SAUT yafuta degree za Madaktari wa Afya 162 waliohitimu Chuo cha Mt. Francis

SAUT yafuta degree za Madaktari wa Afya 162 waliohitimu Chuo cha Mt. Francis

Tuna tatizo la uhaba wa madaktari nchini ukilinganisha Na mahitaji na idadi ya watu hivyo uamuzi ulofanywa wananchi hatuwezi kukubaliana nao mpaka tupewe ufafanuzi wa kina.
Ukweli tuna uhaba wa Madaktari, ila sio kwamba hawapo, Serikali ndio haijajiri, wengi wapo mtaani tu. Wachache wako na ajira, ni kama ishu ya Walimu, uhaba kwenye shule ni mkubwa ila wengi wapo mtaani bila ajira.
 
Hao bado Wapo mkuu ni College bado hizo
Hapana Mkuu!Mwenge waliondoka huku tangu 2014 nafikiri,kutoka Mwenge college of education kuwa Mwenge Catholic University (MWECAU).
 
Tanzania ni Nchi yenye watu wenye roho mbaya sana wakati wangeweza kuwaita hao madaktari wakafanya huo mtihani wenye mashaka nao sema wanajikinga kwenye kivuli cha ukalimu wa kinafiki watu wana roho mbaya kumzidi hata huyo shetani wao ....hivyo viseneti vyao vikikaa kwenye kutunga kitu hakuna kitu cha maana watakuja nacho ni upuuzi mtupu...kwa maamuzi ya hovyo ya namna hiyo wataendelea kuwa na hao watoa maamuzi ya hovyo mpaka lini?
 
Kutorudisha nakala za masomo......
Naomba mtu anieleweshe hapo kosa lipo wapi? Na ina maana chuo inazo orijino lakini inadai nakala (copy) walizonazo wahitimu zirudishwe.

Je kitaaluma imekaaje hii

Nadhani hao wahitimu wanadaiwa ada na chuo , ndio maana walifanya mpango kuchukua nakala kinyemela
 
Tanzania ni Nchi yenye watu wenye roho mbaya sana wakati wangeweza kuwaita hao madaktari wakafanya huo mtihani wenye mashaka nao sema wanajikinga kwenye kivuli cha ukalimu wa kinafiki watu wana roho mbaya kumzidi hata huyo shetani wao ....hivyo viseneti vyao vikikaa kwenye kutunga kitu hakuna kitu cha maana watakuja nacho ni upuuzi mtupu...kwa maamuzi ya hovyo ya namna hiyo wataendelea kuwa na hao watoa maamuzi ya hovyo mpaka lini?
Nenda kwa Millard Msikilize VC wa SAUT Prof Mahalu ameeleza vizuri sana, Watu wamebembekezwa toka 2020/2021 wapo waliotii na wanaendelea kutii na wanapokelewa ila wachache ndio wamegoma
 
Nenda kwa Millard Msikilize VC wa SAUT Prof Mahalu ameeleza vizuri sana, Watu wamebembekezwa toka 2020/2021 wapo waliotii na wanaendelea kutii na wanapokelewa ila wachache ndio wamegoma
Hilo kosa ni la nani ni wanafunzi wanatakiwa kuweka matokeo kwa usahihi au?
 
Watanzania wanajua laumu tu na kukurupuka

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Mwanzoni nilikuwa naona CHUO kina kosa ila baada ya kumsikiliza vizuri VC na namna ambavyo ameelezea hilo suala kiundani nimeona ni ubishi tu ambao hauna maana

Na amesisitiza Duniani kote Shahada ni Mali ya chuo inaweza kukuvua muda wowote ikiona inafaa ila kwa utaratibu ambao upo wazi na unaotambulika mkuu
 
Uongozi pia unakosa na ndio maana tayari viongozi wawili wa juu walishaachishwa kazi mkuu, Ila haihalalishi na wao wakaidi
Mkuu mimi naona wamefanya kienyeji sana je kwa wanafunzi wanaodhaminiwa na kama walitoka Nje ya Nchi inakuaje hapo ?
 
Mkuu mimi naona wamefanya kienyeji sana je kwa wanafunzi wanaodhaminiwa na kama walitoka Nje ya Nchi inakuaje hapo ?
Toka 2020/2021 taarifa haiwezi kukufikia mkuu wametoa tangazo zaidi ya mara 3 mkuu Almunus huwa mnanjia zenu za kupashana habari kuhusu chuo na darasa lenu kwa ujumla unafikiri hawakuiona hiyo taarifa!!

Pande zote zinamakosa mkuu kubali tu na baadhi ya Graduates wanamakosa!!
 
Inamana hawa wakulungwa wamekaza kurudisha hizo transcript chuoni, sasa je mfano watu wameramba asali tayari vitengo mbali mbali vp kuhusu kazi zao watasimamishwa au wataachishwa mana sielewi embu fafanueni ili jambo wajuzi

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom