Alikuja Mzungu mmoja hapa, alianza kwa kutuuliza maswali, nani mwenye simu kati yenu hapa anyooshe kidole?

"Hakuna aliyenyoosha. Akauliza tena, nani mwenye shilingi 10,000 kati yenu nimuongeze shilingi 90,000? Hakuna aliyekuwa nayo.

"Ndipo alipotueleza kuwa, watu wa Igomelo, sisi hatujawaletea samaki, tumewaletea nyavu mkavue samaki, tukiwaletea samaki mtakula na kurudi kule kule, tunawaletea mafunzo, leo hii tunamiliki power tillers (matrekta madogo) zetu wenyewe."

Uboreshaji wa mfumo huo wa umwagiliaji pamoja na mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na Mradi huo wa Daipesa kupitia utaratibu wa shamba darasa ndio kiini cha mapinduzi hayo ya kilimo kwa wakulima hao wadogo wa Igomelo.

Mbuna anasema kuwa kabla walikuwa wakitumia mfereji wa asili uliojengwa mwaka 1950 na ilipofika mwaka 2004 mfereji huo uliboreshwa na kugharimu shilingi milioni 300 kutoka Benki ya Dunia, mabadiliko ambayo yaliwezesha kupanuliwa kwa eneo la umwagiliaji kutoka hekta 100 za mfereji wa zamani hadi hekta 312 hivi sasa.

Mwenyekiti huyo anabainisha ongezeko la tija katika uzalisha mazao mbali mbali kama vile mpunga kutoka tani mbili kwa hekta huko nyuma hadi tani nne, mahindi kutoka tani moja hadi tatu, vitunguu kutoka tani 13 hadi 26 na nyanya kutoka tani tano hadi 35.

Anasema ongezeko katika tija limeyabadili sana maisha ya wakazi eneo hilo ikiwamo kupunguza kwa kiwango kikubwa tatizo la vijana kukimbilia mijini kutokana na kuwapo shughuli za kilimo hapo kijijini zenye kuwapatia kipato kizuri ikilinganishwa na maisha magumu wanayokabiliana nayo wakimbiliapo mijini.

Anayataja mabadiliko mengine kuwa ni pamoja na uwezo wa kusomesha watoto hadi elimu ya juu, kufanikiwa kujenga shule yao ya sekondari, ujenzi wa nyumba bora, ununuzi wa zana za kilimo kama vile matrekta madogo na ununuzi wa vyombo vya usafiri kama vile magari na pikipiki.

Kukua kwa kilimo cha umwagiliaji katika mfumo huo wa Igomelo kunajidhihirisha kwa wasafiri wafikapo katika mji mdogo wa Igawa ambako hukutana na vijana na akina mama wakiuza mahindi ya kuchemsha na karanga, na ni wazi hushangaa kwa sababu ni katika kipindi cha mwaka mzima.

Ushahidi mwingine ni kukua kwa haraka kwa mji huo wa Igawa ambao katika miaka ya nyuma baada ya usafiri kati ya Mbeya na Dar es Salaam kurahisishwa, ulididimia kiuchumi. Sasa hali ni tofauti, unakua kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa tija katika mazao ya kilimo kwenye Skimu hiyo ya Igomelo.

Skimu hiyo ya Igomelo inatoa funzo kwa Serikali kwamba hatuna haja leo hii ya kukimbilia kilimo cha mashamba makubwa ambayo yatatumia eneo kubwa la ardhi na kuwatelekeza wananchi zaidi ya asilimia 80 wanaotegemea kilimo.

Huu ni wakati muafaka wa kuachana na porojo na badala yake kuamua kwa dhati kuwekeza kwa wakulima wadogo kwa kubadili kilimo chao kutoka kile cha kizamani cha jembe la mkono na kuingia kwenye kilimo cha kisasa angalau kwa kuanzia na matrekta madogo, tija itaonekana na tutakuwa tumeingia kwenye mapinduzi ya kweli ya kilimo.
 
Nimekaa sana Mexico na USA, Serikali ya Mexico hairuhusu mtu kutoka nje kuown land hata kwa miaka 5, ila kama unataka kujenga nyumba au hotel unaweza kufanya hivyo. Iweje Tanzania miaka 99 shit. Hii ni kwa sababu ya uvivu wa kufikili na kuzoea omba omba, baada ya kuweka ****** chini na kutumia wataalamu wetu jisi ya kuzalisha chakula na kuuza uko saudi.
 
Mkuu mwanakijiji,maneno matupu ndani ya jf hayavunji mufupa.

Wazo:
Toa t'shirt nyingine za jf zenye ujumbe USIUZE ARDHI YETU KWA SAUDIA-JK,zisambazwe home kama kawa ktk maduka mbalimbali,naam itasaidia na mkwere ataona haya.

Sidhani kama general opinion ya jf ni kwa wawekezaji wa Saudia? Otherwise labda kama na mental retardation kwakukosa iodine ya kutosha na hivyo nimeshindwa ku draw conclusion in general jf members opinion nisaidiwe. Tusiwe tunapenda kupersonalize issue haisadi kwa taifa letu zaidi ya ku create enemity isiyo na sababu wala mshiko.
 
Manta hapo juu umeongea vitu. Sasa hao wa- Saudi na waraabu wa huko Bwana wanapata kidogo kuonja (kwa mfano mchele wa Kyela) sasa unajua uko natural unaharufu ya pekee. huwezi kulinganisha na michele hiyo ya makemikali ya Thailand na kwengineko. Hicho ndio kisa cha Waarabu hao kuanza kutafuta mbinu za kuweza kupata mchele huo wa aina ya Kyela ili warishishe hamu yao ya chakula muruwa. Wanajua wa_Tanzania hawana uwezo wa kuzalisha chakula hata cha kuwatosha wenyewe si kwa,mbia cha kuuza Saudia (ambako mchele unapendwa). Ndio maana wameomba kupatawa kijinafasi - basi watalima wenyewe- lakini waupate mchele wa Tanzania. Mchele bwerere huko kutoka Thailand na Nchi za South East Asia- lakini hawajaupenda huo . Unapendwa wa kwetu. Amini hivyo.
 
Sidhani kama general opinion ya jf ni kwa wawekezaji wa Saudia? Otherwise labda kama na mental retardation kwakukosa iodine ya kutosha na hivyo nimeshindwa ku draw conclusion in general jf members opinion nisaidiwe. Tusiwe tunapenda kupersonalize issue haisadi kwa taifa letu zaidi ya ku create enemity isiyo na sababu wala mshiko.
Wasaudia hawana shida ya pa kutafuta mchele. Wanaweza kuupata tu kununua kutoka katika nchi za Asia(pengine ziko karibu nao kuliko Tanganyika). Lakini ni suala la quality. Mchele wa Tanzania una quality nzuri na wameupenda huo -Una harufu nzuri na mzuri kwa pilau na biriani. Sasa hawa walioutangaza huko(Wazanzibari) nafikiri mngekuwa mnawahishimu na kuwapongeza. Wasaudi hawataki ardhi yenu Bwana. wanahitaji mchele wenye harufu nzuri tu? Jee mnaweza kulima wenyewe? kwa mfano kule Kyela. au katika maeneo mapya ya bonde la Mto Rujfiji na kwengineko. This is a simple issue. Lakini kwa mintarafu ya majadiliano - haya na tuendelee.
 
3. Serikali yetu inaweza kutumia fursa hii, ku-facilitate Saudi iwe soko kubwa la mazao toka Tanzania. We can sell them beef, onions, rice, fruits, sunflower oil etc. More important having processing and preservation facilities on the ground will give us the edge. Hili la kuuza nafaka Saudi watanzania tunaweza. Fifteen years ago, nani alihisi Tanzania tungeweza ku-export mauwa (roses) kwenda Europe. Hapo Arusha na Moshi kuna wazalendo wengi [waziri wa kwanza wa fedha, mbunge wa sasa wa Arusha, even ma-advocate] wakulima wana-green houses na wamefanya export business ya roses kwenda Europe kwa miaka kadhaa. They are organised and have their own (Tanzania Horticulture) association, taking advantage ya flower market ya Europe. Ni hivi karibuni tuu mambo yanakwenda vibaya kwa sababu ya current economic crisis. Ukiweza kuuza mauwa Europe, kwa nini ushindwe kuuza nafaka Saudi? Hili lawezekana na sio lazima ku-lease 500,000 hectors for 99 years kwa Dubai.

4. The bottom line, given incentives & government support (mfano wa Igumilo kule Mbarali) we have able Tanzanian's who can farm and export large quantities of rice & wheat to Saudi. The fully potential of BIG FIVE REGIONS (Mbeya, Ruvuma, Mtwara, Rukwa & Iringa) in terms of food security can be tested to the limit to supply food requirements of Saudi.

1. This is interesting. "We have Tanzanian's who can farm and export large quantities of rice and wheat", what are they waiting for? What I know, even mega producers like Vietnam and Thailand have banned export of food [including rice] due to growing domestic demand, let alone Tanzania. And if we can export food and rice, then Mohamed Enterprises and others wasingekuwa na biashara kabisa. We are importing rather than exporting food.

2. The other fact, very few Sub-Saharan countries (if any) produce sufficient food to feed its people. Hiyo mikoa unayoiita "Big five", nenda kafanye study uone kama watu wanajitosheleza kwa chakula mwaka mzima. And whether they are free from malnutrition.

3. Na unapozungumzia watanzania, ni mimi na wewe. So, unaposema kuna watanzania wanaweza kuzalisha chakula cha ziada, you may be cheating yourself. Hao watanzania ni wewe. Get out, grow rice and wheat and export to Saudi Arabia.

4. I repeat again, Saudi Arabia wanachotaka ni mchele na ngano. Hawajasema wana shida ya nanasi, roses, beef, sunflower oil and onions. I find your point no.3 digressing from the topic. Kuwa na green-house ya roses ni tofauti sana na kulima mchele heka 10,000. What do you think?

5. You are talking about incentives. Is there any other strong incentive than the hungry world?

6. It seems you have been out there for so long that you have lost the touch with the fact on the ground.
 
Wasaudia hawana shida ya pa kutafuta mchele. Wanaweza kuupata tu kununua kutoka katika nchi za Asia(pengine ziko karibu nao kuliko Tanganyika). Lakini ni suala la quality. Mchele wa Tanzania una quality nzuri na wameupenda huo -Una harufu nzuri na mzuri kwa pilau na biriani. Sasa hawa walioutangaza huko(Wazanzibari) nafikiri mngekuwa mnawahishimu na kuwapongeza. Wasaudi hawataki ardhi yenu Bwana. wanahitaji mchele wenye harufu nzuri tu? Jee mnaweza kulima wenyewe? kwa mfano kule Kyela. au katika maeneo mapya ya bonde la Mto Rujfiji na kwengineko. This is a simple issue. Lakini kwa mintarafu ya majadiliano - haya na tuendelee.

Pakacha shukrani kwa taarifa hizo...Kwasababu sasa tunajuwa ni quality ya mchele huo na si vinginevyo...Kwasababu viongozi wetu wasingechelewa kutuambia kuwa...Aaah wataenda nchi nyingine kununua ama wenzetu wa nchi jirani watachamgamkia deal nk....Si unajuwa misemo yao mingi kuwa tusipochukua deal wengine watachukua? Mfano wako kuhusu Thailand pia uma make sense zaidi kwenye kuhitimisha hilo.

Mkandara,pointi hii pia ina uhusiano na maelezo yako kadhaa hapo nyuma kuhusiana na ardhi yetu kupewa waarabu vs wazungu...Haina maana kuwa kwasababu tulifanya blunder kwa wazungu basi we do the same with them Arabs ili kuweka usawa.

Matatizo kama hayo yamei cost nchi yetu mara nyingi sana,kuanzia ulazima wa kubadili marais kwa sababu za dini nk,sasa baadae usije kushangaa ili kuwepo na usawa kila kabila likaanza kudai kuwa na zamu ya urais.

Tukilea mentality kama hizo tutapata hasara.
Na hivyo basi ni muhimu kujipanga na ku correct yale makosa tuliyoyafanya huko nyuma bila ku create divisions,tuwe kama Taifa moja kwasababu bila kufanya hivyo,matokeo yake ni mifarakano na umasikini kubobea.

Na mojawapo ya opportunity ya kuwaondoa wananchi walio wengi kwenye umasikini basi ni LAZIMA umuhimu uwekwe kwenye kilimo. Msaudi kutaka mchele/ardhi ama la,kilimo NI LAZIMA kipewe kipaumbele kama ni kweli viongozi wetu wana nia nzuri na Taifa na wananchi wake. Opportunity kama hii inapokuja,ni kazi ya viongozi wetu kujipanga na kuwaweka wananchi sawa ili wanufaike. Na tatizo siyo kwamba serikali haijui hilo,tizama mission statement ya kampuni ya KAGODA,utachoka,yani kama yale yangetekelezwa kiukweli mbona wananchi wangepata maendeleo!

Na wale wenye kudhani kuwa waafrika hatuwezi wanakosea,wakaazi wa maeneo ya kilimo ni watanzania,asilimia kubwa wanategemea kilimo,sasa bila kuwasaidia wananchi wako,utaleta settler kuja kulima chakula bora na kuondoka nacho kwasababu ame lease ardhi,hilo ni sahihi? Wao wanataka mchele,ni kwanini tusijipange tuwauzie?

Habari hii imeletwa ikionyesha kwamba wasaudia wanataka kulease ekari laki tano kwa madhumuni ya kulima mpunga,hatujui terms and conditions kama wanazo,ila za kwetu sisi tunazijua. Na kama habari hii imeletwa hapa ili kupata maoni,basi yametolewa maoni mazuri zana tu.

Tunaelewa tumeshafanya mikataba mibovu mingi tu,lakini haina maana tuendelee tu kufanya mikataba mibovu,bali kufanya mikataba yenye kuwanafuisha wananchi na kujaribu kuirekebisha ile mibovu sambamba na sheria zinazoisimamia.

Serikali ikitilia mkazo kwenye kilimo,basi tunaweza kuona jinsi Taifa litakavyobadilika ghafla na kuwa na neema.
 
1. This is interesting. "We have Tanzanian's who can farm and export large quantities of rice and wheat", what are they waiting for? What I know, even mega producers like Vietnam and Thailand have banned export of food [including rice] due to growing domestic demand, let alone Tanzania. And if we can export food and rice, then Mohamed Enterprises and others wasingekuwa na biashara kabisa. We are importing rather than exporting food.

2. The other fact, very few Sub-Saharan countries (if any) produce sufficient food to feed its people. Hiyo mikoa unayoiita "Big five", nenda kafanye study uone kama watu wanajitosheleza kwa chakula mwaka mzima. And whether they are free from malnutrition.

3. Na unapozungumzia watanzania, ni mimi na wewe. So, unaposema kuna watanzania wanaweza kuzalisha chakula cha ziada, you may be cheating yourself. Hao watanzania ni wewe. Get out, grow rice and wheat and export to Saudi Arabia.

4. I repeat again, Saudi Arabia wanachotaka ni mchele na ngano. Hawajasema wana shida ya nanasi, roses, beef, sunflower oil and onions. I find your point no.3 digressing from the topic. Kuwa na green-house ya roses ni tofauti sana na kulima mchele heka 10,000. What do you think?

5. You are talking about incentives. Is there any other strong incentive than the hungry world?

Potential of the big 5 regions in food production in Tanzania is under-utilised. With proper policy, investment in research and development, these regions can cater for national need of food and surplus for export. The big problem for these regions includes luck of infrastructure, transportation (road passable throughout the year), food processing and storage facilities. The post harvest loss (mazoa kuoza shambani, kuliwa na wadudu nk) is huge in the big 5 regions and most other areas in Tanzania. Kwa upotevu huo mkubwa wa mazao na miundo mbinu mibovu, ukulima mara nyingi haulipi.

Wakulima wetu hawapati support ya kutosha in terms of mikopo, farm implements, fertiliser supply and adequate technical support such as farm extension officers etc. Also we need investment in irrigation, research (agri-varsities) and development of crops with high yield etc. With proper National agriculture policy and major investment by Tanzania government to support farming industry our country can improve in food production tremendously and make farming profitable. A deliberate effort by government to support its farmers is necessary. Call it farming subsidy or something else, it is a necessary evil. It is for the same reasons US and European governments still provide farm subsidy. If subsidy is removed in these countries, most farmers will not make profit and this has political and economical implication.

On the other hand there are success programs in rice farming in Tanzania. Look at the example of rice irrigation program at Igomelo and Lower Moshi, rice production increased tremendously and farmer’s well being have been transformed. More of such support will increase rice production to cater for export market.

Serikali ya Malawi imefanya miujiza kwa zao la mahindi. Kwa kutoa mbolea na mbegu bora za mahindi (high-yield maize seeds), production increased from 1.2 in 2005 to 3.7 tonnes in 2007 Malawi's farming revolution sets the pace in Africa - Africa, World - The Independent , Malawi was able to produce enough and export maize within 3 years.

Serikali yetu inaweza kufanya zoezi la makusudi (kama walivyofanya Malawi kwa zao la Mahindi) kusaidia wakulima wa mchele na ngano kuongeza uzalishaji wa kutosha na surplus kuuza nje ya nchi kama Saudi. Hili lawezekana na sio lazima ku-lease 500,000 hectares for 99 years kwa Saudi.

Of course horticulture is different from rice farming, hili la mauwa ni mfano kwamba, with right incentives farmers can deliver. In this case main incentive is the European market and proximity of Arusha/Moshi farmers to the international airport KIA which allows flowers to be transported from the farm to the market within 24 hours.
 
Tunajua sasa hivi dunia nzima inaangaika kutafuta chakula especially nchi za Asia mfano China ambayo ilikuwa na ardhi ya kutosha, lakini most of it now imegeuzwa kuwa viwanda na nyingine kuwa makazi ya watu waliokuja kufanya kazi kwenye hivyo viwanda. nNa kwasababu watu wengi wanaishi mijini wana consume more food than living in the rural areas where they eat as community. We need to understand the scarcisity ya commodity inayo face dunia na kutumia to our advantage.

1. I do not disagree na Saudi kuja kuinvest Tanzania kwenye agriculture , what I am dissapointed ni wao kupewa hectare nyingi hivo for 99 year lease. Imagine all f us tunaochangia humu tutakuwa tumeshaondoka na pia some ya vizazi vyetu watakuwa hawapo. Why tuwape ardhi ya watoto wetu amabyo baba zetu walituachia.

2. I suggest wapewe hectare zisizozidi 100,000 na kwa alease isiyozidi miak 25. Then sisi ndio tuchague maeneo yakuwapa na sio wao kutupangia eneo. Possibly mikoa kama Kigoma, Rukwa na Ruvuma ambayo inahitaji maendeleo kutokana na kodi watakazo tozwa.
Kutokana nakuwa na heactre hizo, they will be a need to improve the infrastracture na the energy to power their irrigation na kuweza kufikisha mazo yao bandarini.kwa hiyo watashirikian na serikali yetu kufanikisha including kuboresha bandari.

3. Watanzania tunauwezo wa kulima mashamba makubwa na kuuza mazao nje, mfano ni mashamba ya maua Arusha na Kahawa kilimanjaro. Tunachohitaji ni mikopo ya hizo fedha Jk alizosema za EPa na mamilioni China na Turkey waliyoahidi. Then Saudi watulipe bei nzuri kama the rest of the world hapo ndipo tutajilaumu.
 
Back
Top Bottom