Sauli: Bilionea ambaye Wazungu/Wageni wanamtambua Waswahili hatujamfahamu kabisa

Sauli: Bilionea ambaye Wazungu/Wageni wanamtambua Waswahili hatujamfahamu kabisa

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Mwezi uliopita nlipata bahati ya kutembelea Jiji la Mbeya. Sikuishia Mjini nlienda moja ya Wilaya zilizopo Jijini humo ya Chunya na kufika katika barabara iliyo juu kabisa Katika Afrika Mashariki.

Issue ilikuwa ni kuwasindikiza Jamaa zangu Makaburu toka Kusini mwa Afrika waliokuja kufanya biashara ya Madini na Bwana Mmoja Aliyefahamika kwa jina la Sauli. Nilimpomsikia Sauli kwa mara ya kwanza nlikumbuka bwana Mmoja mwenye maduka ya SH Amon na pia nmekuwa nikitumia sana Hotels zake za Landmark. Hakuwa huyo.

Sauli huyu ni mchimbaji mkubwa wa madini ya Dhahabu huko Chunya wa miaka mingi tu. Huyu alimpa zawadi ya Dhahabu Kilo 5 mh Rais Ben Mkapa. kilo 5 ya dhahabu kama zawadi tu.

Kuwa eee bwana kiongozi... Mimi sina kitu mzee... Chukua haka kadhahabu kiasi nawe ukatengeneze chain, kwa sasa sipo vizuri. Akamkabidhi. Dhahabu Jiwe Gwala.

Nasikia wazungu waliokuwa wanafanya naye Biashara waliamua siku moja kuja mtembelea; kwa ukwasi alio nao walitegemea hata angekuwa na jeshi lake Binafsi. Walishangaa sana kumkuta yupo simple tu.

Mtu ambaye walijua kuingia kwake ingekuwa shida kwa security clearance yake mpaka kufika kumwona mmeshachoka sana, wakamkuta jamaa mshkaji tu. Walimuuliza bro hivi watu si wanaweza kukuibia madini yako yote? Akacheka sana, akasema nawakaribisha waje tu.

Wazungu wakatizamana na kuambiana, "anyway ngoja tuseme yaliyotuleta tusije onekana wambea bure" akasema "haswaaaaaa, nipeni deal"

Huyu jamaa ndio kanunua Scania kaziweka ndio usafiri wa kutoka Dar to Mbeya na Mbeya to Dar. Yeye hanunui mabasi ya mikoani ananunua Scania ( Kiduku Lilo aone) anayanunua anayafungua kwenye karatasi ndio yanaanza tumika. Scania siyo Ching Chong au Jadong. Scania

Jamaa humsikii kwenye Radio wala wapi. Ma-don wenzie ndio wanamfahamu huko ughaibuni na bondeni. Nje wanamtambua kinyama. Mimi nitamfahamia wapi mtu ambaye hafaidiki na kufahamiana nami? Aaaah we acha tu.

Jamaa ana pesa chui haruki. Acha wale machalii wa Arusha wanasema wanapesa mbwa haruki. Jamaa pesa zake Chui haruki.

Mimi nimeweka haya kuna wengine watakuja kuongezea nyama.
 
Huku chuga mwana tulikuwa na MSUYA bana. VX yake mpya ilikwama akatokea jamaa na ndondo lake (mandolini) akamvuta gari ilipotoka akashuka akamwita jamaa wa mandolin akampa funguo la hiyo VX liwe lake kimojaa!! marehemu MSUYA ukifika kwake yuko simpo hamna hata kwere na kabati limejaa mawe hapo! kila mtu anaingia tuu bila shida. utamuibia vipi wakati nyamera wote hapo town wanammanya?
 
Juzi kati tukiwa katika maongezi na my Salty Dawg..
mara tukabadili ukurasa wa maongezi, tukaingia kwenye usafirishaji...
Looh. ndo ikawa mara ya kwanza sikia ilo jina na ikawa ndo mara kwanza kujua kwamba Scania wanatengeneza mabasi...

kwa mara ya pili nimekutana na jina ili hapa jukwaani.


Sent using Jamii Forums mobile app
Ok Mkuu makampuni yote makubwa Volvo, Scania, Man diesel na Mercedes wanatengeneza diesel engine na body za bus pamoja na maroli ingawaje body nyingi wataalamu ni Brazil zina series ya P kuendelea kwa Scania na zipo bus ambazo zina madaraja Kama hotel yaani five star au 3 star...
 
Yaani ndugu yangu, umeshindwa hata kuelezea huyo Bilionea Sauli wa Mbeya ana ukwasi wa kiasi gani? Yaani kuwa na buses za Sauli na kuchimba dhahabu ni bilionea tayari? U bilionea nadhani watu wanaudharau sana, wanaona kama mchezo mchezo tu.
 
Yaani bilionea atoke chunya? Mmhhhh, maana chunya dhahabu zenyewe ni za kutafutiza kweli kweli ... nimewahi kuchimba miaka ya 2000 mwanzoni maeneo ya iwalanje ifwenkenya na makongorosi ... daah acha tu
 
"Alimpa Mkapa dhahabu kilo 5 atengeneze cheni"... tuache utani, dhahabu kilo tano inalisha chunya nzima miezi kama sio miaka....
Acha uongo mkuu....
Tuchukulie dhahabu hii ilipatikana jana ambayo ni sawa na gram 5000
Gram 1 kwa bei ya jana soko la dunia ilikua 127,990 Tsh.
Tuchukulie hii dhahabu ilikua na Purity ya 100% (swala ambalo ni gumu lazilma iwe pungufu)

So
5000*100%*127,990=636,950,000Tsh.
Je hii fedha unailisha chunya kwa miezi au mwaka??
 
huku chuga mwana tulikuwa na MSUYA bana.VX yake mpya ilikwama akatokea jamaa na ndondo lake(mandolini)akamvuta gari ilipotoka akashuka akamwita jamaa wa mandolin akampa funguo la hiyo VX liwe lake kimojaa!!marehem MSUYA ukifika kwake yuko simpo hamna ht kwere na kabati limejaa mawe hapo!kila mtu anaingia tuu bila shida.utamuibia vipi wakati nyamera wote hapo town wanammanya
...alikuwa wa kawaida tu ,acha kuendekeza uongo.
Hiyo hotel hapo Triple A- mbona ya kawaida tu
 
Back
Top Bottom