SAUT yafuta degree za Madaktari wa Afya 162 waliohitimu Chuo cha Mt. Francis

SAUT yafuta degree za Madaktari wa Afya 162 waliohitimu Chuo cha Mt. Francis

Yaan nimemaliza 2015 na gamba mmenipa na nimeshapata ajira halafu unadai nirudishe transcript uidhinishe!!!

Uchawi ndio huu wa nchi yenye mbuzi wasio na mwenyewe wanaozunguka jiji la Mwanza na Ilala.. Anyway
JPM ndo alikuwa anapita na watu hapa , inakuwaj napewa transcript bila idhin ya chuo kama sio walitaka kwenda kuwasafishia matokeo watu wao waliowapata wakiwa mwaka wa mwisho
 
Tukiacha kila mtu afanye anavyofikiria kichwani mwake mambo hayataenda, taratibu ziko wazi fuata kuepuka usumbufu na kama unadhani degree ni kile tu kilichopo kichwani kazi kwako kama utatumia kichwa kuomba kazi.
transcript inafikaje mkonon kwa mtu bilq chuo kuweka idhini? hapo walitaka kufanya ukanjanjaa kweny hizo results slip , kuna watu wao walitaka waweka sawa na wengine kuwaning'inia shingon
 
Ada watawarudishia au yale waliyosoma watayafuta kwenye vichwa vyao? Kosa ni lao au hao wanachuo?
chuo kina makosa maana wamerudia kosa moja kwa miaka 4 mfululizo unatoa results slip bila idhin ya senet?
 
Hii nchi kuna wazee wanaroho za kichawi kabisa, kwahiyo hizo transcript zikisharudishwa ndio wanarudi kuwa madaktari?!
 
Hizo nakala za masomo hao watahiniwa walipewa vipi bila ufahamu na uidhinishaji wa seneti, ina maana zilitolewa kinyemela?

Kuna mtu alikula pesa hapo, naamini atakuwa alishapoteza kazi muda mrefu, ila kama yupo ofisini itakuwa ni maajabu..

Na hao watahiniwa ni kama hawaamini walitoka salama, wanaonekana hawajiamini, ndio maana wameingia mitini wasije zirudisha waambiwe walifeli masomo mawili wanatakiwa kuyarudia.
UCHUNGUZI WA KINA UFANYIKE.1.TAKUKURU WAKICHUNGUZE CHUO.2.WATUHUMIWA WACHUNGUZWE.3.HOSPITALI WALIZOKUWA WANAFANYIA KAZI ZICHUNGUZWE.4.BARAZA LICHUNGUZWE.AFU TAARIFA IFIKE KWA 1.UMMY MWALIMU.2.WAZIRI WA ELIMU.3.WAZIRI MKUU.4.RAISI KWA AJILI YA MAAMUZI.
 
"walikataa kwa makusudi kurudisha nakala za masomo 'transcripts' walizopewa bila ufahamu na uidhinishaji wa seneti ya chuo kikuu" [emoji848]
 
HIVI HII POST SIYO HOAX KWELI? KAMA SIYO HOAX, HIKI KITU KILIWAHI KUFANYIKAJE, NA KWA YA AKILI YA NAMNA GANI?
 
Jamani Jamani 🥲
Kwani hizo transcripts walijichukulia wenyewe?
Nyie kuweni na huruma na maisha ya watoto wa watu
Shule ya udaktari ilivyo ngumu[emoji119]kirahisi tu umfutie mtu elimu aliyoisotea kwa miaka 6[emoji15]!
Kwani wakati wanawapa hawakuona kama hazijaidhinishwa?
Huzuni sana
 
Kuna mambo kabla hujayafanya inatakiwa ufikirie sana.

Je, kwa hili SAUT wanaweza kushitakika kwa kuhatarisha maisha ya watanzania zaidi ya milioni 50?.

Ni swali najiuliza na kufuatilia nikawape mchongo wanaharakati 😂
 
Kuna mambo kabla hujayafanya inatakiwa ufikirie sana.

Je, kwa hili SAUT wanaweza kushitakika kwa kuhatarisha maisha ya watanzania zaidi ya milioni 50?.

Ni swali najiuliza na kufuatilia nikawape mchongo wanaharakati [emoji23]
Ndio inabidi washtakie kwa uzembe huu..
 
Ndio inabidi washtakie kwa uzembe huu..
Maombi kwa Mahakama:-

1. Itamke SAUT wamehatarisha.maisha ya wa Tz
2. Itoe amri kwa wizara husika na TCU kukifungia Chuo cha SAUT
3. SAUT ilipe fidia Tshs zakutosha 😀
4. Gharama za kesi ziwe juu yao
5. Nafuu nyingine kadiri itakavyoonekana ni haki
 
Huzuni sana
Waliwapa za nini hizo transcript kama zilikuwa hazijakamilika?
Walikuwa wanakimbilia wapi?


Waanze kwanza viongozi kuachia ngazi

Eti leo sina hili na lile mtu anaamka tu anafuta kidegree changu nilichokisotea kwa jasho na damu..wazazi wamejipiga huku na huku hadi nimesoma aisee
Hawa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mwanza. Uamuzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino cha Tanzania (SAUT) kufuta shahada za wahitimu 162 kutoka Chuo cha Tiba cha Mtakatifu Francis, Ifakara umeibua mjadala huku wadau wa elimu wakigawanyika.

Licha ya kukiri kuwa seneti ndicho chombo chenye mamlaka na uamuzi wa mwisho wa masuala yote ya vyuo vikuu, baadhi ya wadau wameshauri busara na ubinadamu utumike kwa kufuta taarifa za matokeo badala ya shahada.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa jana na kusainiwa na Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Saut, Profesa Costa Mahalu, uamuzi wa kufuta shahada hizo umefikiwa baada ya wahitimu hao waliohitimu kati ya mwaka 2015 hadi 2019 kukaidi agizo la kurejesha taarifa za matokeo zilizotolewa bila idhini ya seneti.

Waliofutiwa shahada ni kati ya wahitimu zaidi ya 300 waliotakiwa kurejesha taarifa zao za matokeo, ambapo baadhi walitii agizo na 162 kukaidi.

Chuo cha Tiba cha Mtakatifu Francis, Ifakara kiko chini ya SAUT. Akizungumza na Mwananchi kwa simu jana, Profesa Mahalu alisema uamuzi huo uliozingatia kifungu cha 47(1) na (2) cha Sheria ya Vyuo Vikuu namba 7 ya mwaka 2005 ikisomwa pamoja na kifungu cha 6(3)(ii), 7, 8 na kanuni ya 29(1) ya charter ya Saut ulifikiwa na kikao cha dharura cha Seneti kilichoketi Machi 25, 2023.

“Wahitimu wote wanapaswa kufahamu kuwa taarifa za matokeo, vyeti na shahada ni mali ya chuo na lazima zipitishwe na Seneti. Transcripts zilizofutwa hazikupitishwa na seneti. Sasa ni wajibu wao kuzirejesha ili wapewe mpya zilizoidhinishwa,” alisema Profesa Mahalu. Aliongeza, “sasa ni jukumu na wajibu wa wahitimu hao kutii agizo la seneti kwa kurejesha taarifa za matokeo zilizoidhinishwa kwa mujibu wa sheria.”

Alisema agizo la kurejesha taarifa hizo halikuwa na madhara kwa wahitimu wala shahada zao, bali kilichotakiwa kurekebishwa ni alama za ufaulu kulingana na mfumo mpya uliotolewa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) mwaka 2015.

“Kilichotakiwa kufanyika ni kubadilisha transcripts zilizotolewa kimakosa huku wahitimu wakibaki na hati zao na transcripts za zamani ambazo zina grading system iliyopitishwa na Senate ya Saut,” alisema Profesa Mahalu.

Kwa mujibu wa Profesa Mahalu, baadhi ya viongozi wa Chuo cha Tiba cha Mtakatifu Francis waliohusika kutoa taarifa za matokeo ya wahitimu bila kuidhinishwa na seneti tayari wamewajibika kwa kuachia nafasi zao.
Akizungunzia madhara kwa wahitimu waliofutiwa shahada, hasa waliojiendeleza kielimu wakitumia shahada zilizofutwa, Profesa Mahalu alisema Saut haiwezi kuviamulia vyuo vilivyowatunuku shahada hizo nini cha kufanya.

“Hilo litawahusu wahitimu na vyuo walivyohutimu na kutunukiwa shahada zingine zilizotokana na zilizofutwa,” alisema.Hata hivyo, baadhi ya waathirika baadhi yao wakiwa wameajiri, waliiambia Mwananchi kuwa wanaamini wana haki kisheria.

“Tulipewa nakala na vyeti vilivyotiwa saini na seneti ya chuo kikuu na baadhi yetu tulivitumia kuombea kazi, hii si haki kwetu hata kidogo na mimi binafsi nitakata rufaa kisheria,” alieleza mmoja wa wahitimu hao.
Mwingine aliyetaka jina lake lihifadhiwe, alikiri kupokea notisi mara tatu iliyomtaka arejeshe nakala hiyo chuoni, lakini alisita kutekeleza hilo.

Mhitimu mwingine aliyejitaja kama Sophia, alisema hakuona matangazo ya kutakiwa kwa nakala hizo kwenye magazeti, alichokiona ni picha ya kipande cha tangazo la kuvuliwa shahada ikiwa na jina lake.

Akizungumzia suala hilo, mshauri wa masuala ya elimu, Dk Wilberforce Meena alisema, “binafsi naona si sahihi kufuta shahada za wahitimu iwapo walifanya na kufaulu mitihani yao bila udanganyifu; nadhani njia sahihi ingekuwa kuwafutia taarifa za matokeo. Mdau wa Elimu, Avemaria Semakafu alisema kisheria, seneti ndiyo inaidhinisha matokeo ya wahitimu wa vyuo vikuu, hivyo ni kosa iwapo taarifa za matokeo zilitolewa na uongozi wa chuo bila idhini ya seneti.

“Hata hivyo, kosa hilo si la wanafunzi, bali ni la kiutawala kwa uongozi wa chuo uliotoa taarifa ya matokeo yasiyoidhinishwa na seneti,” alisema Semakafu aliyewahi kuwa naibu katibu mkuu Wizara ya Elimu.

Ilivyoanza
Sakata lilianza mwaka 2015 baada ya TCU kutoa mwongozo mpya wa upangaji matokeo kwa vyuo vikuu unaoelekeza alama A kutolewa kuanzia ufaulu wa asilimia 70 hadi 100.

Profesa Mahalu alisema wakati huo kuwa maelekezo hayo yalikinzana na viwango vya ufaulu vya Saut iliyokuwa inaelekeza alama A kutolewa kwa ufaulu unaoanzia asilimia 80 hadi 100 lakini chuo husika kikatumia mfumo tofauti na maelekezo, hivyo kukilazimu uongozi wa Saut kuitisha upya fomu za matokeo ili kutoa nyingine.

MWANANCHI
 
Usiombe yakukute 🤔, ila SERIKALI inabidi ifanye maamuzi sahihi kuhusu ili swala ,
1. Kutengua aya maamuzi ya kukurupuka.
2. Kuiwajibisha hiyo seneti uchwara hususani bwana costa titch.
3. Chuo kiwe na utaratibu mzuri wa kutoa transcript kwa wahitimu.
Mliokuwa mnashabikia huo upopoma wa madaktari mjifunze kunyamaza, mbona sasa wameanza kujisalimisha? Walifanya ujinga sana!
 

Attachments

  • Screenshot_20230329-200750_Opera News.jpg
    Screenshot_20230329-200750_Opera News.jpg
    197.4 KB · Views: 5
Sauti na Bugando ni taasisi mbili tofauti, ila zote ziko Mwanza.
 
Back
Top Bottom