ok,mie nilijua ni vipanga wa ud,sua,mzumbe na udom ndo mikopo inawahusu!kumbe hata huko kwa waliofel wanakumbukagwa,basi serikali yetu ina fedha za mchezo.
Wewe sema tu waliofeli kumbuka hata walioko huko ud,mzumbe sua n,k wengine walitoka shule za private baada ya kufeli darasa la saba na hata form 4.
Hivi kwa akili yako serikali pekee ingeweza kuwa na vyuo vya kutosha kwa wanafunzi wote wanaomaliza form 6 na kutoka vyuoni.
Utaratibu wa vyuo binafsi uko hata huko ulaya walikopiga maendeleo kwenye kila kitu.
Acheni kukarii ud kwani hawana uwezo wa kuchukua wanafunzi wote na imebidi kisingizio kiwe ufaulu wa juu kama ilivyokuwa kwa bodi kwamba ili upate mkopo basi uwe na division 1 au 2.
Mataifa yaliyopiga hatua kielimu mtu mwenye principle 2 hakosi kupata elimu ya chuo kikuu.
Jiulize kama ilikuwa sahihi kwa miaka ya nyuma eti mtu ukiwa na division 2 hupati nafasi pale ud.Sasa unadhani hiyo ilikuwa ni sifa au kudumaza elimu.
Tatizo kwa miaka mingi ilikuwa ni kwa serikali kushindwa kuwekeza ktk elimu ya juu kama ilivyokuwa hata kwa elimu ya sekondari.Jilulize kama elimu ya sekondari ingekuwa ni jikumu la serikali pekee ni wangapi waliopo hapo ud wangekosa nafasi hiyo kwani kuna wengi wametoka shule za sekondari za private baada ya kukosa nafasi ktk shule za serikali na kuambiwa eti wamefeli kumbuka sababu ni kuwa walikosa nafasi.
Kumbuka bongo mtu ukikosa nafasi ktk shule au chuo unaonekana umefeli wakati ni uzembe wa kushindwa kuongeza vyuo na shule.
Ni swala la muda tu kabla hatujasikia baadhi ya vyuo vikuu binafsi kupanda chati na kuwa vyuo bora kabisa.
Kumbuka hata ud ilianza kwa kusuasua tu ukilinganisha na vyuo vingine vya nje kutokana na uchanga wake kwa wakati ule.