Sauli: Bilionea ambaye Wazungu/Wageni wanamtambua Waswahili hatujamfahamu kabisa

Sauli: Bilionea ambaye Wazungu/Wageni wanamtambua Waswahili hatujamfahamu kabisa

Yaani bilionea atoke chunya?? Mmmmmhhhhh, maana chunya dhahabu zenyewe ni za kutafutiza kweli kweli...nimewahi kuchimba miaka ya 2000 mwanzoni maeneo ya iwalanje ifwenkenya na makongorosi...daah acha tu
Kiongozi sikupingi juu ya experience yako. Ila naomba utambue na unielewe kabisa CHUNYA KUNA MADINI YASIYO HATA NA MPANGO WA KUISHA LEO WALA MWAKANI naomba uamini hivyo NA jua lililokupata ilikua bahati mbaya tu
 
Mwezi uliopita nlipata bahati ya kutembelea Jiji la Mbeya. Sikuishia Mjini nlienda moja ya Wilaya zilizopo Jijini humo ya Chunya na kufika katika barabara iliyo juu kabisa Katika Afrika Mashariki.

Issue ilikuwa ni kuwasindikiza Jamaa zangu Makaburu toka Kusini mwa Afrika waliokuja kufanya biashara ya Madini na Bwana Mmoja Aliyefahamika kwa jina la Sauli. Nilimpomsikia Sauli kwa mara ya kwanza nlikumbuka bwana Mmoja mwenye maduka ya SH Amon na pia nmekuwa nikitumia sana Hotels zake za Landmark. Hakuwa huyo.

Sauli huyu ni mchimbaji mkubwa wa madini ya Dhahabu huko Chunya wa miaka mingi tu. Huyu alimpa zawadi ya Dhahabu Kilo 5 mh Rais Ben Mkapa. kilo 5 ya dhahabu kama zawadi tu.

Kuwa eee bwana kiongozi... Mimi sina kitu mzee... Chukua haka kadhahabu kiasi nawe ukatengeneze chain, kwa sasa sipo vizuri. Akamkabidhi. Dhahabu Jiwe Gwala.

Nasikia wazungu waliokuwa wanafanya naye Biashara waliamua siku moja kuja mtembelea kwa ukwasi alio nao walitegemea hata angekuwa na jeshi lake Binafsi. Walishangaa sana kumkuta yupo simple tu.

Mtu ambaye walijua kuingia kwake ingekuwa shida kwa security clearance yake mpaka kufika kumwona mmeshachoka sana... wakamkuta jamaa mshkaji tu... walimuuliza Bro hivi watu si wanaweza kukuibia madini yako yote? Akacheka sana... akasema nawakaribisha waje tu.

Wazungu wakatizamana na kuambiana... "anyway ngoja tuseme yaliyotuleta tusije onekana wambea bure" akasema "haswaaaaaa...nipeni deal"

Huyu jamaa ndio kanunua Scania kaziweka ndio usafiri wa kutoka Dar to Mbeya na Mbeya to Dar. Yeye hanunui mabasi ya mikoani ananunua Scania ( Kiduku Lilo aone ) anayanunua anayafungua kwenye karatasi ndio yanaanza tumika. Scania....siyo ching chong au jadong. Scania

Jamaa humsikii kwenye Radio wala wapi ma Don wenzie ndio wanamfahamu huko ughaibuni na bondeni. Nje wanamtambua kinyama.... Mimi nitamfahamia wapi mtu ambaye hafaidiki na kufahamiana nami? Aaaah we acha tu.

Jamaa ana pesa chui haruki. Acha wale machalii wa Arusha wanasema wanapesa mbwa haruki. Jamaa pesa zake Chui haruki.

Mimi nimeweka haya kuna wengine watakuja kuongezea nyama.........
Pesa za malikale za rupia na sio za kustruggle
 
Story nzima nilikuwa napatafuta utapoandika eti ana pesa kuliko wakina MO walahi ningepigwa BAN huu ujinga nauonaga sana vijiweni huku.

Tz wenye pesa ni wengi sanaaa tena sanaaa ila ni level za u-millionare/Mult millionaire kuwa Billionaire ni kitu kingine kabisa hapa Duniani.
Ni Hadi ukajitangaze Forbes ndo utajulikana
 
"Sauli huyu ni mchimbaji mkubwa wa madini ya Dhahabu huko Chunya wa miaka mingi tu. Huyu alimpa zawadi ya Dhahabu Kilo 5 mh Rais Ben Mkapa. kilo 5 ya dhahabu kama zawadi tu."
Hii statement si ya kweli.[emoji121]
 
Mbona Kama analazimisha tumuelewe wakati inaonekana kabisa huyo mtu bado. Au ndo wivu tu kushindana na wakaskazini.
 
Yaani bilionea atoke chunya? Mmhhhh, maana chunya dhahabu zenyewe ni za kutafutiza kweli kweli ... nimewahi kuchimba miaka ya 2000 mwanzoni maeneo ya iwalanje ifwenkenya na makongorosi ... daah acha tu
Ulitumia nini kuchimba ukakosa?
 
Kiongozi sikupingi juu ya experience yako. Ila naomba utambue na unielewe kabisa CHUNYA KUNA MADINI YASIYO HATA NA MPANGO WA KUISHA LEO WALA MWAKANI naomba uamini hivyo NA jua lililokupata ilikua bahati mbaya tu
Dhahabu pesa yake mbuzi tu,nenda kahama na geita matajiri wa dhahabu wanamiliki lodge na mafuso
 
Hahahahahahhaha habari hizi bhana, huyomtu umemtaja hapa kwa chunya ni mdogo saana sana tena. Doo anayo yakucheba lakin anaweza hata asiwe top 5 ya wenye pesa chunya. Umemkuza sana lakin nazan nikwakuw hukuamua kufanya tafiti ndogo tu. Ila bus kweli ni mpya na brand za kutisha scania na Volvo hana utumbo kule piah ni mpya kabisa. Gari moja karibu 1B eti inagharimu
 
Back
Top Bottom